Ni kwa nini video yangu ina asilimia ya juu ya mibofyo na wastani wa kipindi cha kutazama lakini maonyesho machache?
Je, niepuke kufanya nini na data yangu ya asilimia ya mibofyo?
- Kuamua bila data ya kutosha. Ni muhimu kupitia data yako ya asilimia ya mibofyo bada ya kupata idadi kubwa zaidi ya maonyesho. Epuka kuangalia asilimia yako ya mibofyo mara baada tu ya kupakia.
- Kuboresha kwa mabadiliko madogo katika asilimia ya mibofyo. Ni kawaida kuwa na mabadiliko madogo katika asilimia ya mibofyo, na hufai kuchukua hatua yoyote kwa wakati huo. Maboresho yanaweza kukusaidia iwapo mabadiliko katika asilimia ya mibofyo ni makubwa sana.
- Kujaribu majina au vijipicha kadhaa kwenye video moja. Ni vigumu kuhakikisha kila video inatazamwa na hadhira moja. Tofauti katika asilimia ya mibofyo huenda ikatokana na vyanzo vya watazamaji, badala ya jina au kijipicha.
Nitajuaje iwapo asilimia ya mibofyo ya maonyesho yangu ni kubwa au ndogo?
Asilimia ya mibofyo ya maonyesho hupima mara ambazo watazamaji hutazama video baada ya kuona onyesho lililorekodiwa kwenye YouTube. Huenda ikawakilisha seti ndogo ya utazamaji wa jumla wa kituo, kwa kuwa si maonyesho yote yanahesabiwa katika kipimo hiki, kama vile ya skrini za mwisho au yaliyo kwenye tovuti za nje.
Asilimia ya mibofyo ya maonyesho yatatofautiana kutokana na aina ya maudhui, hadhira na mahali kwenye YouTube ambapo onyesho lilionekana. Kumbuka kuwa vijipicha vya video zako kila wakati hushindana na video zingine, iwe kwenye ukurasa wa kwanza, “Inayofuata” kwenye ukurasa wa kutazama, katika matokeo ya utafutaji na hata katika mipasho ya wanaofuatilia.
Nusu ya vituo na video kwenye YouTube vina asilimia ya mibofyo (CTR) ya maonyesho inayoangukiwa kati ya asilimia 2 na asilimia 10.
Video au vituo vipya (kama vile ambavyo vina chini ya wiki moja tangu vifunguliwe), au video zenye chini ya utazamaji 100 zinaweza kuona asilimia pana hata zaidi. Video ikipata maonyesho mengi (kama vile ikionekana kwenye Ukurasa wa Kwanza), ni kawaida kwa asilimia ya mibofyo (CTR) kuwa ndogo. Video ambazo maonyesho mengi yanatoka kwenye vyanzo kama vile ukurasa wa chaneli yako zinaweza kuwa na kiwango cha juu.
Hatimaye, ni bora kulinganisha asilimia za mibofyo (CTR) kati ya video katika kipindi kirefu na kukumbuka jinsi vyanzo vya watazamaji vitakavyoathiri asilimia ya mibofyo (CTR) yake.
Ni kwa nini nina utazamaji mwingi kuliko maonyesho?
Ni kwa nini kipimo cha asilimia ya mibofyo hakilingani na hesabu zangu?
Je, maonyesho yanahusianaje na uchumaji wa mapato?
Kumbuka: Mapendekezo haya yanatokana na viwango jumlishi vya mafanikio kwenye YouTube. Hayakuhakikishii matokeo yoyote mahususi katika hali yako mahususi.