Kutia ukungu kwenye video zako

Unaweza kutia ukungu katika sehemu za video yako kwenye kompyuta katika Studio ya YouTube.

Kumbuka: Huenda usiweze kuhifadhi mabadiliko kwenye video ambayo haijahaririwa na imetazamwa zaidi ya mara 100,000, isipokuwa kutia ukungu kwenye nyuso. Kizuizi hiki hakitumiki katika chaneli zilizo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Fungua kihariri cha video

Fungua kihariri cha video ili utie ukungu kwenye sehemu ya video yako.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya jina au kijipicha cha video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kihariri.

Kutia ukungu kwenye nyuso

  1. Chagua Tia ukungu , kisha uchague Tia Ukungu kwenye Nyuso.
  2. Uchakataji ukikamilika, chagua nyuso ambazo ungependa kutia ukungu, kisha ubofye TUMIA.
  3. Bofya na uburute kisanduku ili urekebishe ukungu.
  4. Bofya HIFADHI.

Kutia ukungu maalum

  1. Chagua Tia ukungu , kisha uchague Tia Ukungu Maalum.
  2. Bofya na uburute kisanduku ili urekebishe ukungu.
  3. Bofya HIFADHI.

Chaguo zaidi

  • Kusogeza kisanduku cha kutia ukungu mahali tofauti: Bofya na uburute ndani ya kisanduku.
  • Kubadilisha umbo la kutia ukungu: Chagua Mstatili au Duaradufu kama umbo lako la kutia ukungu.
  • Kubadilisha ukubwa wa sehemu inayotiwa ukungu: Bofya na uburute pembe yoyote ya kisanduku ili utie ukungu kwenye sehemu kubwa au ndogo zaidi.
  • Kubadilisha wakati ukungu utakapowekwa: Bofya na uburute ncha za kipengele cha wakati ili uweke wakati ukungu utakapoanza na utakapomaliza kuwekwa.
  • Kuruhusu sehemu iliyotiwa ukungu isogezwe: Chagua Fuatilia kipengee ili uhakikishe kuwa sehemu iliyotiwa ukungu inasogezwa.
  • Kuzuia sehemu iliyotiwa ukungu isisogezwe kabisa: Chagua Fanya sehemu yenye ukungu isibadilike ili uhakikishe kwamba sehemu iliyotiwa ukungu inasalia mahali pamoja.
  • Kutia ukungu kwenye sehemu chache: Bofya na uburute visanduku vipya juu ya sehemu unazotaka kutia ukungu.
  • Unaweza kupakua video uliyohariri kisha uipakie tena ili uchapishe mabadiliko uliyofanya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6890980055869263535
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false