Mikato ya kibodi kwenye YouTube

Okoa muda unapovinjari katika YouTube, ukitumia mikato ya kibodi.

Ili ufikie orodha ya mikato ya kibodi, nenda kwenye picha ya wasifu wako Profile, kisha uchague Mikato ya Kibodi Keyboard. Unaweza pia kuweka SHIFT+? kwenye kibodi yako. Unapoweka kipanya juu ya vitufe vya kichezaji, utaona mikato ya kibodi inayofaa. Kwa mfano, unapowekelea kipanya juu ya aikoni ya skrini nzima, utaona 'Skrini nzima (f),' inayoashiria kuwa unaweza kuweka f ili ufungue skrini nzima.

Mikato ya kibodi | Vidokezo vya (matumizi ya) Kina kutoka Kituo cha Usaidizi cha YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Mikato ya kibodi

Ikiwa unatumia hali mpya ya utumiaji wa kompyuta, ni lazima ubofye kicheza video kabla ya kutumia mikato ya video. Ili urejeshe hali ya awali ya utumiaji wa kompyuta, nenda kwenye picha ya wasifu  kisha ubofye Rejesha mipangilio ya awali ya YouTube.
Mikato ya kibodi Utendaji
Spacebar Kucheza au Kusimamisha wakati upau wa kusogeza umechaguliwa. Washa kitufe ikiwa kimeangaziwa.
Kucheza au Kusimamisha Kitufe cha Maudhui kwenye kibodi Kucheza au Kusimamisha.
k Kusimamisha au Kucheza kwenye kichezaji.
m Kuzima au kurejesha sauti ya video.
Kusitisha Kitufe cha Maudhui kwenye kibodi Kusitisha.
Kitufe cha Maudhui ya Wimbo Unaofuata kwenye kibodi Kuhamia kwenye wimbo unaofuata katika orodha ya kucheza.
Kishale cha Kushoto au Kulia kwenye upau wa kusogeza Kusogeza nyuma au mbele sekunde 5.
j Kusogeza nyuma sekunde 10 kwenye kichezaji.
l Kusogeza mbele sekunde 10 kwenye kichezaji.
. Wakati video imesimamishwa, kuruka kwenye fremu inayofuata.
, Wakati video imesimamishwa, kurudi nyuma kwenye fremu iliyotangulia.
> Kuongeza kasi ya kiwango cha kucheza video.
< Kupunguza kasi ya kiwango cha kucheza video.
Kitufe cha Mwanzo au Mwisho kwenye upau wa kusogeza Kusogeza hadi sekunde za mwanzo au mwisho wa video.
Kishale cha Juu au Chini kwenye upau wa kusogeza Kuongeza au Kupunguza sauti kwa asilimia 5.
Nambari 1 hadi 9 Kusogeza hadi asilimia 10 mpaka 90 ya video.
Nambari 0 Kusogeza hadi mwanzo wa video.
/ Kwenda kwenye kisanduku cha kutafutia.
f Kuwasha skrini nzima. Ikiwa hali ya skrini nzima imewashwa, bofya tena F au bonyeza funga ili uondoe hali ya skrini nzima.
c Kuwasha kipengele cha manukuu ikiwa yanapatikana. Ili ufiche manukuu, washa tena C.
Shift+N Kuhamia kwenye video inayofuata (Ikiwa unatumia orodha ya kucheza, itaenda kwenye video inayofuata kwenye orodha ya kucheza. Ikiwa hutumii orodha ya kucheza, itahamia kwenye video zinazofuata zilizopendekezwa za YouTube).
Shift+P Kuhamia kwenye video iliyotangulia. Kumbuka kuwa njia hii ya mkato inafanya kazi tu wakati unatumia orodha ya kucheza.
i Kufungua Kichezaji kidogo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
3243026086407007726