Maelezo ya mawasiliano katika ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Taarifa fulani binafsi inahitajika unapowasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kupitia fomu yetu ya wavuti.

Jinsi taarifa yako inavyotumiwa

  • Video ikiondolewa kwa ajili ya ukiukaji wa hakimiliki, jina la mwenye hakimiliki litaonekana kwenye YouTube badala ya video hiyo.
  • Jina lako rasmi kamili linahitajika kukamilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Linaweza kushirikiwa na aliyepakia video iliyoondolewa kwa kukiuka hakimiliki.
  • Anwani msingi yako ya barua pepe uliyotumia katika ombi lako la kuondoa video linaweza kushirikiwa na aliyepakia video iliyoondolewa kwa ukiukaji wa hakimiliki. Aliyepakia video anaweza kuwasiliana nawe ili kushughulikia onyo lake la hakimiliki.
  • Anwani yako ya mahali halisi na namba yako ya simu zitawekwa kwa faragha isipokuwa zihitajike kama sehemu ya mashtaka. YouTube ikitakiwa kushiriki maelezo yoyote, tutakuarifu kabla ya kufanya hivyo.
  • Maelezo ya kazi inayodaiwa kukiukwa yataruhusiwa kufikiwa na aliyepakia video iliyoondolewa kwa ukiukaji wa hakimiliki ili aelewe sababu ya kuondolewa kwa video yake. 

Maombi ya kuondoa video yanayopatikana kwa umma

Aliyepakia video inayokiuka hakimiliki anaweza kuomba nakala ya ombi la kuondoa video. Maelezo yanayoonyeshwa kwa umma yanajumuisha:

  • Jina la mwenye hakimiliki
  • Anwani msingi ya barua pepe
  • Anwani ya barua pepe ya pili (sehemu isiyo ya lazima kwenye fomu yetu ya wavuti)
  • Jina lako rasmi kamili
  • Maelezo yako ya kazi inayodaiwa kukiuka hakimiliki
  • Majibu yako kwa maombi ya YouTube ya maelezo zaidi. YouTube itaomba maelezo zaidi iwapo ombi lako la kuondoa video halijakamilika au linaonekana si sahihi.

Malalamiko kuhusu kushiriki maelezo ya mawasiliano

Ikiwa una malalamiko kuwa kuna mtu anakunyanyasa kwenye YouTube, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kuripoti unyanyasaji na uchokozi wa mtandaoni badala ya ukiukaji wa hakimiliki.

Ingawa malalamiko kuhusu unyanyasaji na ukiukaji wa hakimiliki wakati mwingine yanalingana, kwa kesi kama hizi, mchakato wa ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki huenda usiwe chaguo bora. Pia, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kama vile matumizi ya haki kabla ya kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Kumbuka kwamba mwakilishi aliyeidhinishwa (kama vile wakili) anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa niaba ya mwenye hakimiliki. Mwakilishi aliyeidhinishwa lazima atumie akaunti yake ya YouTube kuwasilisha ombi. Pia, anatakiwa abainishe uhusiano wake na mwenye hakimiliki katika ombi la kuondoa video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16039704613828023095
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false