Unaweza kutumia data ya watazamaji wa kipekee kupata taswira bora zaidi ya ukubwa wa hadhira yako, au idadi iliyokadiriwa ya watazamaji waliotazama video zako katika kipindi fulani. Iwe anatazama kwenye kompyuta au simu au anatazama zaidi ya mara moja, anahesabiwa kama mtazamaji mmoja wa kipekee.
Data inapima jumla ya idadi ya watu wanaotazama video au chaneli kwa kutoa maelezo ya matukio ambapo huenda mtazamaji alitazama maudhui kwenye vifaa tofauti au ambapo watazamaji wengi walitazama kwa pamoja kwenye kifaa kimoja. Mfumo unajumuisha data kutoka kwenye vifaa na hujumuisha watazamaji walioingia katika akaunti na ambao waliondoka kwenye akaunti ili kukadiria idadi ya watazamaji.
Kwa ubora wa data, jumla ya idadi ya watazamaji wa kipekee inapatikana kwa vipindi vya hadi siku 90. Unaweza kulinganisha vipindi tofauti vya siku 90 ili uone mabadiliko katika muda fulani. Data ya watazamaji wa kipekee inapatikana kuanzia tarehe 1 Agosti, 2017.
Kwa Video Fupi, vipimo vya kutazama kabisa hutumika kukadiria watazamaji wa kipekee na kuonyesha watu walioendelea kutazama maudhui.
Kupata data ya watazamaji wako wa kipekee
Unaweza kuona watazamaji wako wa kipekee katika sehemu ya hali ya Kina kwenye kompyuta yako.
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu
.
- Katika kona ya juu kulia, bofya hali ya Kina ili uone watazamaji wako wa kipekee na vipimo vingine.
Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia hali ya kina kwenye Takwimu za YouTube.
Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu watazamaji wa kipekee
Ninawezaje kutumia data hii?- Unaweza kuangalia wastani wa watazamaji wa kipekee waliotazama chaneli yako kwa kuangalia kipimo cha “Wastani wa utazamaji kwa kila mtazamaji” katika kichupo cha ANGALIA ZAIDI.
- Linganisha ukubwa wa hadhira yako na idadi ya wanaofuatilia chaneli yako ubaini video zilizokusaidia kufikia hadhira pana zaidi ya wanaofuatilia chaneli yako.
- Baini matukio ambapo video yako ilivutia hadhira mpya kwa kulinganisha watazamaji wa kipekee wa chaneli yako kabla na baada ya kuchapisha video.
- Unaweza kutumia maelezo haya kuongoza mkakati wako wa maudhui.