Kutazama YouTube kwenye Nintendo Switch

Sasa unaweza kutazama video za YouTube kwenye Nintendo Switch. Unaweza kuona vituo unavyofuatilia, kutafuta maudhui na kutumia kifaa cha mkononi kama kidhibiti cha mbali.

Pakua programu ya YouTube

Ingia au uondoke katika akaunti ya YouTube

  1. Nenda kwenye Ingia katika akaunti.
  2. Ingia kwa kutumia Akaunti yako ya Google. Iwapo una zaidi ya Akaunti moja ya Google, hakikisha unachagua akaunti unayotumia na YouTube.
  3. Baada ya kuingia katika akaunti, unaweza kuona orodha ya utambulisho wa Google unaohusiana na akaunti yako. Hakikisha unachagua akaunti ambayo imeunganishwa kwenye chaneli yako ya YouTube. Ukichagua Akaunti ya Biashara ambayo haina chaneli ya YouTube, hutaweza kuingia katika akaunti.
Kumbuka: Unapofungua programu, utaombwa uchague akaunti ya Nintendo ya kutumia. Unaweza kutumia akaunti yoyote ya Nintendo ili kutumia YouTube.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutenganisha akaunti yako kwenye Nintendo Switch yako.

Vidhibiti vya video

Gundua YouTube kupitia usukani wa kushoto au D-pad kwenye kidhibiti chochote kilichounganishwa. Kwa sasa ishara za kutelezesha kidole haziruhusiwi katika programu ya YouTube.
Baada ya kuchagua video ya kucheza, upau wa kidhibiti cha kichezaji utaonekana unaokuruhusu kufanya yafuatayo:
  • Ukurasa wa kwanza: Rudi kwenye ukurasa wa kwanza kwa kugusa B.
  • Kucheza Play icon: Cheza au uendelee kucheza video yako. Unaweza pia kugusa A.
  • Manukuu : Onyesha manukuu ya video, iwapo yapo.

Unapocheza video, chagua “Vitendo Zaidi” ili upate chaguo zaidi:

  • Kufuatilia kituo.
  • Kukadiria video.
  • Kuripoti video kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Kumbuka: Utendaji wa picha ya skrini kwenye Nintendo Switch hautumiki kwenye programu ya YouTube.

Kutafuta video

Kwenye menyu kuu ya YouTube, bonyeza X ili utafute video. Unapotafuta, bonyeza Y ili uweke nafasi, na B ili ufute herufi.
  • Kuvinjari video: Unapotafuta, video zinazohusiana zitaonekana katika sehemu ya chini ya skrini. Ili uvinjari matokeo ya video, bonyeza kulia au kushoto kwenye D-pad au kitufe cha kushoto.
  • Kubadilisha utafutaji wako: Bonyeza X tena au ubofye aikoni ya kibodi ili ufungue kibodi ya kuandikia.
Kumbuka: Kipengele cha skrini ya kugusa hufanya kazi na kibodi ya Tafuta wakati kifaa kinatumiwa katika hali ya kushikiliwa kwa mkono.

Kufuta historia ya Video ulizotazama na mambo uliyotafuta

Ili ufute historia ya video ulizotazama au mambo uliyotafuta:
  1. Nenda kwenye Mipangilio .
  2. Chagua Futa historia ya video ulizotazama au Historia ya mambo uliyotafuta.

Kitendo hiki kitafuta historia ya video ulizootazama au mambo uliyotafutw kwenye akaunti yako katika vifaa vyote na historia ya utazamaji wa hadithi zako.

Vidhibiti vya Wazazi na Kuingia katika Akaunti kwenye Nintendo

Programu ya Nintendo Switch ina Vidhibiti vya Wazazi katika mipangilio ya mfumo wa dashibodi. Ikiwa umewasha Vidhibiti vya Wazazi, huenda programu ya YouTube ikafungwa.

Kuwasha au kuzima Vidhibiti vya Wazazi kwenye Nintendo Switch yako:

  1. Nenda kwenye Mipangilio ya Mfumo.
  2. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  3. Chagua Mipangilio ya Vidhibiti vya Wazazi.
  4. Chagua Nimesakinisha programu. Nini kinafuata? au Sina kifaa mahiri! kisha ufuate vidokezo.
  5. Chagua Kiwango cha Kudhibiti unachopendelea.

Kwa Viwango vya Kudhibiti vya “Vijana” na “Watoto”, programu ya Nintendo Switch imefungwa. Kwa “Vijana” na “Haijadhibitiwa”, programu imefunguliwa.

Kumbuka: Iwapo ungependa kuwasha Vidhibiti vya Wazazi lakini si kwa programu ya YouTube, nenda kwenye Kiwango cha Kudhibiti kisha Mipangilio Maalum kisha Programu Inayodhibitiwa.

Kuoanisha kifaa chako cha mkononi

Tumia kifaa chako cha mkononi kama kidhibiti cha mbali. Unaweza kukioanisha kupitia m.youtube.com, programu ya YouTube ya Android au programu ya YouTube ya iOS.

Tazama maudhui uliyonunua

Unaweza kuona na kutazama maudhui uliyoyanunua katika kichupo cha Maktaba cha programu ya YouTube.
Kumbuka: Sasa hivi, huwezi kununua maudhui moja kwa moja kwenye kifaa.

Kutazama video inayozunguka digrii 360

Unaweza kutazama video za mwonekano wa digrii 360 kwenye Nintendo Switch. Unapotazama video zinazozunguka kwa digrii 360, usukani wa kushoto na kulia kwenye kidhibiti kilichoambatishwa unaweza kutumiwa kugeuza video.

Ubora wa video

Katika hali ya kushikiliwa na mkono, skrini iliyojumuishwa ina ubora wa juu zaidi wa 720p. Katika hali iliyopachikwa, ubora wa juu zaidi ni 1080p.
Ili ubadilishe ubora wa video ukitazama:
  1. Katika kicheza video, chagua Zaidi 3 dot menu icon.
  2. Chagua Ubora .
  3. Chagua ubora wa video unaopendelea.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16754770049925536469
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false