Kikumbusho cha pumzika kidogo

Kikumbusho cha pumzika kidogo kinakuruhusu kuweka kikumbusho cha kupumzika kidogo wakati unatazama video. Kikumbusho kitasitisha video yako hadi utakapokifunga au kuendelea kucheza video. Kipengele hiki kinapatikana kwenye matoleo ya 13.17 na mapya zaidi ya programu ya YouTube kwenye vifaa vya mkononi.

Kidokezo: Kwa watumiaji wenye umri wa miaka 13 hadi 17 kwenye YouTube, mipangilio chaguomsingi ya kikumbusho cha pumzika kidogo ni “Kimewashwa”. Kwa watumiaji wenye umri wa miaka 18 au zaidi, mipangilio chaguomsingi ni “Kimezimwa.” Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote.
Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Weka kikumbusho chako cha kupumzika kidogo:

  1. Gusa picha ya wasifu wako .
  2. Gusa Mipangilio .
  3. Gusa Jumla.
  4. Karibu na sehemu ya Nikumbushe kupumzika kidogo, gusa kipengele cha Washa  au Zima .
    • Ikiwa “Unawasha," chagua mara za kutumwa kwa KIkumbusho kisha uguse Sawa.
Kidokezo: Unaweza pia kuweka vikumbusho vya kupumzika kidogo kwa kugusa picha ya wasifu wako kisha Muda Uliotazama.

Ukipokea kikumbusho, unaweza kugusa Puuza ili kuendelea kutazama video. Unaweza kugusa Mipangilio ili kubadilisha mara za kutumwa kwa kikumbusho au kuwasha au kuzima kikumbusho. 

Kumbuka:

  • Ikiwa utafunga programu, kuondoka, kubadilisha vifaa au kusitisha video kwa zaidi ya dakika 30, kipima muda kitawekwa upya.
  • Unapotazama video za nje ya mtandao au kutuma kutoka kwenye simu yako, kipima muda hakitumiki.


 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7243899651568026844
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false