Ili utazame video za YouTube, hakikisha unatumia toleo jipya zaidi la kivinjari, mfumo wa uendeshaji na muunganisho thabiti wa intaneti:
- Toleo jipya zaidi la Google Chrome, Firefox au Safari
- Muunganisho wa intaneti wenye kasi ya zaidi ya Kbps 500
Masharti ya filamu na vipindi vya televisheni
Baadhi ya video za kulipia kwenye YouTube -- kama vile filamu, vipindi vya televisheni na mitiririko mubashara -- huhitaji muunganisho wa kasi ya juu zaidi na uwezo mkubwa wa uchakataji kwa ajili ya kasi bora ya utiririshaji. Haya ni mambo unayohitaji:
- Toleo jipya zaidi la Google Chrome, Firefox au Safari
- Mfumo wa uendeshaji: Windows 7 au matoleo mapya zaidi, Mac OS X 10.7 au matoleo jipya zaidi na Ubuntu 10 au matoleo mapya zaidi
- Muunganisho wa intaneti wenye kasi ya zaidi ya Mbps 1
Huweza kusaidia kufunga vichupo, vivinjari na programu zingine wakati wa kutiririsha video yako. Kuunganisha kwa kutumia waya kunaweza pia kusaidia kuboresha muunganisho wako wa Intaneti, badala ya kutumia muunganisho wa mtandao pasiwaya.
Jedwali lililo hapa chini linaonyesha makadirio ya kasi zinazopendekezwa ili kucheza kila muundo wa video.
Ubora wa Video |
Kasi inayopendekezwa wakati wote |
---|---|
UHD ya 4K | Mbps 20 |
HD 1080p | Mbps 5 |
HD 720p | Mbps 2.5 |
SD 480p | Mbps 1.1 |
SD 360p | Mbps 0.7 |
- Huwezi kucheza katika ubora wa HD unapotiririsha kwenye kivinjari, isipokuwa katika kivinjari cha Safari kinachotumika kutiririsha ubora wa HD pekee. Unaweza pia kutiririsha katika ubora wa HD ukitumia mojawapo ya vifaa vinavyoruhusiwa vilivyoorodheshwa hapa.
- Wakati mwingine, unaweza kununua au kukodisha toleo la HD/UHD la video kwenye kifaa au kivinjari ambacho hakiruhusu uchezaji wa HD/UHD. Bado unaweza kutazama maudhui katika ubora wa chini kwenye kifaa hicho au utazame katika ubora wa HD au UHD ukitumia kifaa oanifu tofauti.
Vifaa vinavyotumiwa na Chaneli za Primetime (Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia na Uingereza pekee)
Ikiwa uko nchini Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia au Uingereza, unaweza kutazama Chaneli za YouTube Primetime kwenye vifaa vifuatavyo:
Vifaa vya michezo ya video |
|
---|---|
|
|
Skrini mahiri |
|
Simu mahiri na vishikwambi | Simu na vishikwambi vinavyotumia toleo la Android 6.0 Marshmallow au matoleo mapya zaidi |
iPhone na iPad zinazotumia toleo la iOS 12 au matoleo mapya zaidi | |
Televisheni Zinazoweza Kuunganisha Kwenye Intaneti | Televisheni za Hisense Zinazoweza Kuunganisha Kwenye Intaneti(miundo mahususi) |
Televisheni za LG zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti (miundo ya mwaka 2016 na miundo mipya zaidi pekee) | |
Televisheni za Roku (miundo yote) | |
Televisheni za Samsung zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti (miundo ya mwaka 2017 na miundo mipya zaidi pekee) | |
Televisheni za Sharp zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti (miundo mahususi pekee) | |
Televisheni za Sony zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti (miundo mahususi pekee) | |
Televisheni za Vizio SmartCast (miundo mahususi pekee) | |
Televisheni mahususi zilizo na kiolesura cha Android TV na NVIDIA Shield | |
Televisheni Mahususi Zinazoweza Kuunganisha kwenye Intaneti za Toleo la Fire TV | |
Vifaa vya kutiririsha | Apple TV (toleo la 4 na 4K) |
Chromecast yenye Google TV | |
|
|
Vifaa vya televisheni mahususi vya kebo (kama vile Xfinity X1) |
Unaweza kutazama lakini si kununua Chaneli za YouTube Primetime kwenye kifaa chochote kati ya vifuatavyo:
- Apple TV
- Xbox
- Televisheni Mahususi za Panasonic