Tuzo za Watayarishi wa YouTube ni njia yetu ya kutambua jitihada za ziada wanazoweka watayarishi katika kukuza chaneli zao na kujenga jumuiya zilizochangamka, kwa njia inayofaa. Ili kushiriki katika Tuzo za Watayarishi, watayarishi wanahitaji kutimiza masharti ya kujiunga na ni lazima wafuate sera zetu.
Tuzo za Watayarishi wa YouTube
Watayarishi wengi kuliko hapo awali wanafikia mafanikio makubwa kwenye YouTube na kunufaika na ari yao kupitia Tuzo za Watayarishi.
Kuanzia Agosti 2024, tunawaletea tuzo mpya nyepesi. Usiwe na hofu, ubora na muundo pamoja na hadhi na utambuzi unaostahili hautabadilika.
Fahamu iwapo chaneli yako imetimiza masharti ya kupata Tuzo ya Watayarishi wa YouTube na upate msimbo wa kudai tuzo yako ikiwa imetimiza masharti hayo:
Pata Tuzo ya Mtayarishi wa YouTube
Masharti ya kupata tuzo
Ili utumize masharti ya kushiriki katika Tuzo za Watayarishi, unahitaji kukidhi mwongozo ufuatao:
- Utimize kigezo mahususi cha wanaofuatilia:
- Fedha: Unapopata watu 100,000 wanaofuatilia chaneli yako
- Dhahabu: Unapopata watu 1,000,000 wanaofuatilia chaneli yako
- Almasi: Unapopata watu 10,000,000 wanaofuatilia chaneli yako
- Almasi Nyekundu: Unapopata watu 100,000,000 wanaofuatilia chaneli yako
- Chaneli yako inatumika (imepakia video ndani ya miezi 6 iliyopita).
- Usiwe na tukio linaloendelea la ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya na usiwe na ukiukaji katika siku 365 zilizopita.
- Unatii Sheria na Masharti ya YouTube.
- Hujakataliwa au kusimamishwa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.
- Chaneli yako haijafungwa au kuhusishwa na akaunti ambayo imefungwa.
- Huna maudhui yanayopotosha, ya taka au ya ulaghai.
- Maudhui yako makuu ni halisi. Chaneli ambazo zinalenga mikusanyiko, miseto, uratibu au matumizi makubwa ya wahusika au maudhui yaliyo na hakimiliki ya mtu mwingine huenda zisitimize masharti ya kushiriki.
Si lazima uwe mwanachama wa Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ili utimize masharti ya kupata tuzo. Tuzo za Watayarishi hutolewa kwa hiari ya YouTube. Kila chaneli hukaguliwa kwa umakini ili kuhakikisha kuwa imetimiza masharti.
Tuzo za Watayarishi ni za matumizi ya binafsi pekee na hazipaswi kuuzwa au kusambazwa kwa mtu yeyote ambaye si mhusika wa timu inayosimamia chaneli yako. Ukikiuka sera hii, huenda ukaadhibiwa.
Adhabu inaweza kuwa ni pamoja na:
- Kukosa kupata tuzo
- Kutotimiza masharti ya kupata tuzo zijazo
- Huenda akaunti yako ya YouTube au Google ikasimamishwa
Upatikanaji katika nchi au maeneo
Mpango wa Tuzo za Watayarishi wa YouTube haupatikani kwenye chaneli zilizopo katika nchi au maeneo yafuatayo:
|
|
|
Kudai Tuzo ya Watayarishi wa YouTube
Baada ya kutimiza vigezo vyetu vya kupata tuzo, tutakutumia msimbo wa kuidai. Fuata hatua hizi ili udai tuzo yako:
- Tafuta na unakili namba ya kupata tuzo tuliokutumia.
- Ikiwa umepoteza namba ya kupata tuzo, tembelea ukurasa wetu wa ukaguzi shirikishi wa kutimiza masharti ili upate namba yako ya kupata tuzo.
- Nenda kwenye tovuti ya kudai Tuzo za Watayarishi kisha uweke namba yako ya kupata tuzo.
- Weka maelezo yako ya usafirishaji na ubainishe jinsi ambavyo ungependa jina la chaneli yako lionekane kwenye tuzo yako.
- Chagua “Agiza Sasa” ili umalize kudai tuzo yako.
Ikiwa unaishi nchini Brazili au India, utaombwa maelezo ya ziada kama vile namba ya ushuru wakati unadai Tuzo yako ya Watayarishi. Ofisi husika za forodha zinahitaji maelezo haya.
Usafirishaji na uwasilishaji
Baada ya kutuma maelezo yako ya usafirishaji na kudai tuzo yako, tutaileta kwako baada ya takribani wiki 2-3. Oda zilizowekwa baada ya tarehe 1 Juni, 2023 zinaweza kufuatiliwa hapa. Ili kuhakikisha tuzo yako inakufikia kwa wakati unaofaa, kumbuka yafuatayo:
- Usisahau kutumia jina lako rasmi kamili unapowasilisha maelezo ya usafirishaji. Hii husaidia pale ambapo utahitajika kuichukua kutoka kwenye ghala la forodha au ofisi ya uwasilishaji.
- Utapokea barua pepe iliyotumwa kiotomatiki na kampuni ya usafirishaji yenye namba ya kufuatilia mara baada ya kusafirisha tuzo yako. Jisajili ili upokee arifa za ufuatiliaji ili uhakikishe tuzo yako inakufikia.
- Utawajibika iwapo kampuni ya usafirishaji itawasiliana nawe na kukuomba hati au maelezo zaidi. Hatua hii inaweza kusaidia tuzo yako ipitishwe kwenye ofisi za forodha au iletwe kwako.
- Utawajibika kulipia ushuru wowote na/au kodi zinazohitajika katika nchi au maeneo fulani. Kisheria, YouTube haipaswi kulipia gharama hizi. Nchi hizi ni pamoja na, lakini si tu: Armenia, Azabaijani, Kambodia, Kyrgyzstani, na Uzbekistani.
- Usipowasiliana na kampuni ya usafirishaji, Tuzo yako ya Watayarishi inaweza kurudishwa au kupotea. Katika hali hizi, huenda ukalazimika kununua tuzo mbadala ikiwa ungependa kupata Tuzo yako ya Watayarishi.
-
Baada ya kupokea, una hadi siku saba kuripoti uharibifu wowote kwenye Society Awards kwa kuwasilisha fomu hii. Utatakiwa kutuma picha za tuzo husika na kasha, kwa hivyo tafadhali hifadhi vifaa vyote vya kufungashia. Pia, hali hii itakuruhusu kurejesha tuzo kwa muuzaji ili upate tuzo mbadala. Tafadhali kumbuka kuwa utapata tu tuzo mbadala bila malipo baada ya tuzo halisi kurejeshwa na kutathminiwa.