Kupunguza video zako

Unaweza kukata sehemu ya mwanzo, katikati au mwisho wa video yako kwenye kompyuta. Huhitaji kupakia video upya ili uipunguze. URL ya video, mara ilizotazamwa na maoni yatasalia vile vile. Kipengele hiki kinapatikana kwenye video zenye urefu usiozidi saa sita.

Jinsi ya Kupunguza na Kukata Video Zako ukitumia Kihariri cha Video katika Studio ya YouTube

Kumbuka: Huenda usiweze kuhifadhi mabadiliko kwenye video ambayo haijahaririwa na imetazamwa zaidi ya mara 100,000, isipokuwa kutia ukungu kwenye nyuso. Kizuizi hiki hakitumiki katika chaneli zilizo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Fungua kihariri cha video ili upunguze au uondoe sehemu ya video yako.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya jina au kijipicha cha video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kihariri.

Kupunguza sehemu ya mwanzo au mwisho wa video yako

 

  1. Chagua Punguza na ukate . Kisanduku cha buluu kitaonekana kwenye kihariri.
  2. Buruta pande za kisanduku hicho cha buluu. Acha kuburuta wakati kisanduku kimejumuisha sehemu ya video ambayo ungependa kuhifadhi. Chochote ambacho hakipo kwenye kisanduku kitaondolewa kwenye video.
  3. Bofya Hifadhi.

Kuondoa sehemu ya video yako

  1. Chagua Punguza na ukate , kisha ubofye KATA SEHEMU MPYA. Kisanduku chekundu kitaonekana kwenye kihariri.
  2. Buruta pande za kisanduku hicho chekundu. Acha kuburuta wakati kisanduku chekundu kimejumuisha sehemu ya video ambayo ungependa kuondoa. Chochote ambacho hakipo kwenye kisanduku chekundu kitasalia kwenye  video.
  3. Ili uthibitishe mabadiliko uliyofanya, chagua Kata .
  4. Bofya Hifadhi.

Ikiwa unataka kupunguza au kukata video yako katika wakati mahususi, unaweza kuweka wakati huo kwenye kisanduku. Ili ukague mabadiliko uliyofanya, chagua Kagua kwanza. Ili utendue kitendo cha kukata sehemu hiyo, bofya TENDUA. Unaweza kubofya ONDOA MABADILIKO wakati wowote ili ughairi mabadiliko uliyofanya.

Chaguo zaidi

  • Chagua Zaidi '' kisha Rejesha video ya awali ili uondoe mabadiliko yoyote ambayo hayajahifadhiwa uliyofanya kwenye rasimu yako.
  • Unaweza kupakua video uliyohariri kisha uipakie tena ili uchapishe mabadiliko uliyofanya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5944399595532462642
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false