Taarifa kwa watayarishaji

Tumia makala haya ili kupata habari kuhusu mihtasari ya taarifa kwa watayarishi. Kwa mada nyingine, angalia makala haya:

Taarifa za hivi majuzi

Taarifa kutoka wiki 2 zilizopita

Studio ya YouTube
  • Mipangilio ya maudhui yaliyobadilishwa: Kuanzia tarehe 18 Machi 2024, duniani kote utahitajika kufumbua katika utaratibu wa kupakia ikiwa maudhui unayopakia yamebadilishwa kwa kiasi kikubwa au yamezalishwa kwa njia ya usanisi. Zana hii itapatikana kwanza katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta kisha ipanuliwe katika toleo la Studio ya YouTube linalotumika kwenye vifaa vya mkononi. Pata maelezo zaidi.
  • Sehemu ya "Klipu maarufu za jumuiya": Unaweza kuonyesha klipu maarufu za video zako kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. Wewe au jumuiya yako mnaweza kutayarisha klipu hizi. Zikishawekwa kwenye kichupo chako cha Ukurasa wa kwanza, klipu hizo huonekana kwa umma na kupangwa kulingana na umaarufu na jinsi zilivyotayarishwa hivi majuzi. Pata maelezo zaidi.
  • Maudhui uliyopakia katika programu ya Vifaa vya Mkononi ya Studio: Sasa unaweza kupakia maudhui na kuweka hali ya uchumaji wa mapato ya video na Video Fupi moja kwa moja katika Studio ya YouTube kwenye vifaa vyako vya mkononi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakia video na Video Fupi ukitumia Studio ya YouTube. 
Takwimu za YouTube
  • Utazamaji kwenye Mtiririko Mubashara Ulio Wima: Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi watazamaji wanavyogundua Mtiririko Mubashara Ulio Wima ukitumia vyanzo vya watazamaji. Unaweza kufahamu mahali Mtiririko wako Mubashara uliochapishwa Ulio Wima unapochezewa na vyanzo vya watazamaji wako katika sehemu ya chanzo cha watazamaji ya Mpasho Mubashara Ulio Wima.
Video Fupi za YouTube
  • Dream Track: Dream Track kwenye Video Fupi ni zana ya majaribio ya kutayarisha nyimbo ambayo huwawezesha watayarishi kutunga nyimbo za kipekee za sekunde 30 wakitumia sauti za wasanii wanaoshiriki. Zana hii huleta pamoja utaalamu wa Google DeepMind na watafiti wabunifu zaidi wa YouTube walio na utaalamu wa washirika wetu katika sekta ya muziki, ili kufungua njia mpya kwa ajili ya watayarishi katika Video Fupi ili kutayarisha na kushirikiana na wasanii. Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana tu kwa kikundi kidogo cha watayarishi nchini Marekani na kwenye vifaa fulani vya mkononi. Tunatarajia kujumuisha maoni kutoka kwenye jaribio hili katika fursa za bidhaa zinazoweza kuwanufaisha wasanii na watayarishi. Hadhira kote ulimwenguni zinaweza kutumia nyimbo kama zilivyo ili kuandaa miseto ya Video zao Fupi.

Taarifa nyingine

Video ya Muhtasari wa kila mwezi kutoka Chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube

Video ya Muhtasari wa kila mwezi wa Watayarishi wa YouTube

 

Taarifa za awali

Taarifa za miezi 6 iliyopita

Novemba 2023

YouTube Music

Takwimu za YouTube

  • Vipimo kulingana na aina ya maudhui: Sasa unaweza kuangalia takwimu za watazamaji wapya na wanaorudi tena kulingana na aina ya maudhui ili ufahamu aina gani za maudhui wanayotazama kwenye chaneli yako. Pata maelezo zaidi.
Studio ya YouTube
  • Sehemu ya "Kwa ajili yako": Sehemu ya "Kwa ajili yako" kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako hukuwezesha kushiriki mseto wa maudhui kutoka kwenye chaneli yako yaliyowekewa mapendeleo ili kuwafaa watazamaji binafsi. Unaweza kuanza kuandaa sehemu ya “Kwa ajili yako” kwenye chaneli yako kuanzia tarehe 8 Novemba, 2023. Hadhira yako itaiona kuanzia tarehe 20 Novemba, 2023. Pata maelezo zaidi.
  • Maelezo mapya ya malipo katika programu ya Studio: Tunawaletea toleo jipya la Beta linaloleta maelezo ya malipo kwenye kichupo cha 'Chuma Mapato' cha programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube. Watayarishi wanaotimiza masharti wanaweza kuangalia hatua walizopiga kwa ajili ya malipo yanayofuata na historia yao ya malipo. Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la beta katika chapisho letu la jukwaa.
  • Kichupo cha Ukurasa wa mwanzo cha chaneli ya YouTube kilichorahisishwa: Kichupo kilichosasishwa cha Ukurasa wa mwanzo cha chaneli ya YouTube huficha vichupo visivyo na chochote na kuondoa vichupo vya "Kuhusu" na "Chaneli" ili kurahisisha hali ya utumiaji. Maelezo ambayo awali yalipatikana kwenye vichupo hivi yanapatikana katika sehemu nyingine kwenye chaneli yako. Unaweza kupata maelezo ya chaneli yako kwenye kichwa cha chaneli na chaneli zozote zilizoangaziwa kwenye kichupo cha Ukurasa wa mwanzo.
  • Kuonyesha viungo kwenye chaneli yako:  Sasa viungo vya watayarishi vilivyo kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza cha chaneli vinaonyeshwa kwa udhahiri kwenye kichwa cha wasifu wa Chaneli karibu na kitufe cha "Fuatilia". Watayarishi hawataweza tena kuonyesha viungo kwenye bango.
  • Tazama Muhtasari wako wa Msanii: Tumia Muhtasari wako wa Msanii kusherehekea mafanikio ya mwaka mzima na upate maelezo kuhusu jinsi mashabiki wanavyosikiliza muziki wako kwenye YouTube. Kisha, shiriki mafanikio yako kwenye mitandao ya kijamii ukitumia kadi maalum za data. Pata maelezo zaidi kuhusu Muhtasari wako wa Msanii.

Oktoba 2023

Uchumaji wa mapato

  • Kipengele cha YouTube cha Nunua kupitia Google kinaondolewa: Kuanzia tarehe 26 Oktoba 2023, kipengele cha YouTube cha Nunua kupitia Google, kinachotumika kulipia bidhaa za ndani ya programu kwenye YouTube, hakitapatikana tena nchini Marekani. Oda zozote zitakazowekwa tarehe 25 Oktoba 2023 au zilizowekwa kabla ya tarehe hiyo bado zitatekelezwa. Hivi karibuni, tutazipa kipaumbele njia nyinginezo ili kuhakikisha kuwa tunatoa mbinu zinazofaa za kufanya malipo kwenye tovuti kwa ajili ya wauzaji wa rejareja, watayarishi na watazamaji wetu.

Septemba 2023

Studio ya YouTube
  • Klipu kwenye Studio ya YouTube: Sasa watayarishi wanaweza kutazama, kudhibiti na kushiriki Klipu katika Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Agosti 2023

Taarifa nyingine

  • Mabadiliko kuhusu viungo kwenye YouTube: Ili kupunguza taka na majaribio ya ulaghai, viungo vilivyo katika maoni kwenye Video Fupi za YouTube na maelezo ya Video Fupi vitakuwa visivyoweza kubofyeka kuanzia tarehe 31 Agosti, 2023-mabadiliko haya yatafanyika hatua kwa hatua. Pia, tutakomesha kuonyesha viungo kwenye bango kuanzia tarehe 10 Agosti, 2023 na kuanzisha njia mpya ya kuangazia viungo muhimu kwenye ukurasa wa chaneli yako. Unaweza kuanza kutayarisha viungo vya wasifu wa chaneli tarehe 10 Agosti na hadhira yako itaviona kuanzia tarehe 23 Agosti. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya.
  • Kipengele kipya cha kina kwenye YouTube: Kuanzia tarehe 17 Agosti 2023, unaweza kuhariri Video zako Fupi ili ujumuishe kiungo cha video kutoka kwenye chaneli yako. Kiungo kitaonekana kwenye kichezaji cha Video Fupi ili kisaidie kuelekeza watazamaji kutoka kwenye Video zako Fupi kwenda katika maudhui yako mengine ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Julai 2023

Studio ya YouTube
  • Upanuzi wa ruhusa za chaneli: Watumiaji wenye ruhusa wanaweza kuchukua hatua zinazohusiana na chaneli yako moja kwa moja kwenye YouTube pamoja na Studio ya YouTube. Sasa, watumiaji waliokabidhiwa uwezo wa kudhibiti au kuhariri wanaweza kutayarisha Video fupi, kuweka chapisho, kudhibiti orodha ya kucheza au kutoa maoni kwenye video yoyote ya YouTube kama mmiliki. Pata maelezo zaidi.

Juni 2023

Uchumaji wa mapato
  • Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube sasa unapatikana kwa watayarishi wote walioko Marekani ambao wanatimiza masharti: Kuanzia Tarehe 13 Juni, 2023, Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube sasa unapatikana kwa watayarishi wote walioko Marekani ambao wanatimiza masharti. Kwa muhtasari, Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube huwaruhusu watayarishi kuwekea lebo bidhaa za chapa na wauzaji maarufu wa rejareja zilioangaziwa kwenye video zao. Pata maelezo zaidi.
Takwimu za YouTube
Kadi mpya ya ‘Watazamaji kwenye miundo mbalimbali’ katika Takwimu za YouTube: Kwenye Kichupo cha maudhui katika Takwimu za YouTube, sasa unaweza kuona kama na idadi ya watazamaji wako wanaorejea mara nyingine wanaotazama zaidi ya muundo mmoja na jinsi gani muingiliano ulivyo mkubwa. Hii inapatikana kwa Video, Video Fupi, na za moja kwa moja. Pata maelezo zaidi.
Vipimo vipya vya mpango wa washirika wa ununuzi katika Studio: Ndani ya kichupo cha Mapato kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi, sasa unaweza kupata data zaidi ya mpango wa washirika wa ununuzi kwenye sehemu ya "Mshirika.” Vipimo hivi vipya vitakupa maarifa kuhusu makadirio ya mapato yako, jumla ya mauzo, idadi ya oda na utendaji wa bidhaa kwa ujumla. Pata maelezo zaidi.

Mei 2023

Uchumaji wa mapato
  • Punguzo la asilimia 25 kwa bidhaa zilizo kwenye duka lako la Spring: Tunafadhili punguzo la asilimia 25 kwa bidhaa zozote zilizo kwenye duka lako la Spring. Ofa hii inatolewa kulingana na wanaotangulia mapema na inapatikana tu kwa muda mfupi. Ili unufaike na ofa hii, pata msimbo wako na uanze kuweka lebo kwenye bidhaa zako katika maudhui ili ushiriki ofa na mashabiki.

  • Skrini za mwisho za bidhaa zinaondolewa: Hapa YouTube, tunataka kuhakikisha kuwa unazingatia zaidi vipengele vinavyowashirikisha watazamaji kwenye bidhaa zako ili uweze kukuza biashara yako. Ili tuendelee kuboresha hali ya Ununuzi kwa watayarishi na watazamaji, skrini za mwisho hazitatumika tena. Ili ushirikishe bidhaa zako, tayarisha maudhui yanayoonyesha thamani ya bidhaa hizo kisha uweke lebo kwenye bidhaa zilizoangaziwa ili hadhira yako iweze kununua.

Takwimu za YouTube
  • Uchanganuzi mpya wa mapato kwenye Takwimu za YouTube: Sasa unaweza kwenda kwenye kichupo cha Mapato katika Takwimu za YouTube ili uone mapato yako yalivyochanganuliwa kulingana na Matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama, Matangazo kwenye Mipasho ya Video Fupi, Uanachama, Supers, Maduka Yaliyounganishwa na Washirika wa Ununuzi kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.

  • Ripoti ya miundo mipya ya jinsi watazamaji wako wanavyotazama kwenye Studio ya YouTube: Kwenye kichupo cha Hadhira, sasa unaweza kutafuta ripoti inayoonyesha ni miundo ipi (ya Video, Video Fupi na Mubashara) ambayo hadhira yako ilitazama mara kwa mara kwenye vituo vingine katika siku 28 zilizopita. Data hii inaweza kukusaidia kutoa taarifa ya mkakati wa maudhui yako. Pata maelezo zaidi.

Taarifa nyingine
  • Kipengele cha Hadithi hakitapatikana tena kuanzia tarehe 26 Juni: Kuanzia tarehe 26 Juni, kipengele cha Hadithi hakitapatikana tena na Hadithi zozote ulizochapisha tarehe 26 Juni zitaondolewa siku 7 baada ya kushirikiwa kwa mara ya kwanza. YouTube itavipatia kipaumbele vipengele vingine muhimu ili kukusaidia kufanikiwa zaidi na kukuza jumuiya yako. Idadi ya mara ambazo Hadithi zimetazamwa bado itaonekana katika Takwimu za YouTube. Pata maelezo zaidi.

Aprili 2023

YouTube Music Kutiririsha mubashara
  • Miitikio inayopatikana katika gumzo la moja kwa moja kwenye vifaa vya iPhone & iPad: Watazamaji wanapotazama mtiririko mubashara kwenye kifaa cha iPhone au iPad, wanaweza kujibu papo hapo kwa kugusa mwitikio unaolingana na hisia zao. Pata maelezo zaidi.
Video Fupi za YouTube
  • Miseto ya Klipu: Sasa unaweza kutayarisha mseto wa klipu kuwa Video Fupi. Bofya hapa ili upate maelezo kuhusu kutayarisha Video Fupi ukitumia maudhui mseto.

Machi 2023

Studio ya YouTube
  • Ruhusa za chaneli zinapatikana kwenye programu ya Studio ya YouTube: Sasa unaweza kudhibiti uliowawekea majukumu kupitia ruhusa za chaneli katika programu ya Studio ya YouTube. Waliowekewa majukumu, sasa wanaweza kuchukua hatua kwenye Studio katika kompyuta, kwenye programu ya Studio au katika programu ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9297265847863990267
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false