Unaweza kupata zawadi za nje ya mfumo unapotazama mitiririko mubashara inayotimiza masharti kwenye YouTube kwa kuunganisha Akaunti yako ya Google na akaunti ya mshirika.
Vidokezo
- Huenda kipengele hiki kisitumike kwenye matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube.
- Kuna kikomo cha idadi ya orodha za video za umma ambazo chaneli inaweza kutayarisha kila siku katika YouTube Music, programu kuu ya YouTube na API ya YouTube. Unaweza kuongeza kikomo chako cha kila siku kwa kupata ufikiaji wa vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi.
Kuunganisha au kutenganisha akaunti zako
Kwenye mipangilio ya YouTube
Kuunganisha akaunti
- Ingia katika YouTube.
- Nenda kwenye picha yako ya wasifu
kisha uchague Mipangilio
.
- Nenda kwenye sehemu ya Programu zilizounganishwa.
- Bofya UNGANISHA karibu na mshirika ambaye ungependa kuunganisha.
- Ikiwa huna akaunti, fuata maagizo yaliyo kwenye tovuti ya mshirika ili ufungue akaunti. Kisha uanzie hatua ya 2.
- Fuata hatua za kuingia katika akaunti yako ya mshirika.
Kutenganisha akaunti
- Ingia katika YouTube.
- Bofya picha yako ya wasifu
kisha uchague Mipangilio
.
- Nenda kwenye sehemu ya Programu zilizounganishwa.
- Bofya TENGANISHA karibu na akaunti ya mshirika ambayo ungependa kuitenganisha.
Kwenye Ukurasa wa Kutazama wa YouTube
Kuunganisha akaunti
- Ingia katika YouTube.
- Nenda kwenye video au mtiririko mubashara wowote unaotimiza masharti ya kupata zawadi.
- Kwenye Ukurasa wa kutazama, bofya UNGANISHA
chini ya kichezaji.
- Fuata hatua ili uingie katika akaunti yako ya mshirika.
Kutenganisha akaunti
- Ingia katika YouTube.
- Nenda kwenye video au mtiririko mubashara wowote unaotimiza masharti.
- Kwenye Ukurasa wa kutazama, bofya ILIYOUNGANISHWA
chini ya kichezaji.
- Bofya TENGANISHA.
Kwenye Akaunti yako ya Google
Unaweza kutenganisha akaunti ya mshirika na Akaunti yako ya Google.
- Ingia katika akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myaccount.google.com/accountlinking.
- Karibu na akaunti ambayo ungependa kutenganisha, bofya Tenganisha.
Kumbuka: Baada ya kutenganisha akaunti zako, hutatimiza tena masharti ya kupata zawadi kwenye programu hiyo kwa kutazama video au mitiririko mubashara inayotimiza masharti. Huenda washirika wetu wakahifadhi kumbukumbu ya maudhui uliyotazama hata ikiwa umetenganisha akaunti. Rejelea akaunti yako ya mshirika ili udhibiti data yako.
Akaunti za washirika
ActivisionActivision ndiyo kampuni iliyounda Call of Duty. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Activision, tazama mitiririko mubashara mahususi ya Call of Duty ili ustahiki kupata zawadi.
Blizzard ndiyo kampuni iliyosanidi Battle.net, Overwatch na Hearthstone. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Battle.net, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya Blizzard ili utimize masharti ya kupata zawadi.
Electronic Arts
Epic Games
Electronic Arts (EA) ndiyo kampuni iliyounda FIFA na Madden. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya EA, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya EA ili ustahiki kupata zawadi.
Epic Games ndiyo kampuni iliyounda Fortnite. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Fortnite, tazama maudhui mahususi ya Kombe la Dunia la Fortnite ili ustahiki kupata zawadi.
Garena ndiyo kampuni iliyounda Free Fire. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Garena Free Fire, tazama maudhui mahususi ya Garena Free Fire ili ustahiki kupata zawadi.
Moonton ndiyo kampuni iliyosanidi Mobile Legends: Bang Bang (MLBB). Baada ya kuunganisha akaunti yako ya MLBB, tazama mitiririko mubashara mahususi ya MLBB ili utimize masharti ya kupata zawadi.
NBA
Ili upate zawadi za nje ya mfumo kutoka NBA, unganisha akaunti yako ya NFL ID. Unapounganisha akaunti yako ya NFL ID na Google, data yako ya akaunti hiyo ya NFL ID hutumika kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google. Maelezo yanaweza kujumuisha, lakini si tu, timu na wachezaji unaopenda na hali ya usajili wako wa League Pass. Maelezo haya yatatumiwa kuboresha matumizi yako kwenye Google kwa madhumuni yanayojumuisha, lakini si tu, kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google kama vile kupendekeza maudhui yanayofaa. Pata maelezo zaidi.
Unaweza kutenganisha wakati wowote katika Mipangilio ya YouTube.
NFL
Ili upate zawadi za nje ya mfumo kutoka NFL, unganisha akaunti yako ya NFL ID. Unapounganisha akaunti yako ya NFL ID na Google, data ya akaunti yako ya NFL itatumiwa kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google. Maelezo yanaweza kujumuisha, lakini si tu, jina, wachezaji, alama ambazo timu yako ya kidhahania imepata na maelezo kuhusu timu nyingine katika ligi yako ya kidhahania. Maelezo haya yatatumiwa kuboresha matumizi yako kwenye Google kwa madhumuni yanayojumuisha, lakini si tu, kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google kama vile kupendekeza maudhui yanayofaa.
Krafton (PUBG)
PlayerUnknown's Battlegrounds ya Vifaa vya Mkononi (PUBG ya Vifaa vya Mkononi)
Krafton ndiyo kampuni iliyounda PLAYERUNKNOWN’S BATTLEGROUNDS. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara inayotimiza masharti ili upate zawadi.
Tencent Games ndiyo kampuni iliyosanidi mchezo wa PlayerUnknown’s Battlegrounds (PUBG) wa Vifaa vya Mkononi. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara mahususi ya mchezo wa PUBG wa Vifaa vya Mkononi ili utimize masharti ya kupata zawadi.
Riot Games ndiyo kampuni iliyosanidi League of Legends, Legends of Runeterra na Teamfight Tactics. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara inayotimiza masharti ili upate zawadi.
Supercell ndiyo kampuni iliyounda Clash Royale. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya Supercell, tazama mitiririko mubashara mahususi ya Clash Royale au Ligi ya Clash Royale ili ustahiki kupata zawadi.
Ubisoft
Ubisoft ndiyo kampuni iliyosanidi Assassin's Creed na Rainbow Six ya Tom Clancy. Baada ya kuunganisha akaunti yako, tazama mitiririko mubashara mahususi ya michezo ya Ubisoft ili utimize masharti ya kupata zawadi.
Yahoo
Ukiwa umeunganisha akaunti yako ya Yahoo na Google, data ya akaunti yako ya Yahoo itatumiwa kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google Play. Maelezo yanaweza kujumuisha, lakini si tu, jina, wachezaji, alama ambazo timu yako ya kidhahania imepata na maelezo kuhusu timu nyingine katika ligi yako ya kidhahania. Maelezo haya yatatumiwa kuboresha matumizi yako kwenye Google kwa madhumuni yanayojumuisha, lakini si tu, kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji kwenye Google kama vile kupendekeza maudhui yanayofaa.
Maswali Yanayoulizwa Sana
Nimeunganisha akaunti zangu na ninatazama mtiririko mubashara unaotimiza masharti. Kwa nini sijajishindia zawadi yoyote?
Washirika wetu hubainisha watazamaji wanaotimiza masharti ambao watashinda kulingana na kanuni za kila mtiririko. Kanuni zinaweza kutofautiana kulingana na mshirika.
Ili uhakikishe kuwa unatimiza masharti, hakikisha kuwa umeunganisha akaunti na unatazama kwenye kompyuta yako, programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi au katika tovuti yetu ya vifaa vya mkononi. Iwapo unatazama katika vichezaji vilivyopachikwa, ukitumia programu ya YouTube ya televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti au kwa kutuma maudhui, hutatimiza masharti ya kupata zawadi.
To check if the video is eligible, you can look at the videos’ Player Settings, where eligible videos will include an option for you to review your linked account state.
Iwapo unatazama kwenye Android au iOS, hakikisha kuwa unatumia toleo jipya kabisa la YouTube.
Nitajuaje kuwa nimepata zawadi?
Baada ya kujishindia, zawadi zitasambazwa kwenye akaunti yako ya mshirika. Zawadi hizi zinaweza kuchukua hadi siku moja kabla hazijaonekana. Pata maelezo zaidi moja kwa moja kwenye tovuti ya mshirika.
Je, kipengele hiki kinapatikana kwenye vifaa vya mkononi?
Zawadi zinapatikana unapotazama kwenye kompyuta, programu ya vifaa vya mkononi, katika tovuti yetu ya vifaa vya mkononi m.youtube.com na kupitia hali ya kupachika picha ndani ya picha nyingine. Iwapo unatazama kwenye vichezaji vilivyopachikwa, hutatimiza masharti ya kupata zawadi.
Kwanza, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti. Huenda ukahitaji kuwasha madirisha ibukizi kwenye kivinjari chako ili uweze kuunganisha akaunti zako. Iwapo umeshindwa kuunganisha kwenye Safari, jaribu kivinjari kingine.
Kumbuka: Unaweza tu kuunganisha akaunti binafsi, wala si Akaunti za Biashara. Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti binafsi unapojaribu kuunganisha.
Iwapo video imebainishwa kuwa Inalenga Watoto, kipengele cha kuunganisha akaunti hakitapatikana.
Nilipokea ujumbe kwamba akaunti zangu zimeunganishwa, lakini hazionyeshi kuwa zimeunganishwa. Je, bado ninastahiki kupata zawadi?
Wakati mwingine kuna ucheleweshaji baina ya wakati akaunti zako zinaunganishwa na wakati zinaonyesha kuwa zimeunganishwa.
Tembelea ukurasa huu ili uthibitishe kuwa akaunti zako zimeunganishwa. Kwenye ukurasa huu, unaweza kuangalia huduma zote zilizounganishwa na akaunti yako. Unaweza pia kutenganisha huduma yoyote.
Ilimradi ukurusa huu unaonyesha kuwa akaunti zako zimeunganishwa, unastahiki kupata zawadi.
Iwapo akaunti zako hazionyeshi kuwa zimeunganishwa, unaweza pia kujaribu kuzitenganisha, kisha uziunganishe tena.
Ninajaribu kutenganisha akaunti zangu lakini bado zinaonyesha kuwa zimeunganishwa. Kwa nini?
Wakati mwingine kuna ucheleweshaji kati ya wakati ambao akaunti zako zinatenganishwa na wakati zinaonyesha kuwa zimetenganishwa.
Tembelea ukurasa huu ili uthibitishe kuwa akaunti zako zimetenganishwa. Ikiwa huduma haijaorodheshwa kwenye ukurasa huu, inamaanisha kuwa akaunti zako hazijaunganishwa.
Ninapounganisha akaunti yangu, maelezo ya aina gani huruhusiwa yafikiwe baina ya Google na akaunti yangu ya mshirika?
Baada ya kuunganisha akaunti yako na YouTube, YouTube inaweza kuruhusu maelezo ya utazamaji na hali yako ya usajili ifikiwe na mshirika anaweza kuruhusu taarifa za msingi za akaunti zifikiwe na Google au YouTube. Maelezo haya yatatusaidia kujua akaunti zinazostahiki kupata zawadi.