Muhtasari wa Uthibitishaji Unaojifanyia wa YouTube

Ukiwa na uwezo wa kufikia Uthibitishaji Unaojifanyika, tunakuuliza ukadirie video zako dhidi ya mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Mpango wa Uthibitishaji Unaojifanyia kwenye YouTube

Uthibitishaji Unaojifanyia una umuhimu gani?

Maoni yako yanaweza kutusaidia kufanya uamuzi wa uchumaji wa mapato haraka na kwa usahihi zaidi. Kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia:

  1. Unaweza kutufahamisha kilicho katika video yako.
  2. Kisha mifumo yetu ya kiotomatiki itakagua na kuamua.
  3. Iwapo hukubailiani na mifumo yetu ya kiotomatiki, unaweza kuomba ukaguzi unaofanywa na binadamu.
  4. Mkaguzi atakagua video yako na kutoa maoni. Unaweza kuona mahali ambapo wewe na mkaguzi hamkubaliani (kwa mfano, lugha isiyofaa” au “masuala nyeti”) kwenye maudhui ndani ya video hiyo.

Ukitathmini video zako kwa njia sahihi, tutategemea maoni yako badala ya mifumo yetu ya kiotomatiki. Maoni yako pia yatatumiwa kuboresha mifumo yetu kwa jumuiya yote ya watayarishi wanaochuma mapato.

Uthibitishaji Unaojifanyia unapatikana kwa maudhui yaliyowekewa alama kuwa “yanalenga watoto”. Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu bora za watoto na maudhui ya familia, na mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji yaliyobuniwa hasa kwa maudhui ya watoto.

Hatua unazohitaji kuchukua

Kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia, utahitaji kukadiria:

  • Video zote mpya ambako umewasha matangazo.
  • Video ulizopakia awali ambako sasa ungependa kuwasha matangazo.

Si lazima kukadiria video zilizopo ambako umewasha matangazo.

Jinsi ya kukadiria video zako

Fuata hatua hizi ili ukadirie video zako dhidi ya mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji:

  1. Fuata hatua ili upakie video katika Studio ya YouTube. Wakati video yako inapakiwa, chagua menyu kunjuzi ya Uchumaji wa mapato kisha chagua Washa kisha bofya Nimemaliza kisha bofya Endelea.
  2. Chagua vipengele vyovyote vinavyofaa kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina kisha bofya Endelea.
  3. Jaza dodoso kwenye ukurasa wa Ufaafu kwa matangazo kisha bofya Tuma Ukadiriaji kisha bofya Endelea.
    • Iwapo video yako haijumuishi maudhui yaliyoorodheshwa katika dodoso, unaweza kuenda chini na kuteua kisanduku karibu na “Hamna kati ya yaliyo hapa juu”.
  4. Ukurasa wa Ukaguzi hutumia mifumo yetu kukagua video yako ili kubaini ufaafu kwa matangazo baada ya wewe kuikadiria. Baada ya hili kufanyika kisha bofya Endelea.
  5. Chagua hali ya uonekanaji wa video yako.
  6. Bofya Nimemaliza.

Je, unakadiria mwenyewe maudhui yanayolenga watoto? Iwapo ni hivyo, hakikisha unafahamu desturi bora za maudhui ya watoto na familia. Ili upate hatua za kuweka alama kuwa video zinalenga watoto (ili uweze kuzikadiria katika Studio), tembelea ukurasa huu.

Kuelewa hali ya ukadiriaji wako

Ukiwa kwenye mpango, utapata ukurasa wa usahihi wa ukadiriaji.

  • Angalia usahihi wa ukadiriaji wako.
  • Angalia sehemu ambayo wewe na YouTube hamkubailiani kuhusu ukadiriaji.
  • Omba maoni kutoka kwa wakadiriaji wetu au uone maoni ambayo wakadiriaji wetu walitoa.

Unaweza kuona jinsi historia yako ya ukadiriaji inalingana na ukadiriaji wa mifumo yetu na wakaguzi wanadamu. Kwa kawaida tunaweza kubaini usahihi wako baada ya kukadiria video 20 zako. Maelezo haya ni muhimu kwa sababu kadri ukadiriaji wako ulivyo sahihi, ndivyo tunaweza kuutumia kuamua matangazo ya kuonyesha.

Jinsi ya kusoma ukadiriaji wako wa usahihi
Unavyokadiria video zaidi, unaweza kupata jinsi ukadiriaji wako unalingana na wa mifumo yetu ya kiotomatiki na wakaguzi wanadamu.

Tafuta ukurasa wa hali ya ukadiriaji wako

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube kupitia kituo chako ambacho ni sehemu ya Uthibitishaji Unaojifanyia.
  2. Nenda kwenye https://studio.youtube.com/channel/UC/videos/contentratings.
  3. Utaona ukurasa wa ukadiriaji wa hali.

Maana ya kila safu wima katika ukurasa wa hali ya ukadiriaji wako

  • Video: Video inayokadiriwa.
  • Tarehe ulipokadiria: Tarehe ulipokadiria video yako.
  • Ukadiriaji wako: Utabiri wa mifumo yetu kuhusu hali ya uchumaji wa mapato wa video yako utalingana na jinsi ulivyokadiria video yako.
  • Ukadiriaji wa YouTube: Kile ambacho mifumo ya YouTube au wakaguzi wanadamu wanaamini hali ya uchumaji wa mapato wa video hii inapaswa kuwa.
  • Aina ya Ukaguzi wa YouTube: Utaona aikoni 2 tofauti. Moja inaonyesha kuwa mifumo yetu ya kiotomatiki ilikagua video yako, na nyingine inaonyesha kuwa mtaalamu wa sera aliikagua.
    • KOMPYUTA: Aikoni hii inamaanisha mifumo yetu ya kiotomatiki ilifanya uamuzi kuhusu uchumaji wa mapato.
    • BINADAMU: Aikoni hii inamaanisha mtaalamu wa sera -- mtu halisi -- alikagua video.
  • Kitendo: Safu wima hii inakufahamisha hatua unayoweza kuchukua kuhusu uamuzi wa kuchuma mapato.
    • Omba ukaguzi: Mifumo yetu ya kiotomatiki ilikagua video yako. Wakati mwingine mifumo yetu hukosea. Unaweza kubofya Omba ukaguzi ili upate mojawapo ya wataalamu wetu wa sera kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu uchumaji wa mapato.
    • Angalia maoni: Mtaalamu wa sera amekagua video yako na kufanya uamuzi wa mwisho. Baada ya mkaguzi mwanadamu kufanya uamuzi, hali ya uchumaji wa mapato haiwezi kubadilishwa. Ukibofya Angalia maoni, utaona tofauti kati ya jinsi ulivyokadiria video na jinsi wataalamu wetu wa sera walikadiria video. Pata maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa ukaguzi wa uchumaji wa mapato unaofaa watangazaji.
Jinsi ukadiriaji wako huathiri kituo chako
Utapewa hali ya ukadiriaji kulingana na mara ambazo uamuzi wetu wa uchumaji wa mapato unalingana na jinsi ulivyokadiria hali ya uchumaji wa mapato wa video yako.
Iwapo usahihi wako ni wa juu: Hiyo inamaanisha kuwa tutatumia ukaguzi wako kusaidia kuamua matangazo ambayo yanaweza kuonyeshwa kwa video zako.
Iwapo usahihi wa ukadiriaji wako ni wa chini, au iwapo hujakadiria video nyingi: Huenda ukahitaji kukagua maoni ya mtaalamu wetu wa sera ili kufahamu vyema jinsi mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji hufanya kazi, au ukadirie video zaidi. Baada ya usahihi wa ukadiriaji wako kuwa bora, tutatumia ukaguzi wako mara nyingi ili kusaidia kuamua matangazo yanayoweza kuonyeshwa kwa video zako.
Usahihi wa ukadiriaji wako unaweza kubadilika kadri muda unavyosonga.

Maswali Yanayoulizwa Sana Kuhusu Mpango

Ninawezaje kufikia Uthibitishaji Unaojifanyia?

Wakati una uwezo wa kufikia Uthibitishaji Unaojifanyia, utaona ujumbe katika Studio ya YouTube unaokufahamisha kuwa sasa unaweza kukadiria video zako. Kwa kawaida hili hufanyika mwezi mmoja au miwili baada ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. 

Nitakapoanza kukadiria video zangu, je hali hii inamaanisha kuwa nitachuma mapato?

Iwapo video yako haitimizi mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji na ujaribu kuwasha matangazo, bado wataalamu wa sera watakomesha uchumaji wa mapato kwenye video yako. Upande mwingine, iwapo utaendelea kkufanya uamuzi sahihi wa uchumaji wa mapato kwa video yako, huenda ukaona aikoni chache za manjano kadri muda unavyosonga. Mabadiliko haya ni kwa sababu tunatumia ukadiriaji wako badala ya ukadiriaji wa mifumo yetu ya kiotomatiki ili kubaini matangazo yatakayoonyeshwa kwenye video zako.

Je, kuna njia ya kuona uchumaji wa mapato wa video yangu kabla niiweke hadharani?
Iwapo ungependa kukagua hali ya uchumaji wa mapato kabla ya kufanya video ya umma, unaweza kusubiri ukaguzi wa kubaini ufaafu kwa matangazo kukamilika wakati wa mchakato wa upakiaji.
Ninawezaje kuboresha usahihi wa ukadiriaji wangu?
Kuna njia 3 unaweza kujifuza jinsi ya kukadiria video yako kwa njia sahihi:

Tumia ukurasa wa ukaguzi wakati wa kupakia

Unaweza kutumia ukurasa wa ukaguzi wakati wa kupakia ili ukague video yako ili kubaini ufaafu kwa matangazo na madai ya hakimiliki kabla ya kuichapisha.
Kagua mwongozo wetu
Unaweza kuangalia mwongozo wetu wa kujikadiria dhidi ya mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji. Nyenzo hii itakusaidia kufahamu kinachofaa na kisichofaa kwa watangazaji wote. Iwapo unakadiria mwenyewe maudhui yanayolenga watoto, hakikisha unafahamu desturi zetu bora za maudhui ya watoto na familia.
Pata maoni kutoka kwa wakaguzi wa YouTube
Iwapo bado huna uhakika kuhusu ukadiriaji wa video yako, unaweza:
  1. Kukadiria video yako.
  2. Omba tukague wenyewe.
    • Unapokadiria video yako kama ambayo haifai matangazo na uombe ukaguzi wa binadamu, tutaharakisha muda wa kukagua.
  3. Wakadiriaji wetu watakagua video yako na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu uchumaji wa mapato.
  4. Kagua maoni kutoka kwa mkadiriaji.
Nini kitafanyika iwapo nitakosea na nikadirie video zangu kwa njia isiyo sahihi?

Kwa kuwa tunataka kutumia ukadiriaji wako kufanya uamuzi sahihi wa uchumaji wa mapato, ni muhimu ukadirie maudhui yako uwezavyo.

Iwapo tutaona makosa mengi yanayorudiwa kulingana na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watagazaji, kituo chako kitakaguliwa ili kijumuishwe katika Mpango wa Washirika wa YouTube.

Kwa nini mwongozo wa maudhui ni tofauti kwenye YouTube ikilinganishwa na kwenye Televisheni?
Watangazaji wana matarajio tofauti ya YouTube ikilinganishwa na Televisheni. Kwenye TV, kwa kawaida watangazaji wana fursa ya kukagua maudhui kabla yaonyeshwe ili kubaini iwapo yako sawa. Kwenye YouTube, watangazaji hawawezi kukagua kila video inayoonyesha matangazo yao. Mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji unaangazia kile ambacho watangazaji wangependa kuhusisha chapa zao kwake. Ingawa watangazaji wanaweza kubadilisha mapendeleo yao binafsi, mwongozo wetu unawakilisha kinachofaa watangazaji wote kote duniani.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6217431323859719853
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false