Kubadilisha mipangilio ya lugha au mahali

 

Unaweza kuchagua lugha na eneo unalopendelea kwenye YouTube ukitumia kompyuta yako, programu ya YouTube au kivinjari chako cha kifaa cha mkononi. 

Mipangilio ya lugha hubadilisha metadata ya video, kama vile jina la kituo na jina la video, inapopatikana na lugha inayotumika kwenye kipengele cha Kutafuta kwa Kutamka. Mahali unapochagua huathiri video zinazoonyeshwa katika sehemu ya: 

  • Mapendekezo
  • Zinazovuma
  • Habari

YouTube hutoa mapendeleo ya lugha na maudhui kwa nchi, maeneo na lugha zote zinazotumika kwenye YouTube. Tunaendelea kupanua uwezo wa huduma hii ili kuwafikia watumiaji zaidi. Ikiwa huwezi kupata lugha, nchi au eneo uliko, teua chaguo linalofaa zaidi kwa mahitaji na mambo unayopendelea.

Ikiwa YouTube haiwezi kupata nchi au eneo uliko, mahali chaguomsingi ni Marekani.

Kubadilisha lugha yako kwenye wavuti au programu ya YouTube

Fuata maagizo yaliyo hapa chini kuhusu tovuti ya kifaa cha mkononi au programu ya YouTube.

Programu ya YouTube

  1. Gusa picha yako ya wasifu .
  2. Gusa Mipangilio .
  3. Gusa Jumla.
  4. Gusa Mahali au Lugha ya programu.
  5. Gusa mahali au lugha ambayo ungependa kutumia.

Wavuti wa vifaa vya mkononi

Kwa chaguomsingi, tovuti ya kifaa cha mkononi ya YouTube hufuata mipangilio ya lugha inayotumika kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha lugha na mipangilio ya mahali kwenye tovuti ya kifaa cha mkononi.

  1. Nenda kwenye Akaunti yako .
  2. Gusa Mipangilio .
  3. Gusa Akaunti .
  4. Gusa Lugha ili uchague lugha tofauti.
  5. Gusa Mahali ili uchague mahali tofauti.

YouTube kwenye TV

  1. Bofya Mipangilio  kwenye programu ya YouTube kwenye TV.
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Lugha na Mahali".
  3. Chagua Lugha.
  4. Bofya Badilisha .
  5. Nenda kwenye lugha uliyochagua.
  6. Bofya Thibitisha Mabadiliko.

How to change the language and country settings on YouTube from your mobile device

Kubadilisha lugha ya arifa za barua pepe

Barua pepe zako kutoka YouTube hutumwa zikiwa katika lugha chaguomsingi ya nchi yako. Ikiwa umebadilisha mipangilio yako ya lugha ya YouTube, unaweza kubadilisha mipangilio yako ya barua pepe ili ilingane:

  1. Nenda kwenye mipangilio ya barua pepe.
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Lugha" ili ubadilishe lugha ya arifa zako za barua pepe.

Kubadilisha mipangilio ya mahali au lugha unayotumia kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, vifaa vya kutiririsha na vifaa vya michezo ya video


Kwa chaguomsingi, programu ya YouTube katika televisheni zinazoweza kuunganishwa kwenye intaneti, vifaa vya kutiririsha na vifaa vya michezo ya video vitafuata mipangilio ya lugha na ya mahali kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio hii ya YouTube wakati wowote. Ili ubadilishe mipangilio hii:

  • Fungua programu ya YouTube kwenye kifaa chako.
  • Chagua Mipangilio
  • Teua Lugha ili uchague lugha tofauti.
  • Teua Mahali ili uchague mahali tofauti.

Kubadilisha lugha ya utafutaji ya kibodi yako

Unaweza pia kubadilisha mipangilio ya lugha ya utafutaji katika kibodi ya utafutaji:

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, kifaa cha kutiririsha au kifaa chako cha michezo ya video.
  2. Teua Tafuta kisha Chagua lugha.

Kibodi ya utafutaji inaweza kutumia lugha zifuatazo:
 

  • Kiarabu
  • Kikorea
  • Kichina Kilichorahisishwa 
  • Kinorwe
  • Kichina cha Jadi (Hong Kong)
  • Kipolandi
  • Kichina cha Jadi (Taiwani)
  • Kireno
  • Kidenmaki
  • Kireno (Brazili)
  • Kiholanzi
  • Kirusi
  • Kiingereza
  • Kihispania
  • Kifaransa
  • Kihispania (Meksiko)
  • Kifaransa (Kanada)
  • Kihispania (US)
  • Kijerumani
  • Kiswidi
  • Kigiriki
  • Kithai
  • Kiyahudi
  • Kituruki
  • Kihungaria
  • Kiukraini
  • Kiitaliano
  • Kivietinamu
  • Kijapani

 

Kidokezo: Ikiwa lugha ya programu yako haitumiki, kibodi ya utafutaji itatumia Kiingereza kama lugha chaguomsingi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
193072829882358235
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false