Kununua Super Chat au Super Sticker

Kumbuka: Baadhi ya Super Chat, Super Stickers, au Shukrani Moto mpya zinazonunuliwa kwenye programu ya YouTube katika Android zitatozwa kupitia Google Play. Mabadiliko haya hayaathiri bei au gharama, yanaathiri tu sehemu ambako ununuzi unatozwa. Unaweza kwenda kwenye pay.google.com ili uangalie gharama mpya na jinsi unavyotozwa.

Boresha gumzo la moja kwa moja ukitumia Super Chat au Super Stickers. Unaponunua na kutuma Super Chat, unaweza kuangazia ujumbe wako ndani ya mipasho ya gumzo la moja kwa moja. Ukiwa na Super Stickers, utaona ujumbe dijitali au uliohuishwa ambao unaibuka wakati wa mipasho ya gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu upatikanaji na masharti ya mfumo. Watayarishi hupokea kiasi kikubwa cha mgawo wa mapato ya Super Chat na Super Stickers.

Kununua Super Chat au Super Sticker

Fuata maagizo haya ili ununue Super Chat au Super Sticker kwenye kompyuta yako:
  1. Bofya alama ya dola kwenye gumzo la moja kwa moja. Ni lazima gumzo la moja kwa moja lionekane.
  2. Chagua moja kati ya yafuatayo:​
    1. Super Sticker kisha pata kifurushi unachopenda kisha chagua kibandiko mahususi ili ununue.
    2. Super Chat kisha ili uchague kiasi, buruta kitelezi au uandike thamani unayopenda kisha ongeza ujumbe wa hiari.
      • Rangi na kiasi cha wakati ulichobandika katika sehemu ya juu ya mipasho ya gumzo hubadilika kulingana na kiasi unachotumia. 
  3. Bofya Nunua na utume.
  4. Ili ukamilishe ununuzi, fuata maagizo hayo.

Baada ya kununua Super Chat au Super Sticker:

  • Kulingana na thamani ya ununuzi, tunaweza kubandika Super Chat au Super Sticker yako juu ya mipasho ya gumzo la moja kwa moja. Sehemu ya gumzo ya kuhesabu muda itaonyesha muda ambao Super Chat au Super Sticker zitabandikwa. Mtayarishi anaweza kumaliza gumzo la moja kwa moja au mtiririko mubashara kabla ya kuisha kwa muda wako katika sehemu ya gumzo. Super Stickers na Super Chat hazihamishwi kati ya video.
  • Kama sehemu ya ununuzi wako wa Super Chat au Super Sticker, tunaweza kutangaza kwa umma hatua muhimu ya ununuzi, kama vile mara ya kwanza unaponunua Super Chat, ili wengine waweze kusherehekea hatua yako muhimu. Kabla ya kununua, utapata toleo la kukagua la tangazo la kusherekea hatua muhimu. Mafanikio yako yanatokana na historia yako ya ununuzi, inayopatikana katika sehemu ya Shughuli Zangu.
  • Mtayarishi au watazamaji wengine wanaweza kutumia Super Chat yako kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja kwa “Kuiwekea emoji ya moyo” au “Kuiwekea alama ya nimeipenda”. Ikiwa mtumiaji “ataweka alama ya nimeipenda” kwenye ujumbe wa Super Chat, itaonekana kwenye mtiririko mubashara, lakini haitahifadhiwa wakati huo au baada ya hapo, k.m., kwenye kumbukumbu ya mtiririko mubashara.
Vidokezo:
  • Super Chat au Super Sticker yako, jina la chaneli, picha ya wasifu na gharama huonekana kwa umma.
  • Sawa na vitu vingine kwenye YouTube, lazima Super Chat na Super Stickers unazotuma zitii Mwongozo wa Jumuiya yetu.
  • YouTube itadokeza idadi ya ununuzi unaofanya, ili uweze kutambulika kwa umma kutokana na hatua muhimu za ununuzi. Iwapo hungependa kushiriki katika hatua muhimu za ununuzi, nenda kwenye Shughuli Zangu ili uondoe data yako ya historia ya ununuzi.

Vikomo vya ununuzi

Ununuzi usiozidi USD $5 (au kulingana na kiasi cha sarafu ya eneo uliko) hautaonekana katika sehemu ya gumzo.

Kulingana na nchi au eneo uliko, kikomo cha ununuzi cha kila siku na kila wiki kitatofautiana. Kwa jumla, unaweza kutumia hadi USD $500 kwa siku au USD $2,000 kwa wiki (au kiasi sawa cha sarafu ya nchi ulimo) kwenye:

  • Super Chats
  • Super Stickers
  • Shukrani Moto
  • Zote 3 pamoja

Udhibiti wa gumzo

Ujumbe wote wa gumzo, zikiwemo picha na maandishi, unaweza kudhibitiwa na watayarishi na YouTube. Magumzo yanayodhibitiwa yanaweza kuondolewa yasionekane. Wewe na/au wengine mnaweza kuyaondoa wakati wowote, kwa sababu yoyote na bila kutoa arifa.

Unaweza pia kuondoa Super Chat au Super Sticker ambayo umenunua na uliyotuma. Bofya Zaidi '' kisha Ondoa.

Hutarejeshewa pesa za Super Chat na Super Stickers zilizodhibitiwa au kuondolewa. Iwapo una shaka, unaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi wa YouTube au kuangalia sera yetu ya kurejesha pesa.

Sera za Super Chat na Super Sticker

Sawa na vitu vingine kwenye YouTube, lazima Super Chat na Super Stickers unazotuma zitii Mwongozo wa Jumuiya yetu.

Ni lazima pia uendelee kutii sheria zote zinazotumika kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya YouTube. Pesa zinazotumiwa kwenye Super Chat na Super Stickers zinaweza kushughulikiwa kwa njia tofauti kulingana na sheria zinazotumika kwako na shughuli zako. Tafadhali kumbuka kuwa Super Chat na Super Stickers si zana za ufadhili au kuchangisha pesa. Una wajibu wa kufahamu na kutii kikamilifu sheria zote zinazotumika - hata kama unaweza au huwezi kununua Super Chat au Super Stickers.

Kutuma malalamiko ya hakimiliki za Super Stickers

Iwapo unafikiri kuwa Super Sticker inakiuka hakimiliki yako, unaweza kutuma arifa ya ukiukaji wa hakimiliki. Kufanya hivyo kutaanzisha mchakato wa kisheria. Ili utume malalamiko, utahitaji kuweka URL ya Super Sticker ambayo unafikiri kuwa unakiuka hakimiliki yako.

Ili uwasilishe malalamiko, utahitaji kutuma barua pepe iliyo na maelezo yafuatayo kwa copyright@youtube.com:

  1. Maelezo yako ya mawasiliano
    Utahitaji kutoa maelezo ambayo yataturuhusu sisi na aliyepakia Super Sticker yoyote unayoondoa ili tuwasiliane nawe kuhusu malalamiko yako, kama vile anwani ya barua pepe, anwani ya mahali halisi au nambari ya simu.

  2. Maelezo ya kazi ambayo unaamini kuwa hakimiliki yake imekiukwa
    Katika malalamiko yako, hakikisha kuwa unafafanua kwa njia dhahiri na kamilifu maudhui yaliyo na hakimiliki ambayo unalenga kulinda Ikiwa kazi nyingi zenye hakimiliki zinajumuishwa katika malalamiko yako, sheria huruhusu orodha wakilishi ya kazi kama hizo.

  3. Kila URL mahususi ya Super Sticker inayodaiwa kukiuka haki
    Ni lazima malalamiko yako yawe na URL mahususi ya Super Sticker ambayo unaamini kuwa inakiuka haki zako, au hatutaweza kuitambua na kuiondoa. Maelezo ya jumla kuhusu Super Sticker hiyo, kama vile jina la mtumiaji au URL ya kituo, hayatoshi.

    • Ili upate URL: Kwenye kompyuta, nenda kwenye Super Sticker katika mipasho ya gumzo au utaratibu wa kununua Super Sticker kisha bofya kulia kwenye Super Sticker kisha Nakili Picha ya Anwani.

  4. Ni lazima ukubali na ujumuishe taarifa ifuatayo:
    “Nina nia njema ya kuamini kuwa utumiaji wa nyenzo kwa namna inayolalamikiwa haujaidhinishwa na mwenye hakimiliki, wakala wake au sheria.”

  5. Na taarifa ifuatayo:
    "Maelezo yaliyo katika arifa hii ni sahihi na nitaadhibiwa kwa kusema uwongo, mimi ni mmiliki au wakala aliyeidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya mmiliki, wa haki ya kipekee ambayo inadaiwa kukiukwa.”

  6. Sahihi yako
    Kukamilisha malalamiko kunahitaji sahihi halisi au ya kielektroniki ya mwenye hakimiliki au mwakilishi aliyeidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba yake. Ili kutimiza masharti haya, unaweza kuandika jina lako rasmi kamili (jina la kwanza na la mwisho, wala si jina la kampuni) ili liwakilishe sahihi yako katika sehemu ya chini ya malalamiko yako.

Maeneo ambako Super Chat na Super Stickers zinapatikana

Super Chat na Super Stickers zinapatikana katika maeneo yafuatayo:
  • Aljeria
  • Samoa ya Marekani
  • Ajentina
  • Aruba
  • Australia
  • Austria
  • Bahareni
  • Belarusi
  • Ubelgiji
  • Bermuda
  • Bolivia
  • Bosnia na Hezegovina
  • Brazili
  • Bulgaria
  • Kanada
  • Visiwa vya Cayman
  • Chile
  • Kolombia
  • Kostarika
  • Korasia
  • Kuprosi
  • Jamhuri ya Zechia
  • Denmaki
  • Jamhuri ya Dominika
  • Ekwado
  • Misri
  • Elsavado
  • Estonia
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Guyana ya Ufaransa
  • Polinesia ya Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ugiriki
  • Guadalupe
  • Guam
  • Gwatemala
  • Hondurasi
  • Hong Kong
  • Hangaria
  • Aisilandi
  • India
  • Indonesia
  • Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Japani
  • Yordani
  • Kenya
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Lebanoni
  • Lishenteni
  • Litwania
  • Lasembagi
  • Masedonia
  • Malesia
  • Malta
  • Meksiko
  • Moroko
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Nikaragua
  • Naijeria
  • Visiwa vya Mariana Kaskazini
  • Norwe
  • Omani
  • Panama
  • Papua
  • Paragwai
  • Peru
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Ureno
  • Pwetoriko
  • Katari
  • Romania
  • Saudia
  • Senegali
  • Sabia
  • Singapoo
  • Slovakia
  • Slovenia
  • Afrika Kusini
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani
  • Tailandi
  • Uturuki
  • Visiwa vya Turks na Caicos
  • Visiwa vya Virgin vya Marekani
  • Uganda
  • Falme za Kiarabu
  • Uingereza
  • Marekani
  • Urugwai
  • Vietinamu

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16179001727250977401
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false