Kuhusu programu ya Wapigaripoti Wanaopewa Kipaumbele kwenye YouTube

Mpango wa Wapigaripoti Wanaopewa Kipaumbele kwenye YouTube unasaidia kutoa zana imara kwa mashirika ya serikali na mashirika yasiyo ya serikali (NGO). NGO na mashirika haya yana ufanisi hususan katika kutambua maudhui ya YouTube yanayokiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Mpango wa Wapigaripoti Wanaopewa Kipaumbele kwenye YouTube unajumuisha:

  • Fomu ya wavuti ambayo NGO na mashirika ya serikali yanaweza kutumia kuwasiliana na YouTube moja kwa moja
  • Uwezo wa kuona maamuzi kuhusu maudhui yaliyoripotiwa
  • Kupa kipaumbele ukaguzi wa maudhui yaliyoripotiwa ili hatua ichukuliwe haraka
  • Majadiliano yanayoendelea na maoni kuhusu nyanja za maudhui ya YouTube
  • Mafunzo ya mara moja moja mtandaoni

Masharti ya kujiunga kwenye mpango

NGO na mashirika ya serikali yametimiza masharti ya kushiriki katika mpango wa Wapigaripoti Wanaopewa Kipaumbele kwenye YouTube. Wanaostahili:

  • Walio na ujuzi uliotambuliwa katika angalau kipengee kimoja cha sera
  • Wanaoripoti maudhui mara kwa mara kwa usahihi wa hali ya juu
  • Walio tayari kushiriki katika majadiliano yanayoendelea na maoni kuhusu nyanja za maudhui ya YouTube

Baadhi ya mashirika, ikiwa ni pamoja na mashirika kutoka nchi au maeneo ambayo kuna historia ya matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu au ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, yanaweza kufanyiwa ukaguzi zaidi.

Jinsi ya kujiunga kwenye mpango wa Wapigaripoti Wanaopewa Kipaumbele kwenye YouTube

Ikiwa unawakilisha NGO au Shirika la serikali, tafuta mtu wa kuwasiliana naye kwenye YouTube au Google katika eneo ulipo.

Kidokezo: Kabla ya kuwa Mpigaripoti Mwenye Kipaumbele, washiriki kutoka serikali na NGO wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya YouTube kuhusu Mwongozo wa Jumuiya na michakato yetu ya utekelezaji.

Mahitaji ya programu

Mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele upo ili kusaidia kutekeleza Mwongozo wetu wa Jumuiya. Ni lazima washiriki:

  • Wajitolee kuripoti maudhui yanayokiuka mwongozo wetu kila mara. YouTube inahifadhi haki ya kuondoa mshiriki yeyote ambaye hashiriki katika mpango huu kwa njia ya maana.
  • Wawe tayari kushiriki katika majadiliano yanayoendelea na kutoa maoni kuhusu nyanja mbalimbali za maudhui ya YouTube.
  • Waingie katika akaunti kwenye YouTube ili watume ripoti kuhusu maudhui kama sehemu ya mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele.
  • Watoe anwani yao ya barua pepe au angalau anwani ya mtu mmoja katika shirika lao ambaye ndiye mtu wa kuendelea kuwasiliana naye kuhusu mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele. Tutatuma barua pepe baada ya kipindi fulani kuhusu mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele kwenye anwani hii ya barua pepe.

Washiriki wote wanaoshiriki kwenye mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele wako chini ya mkataba wa kutofichua siri (NDA).

YouTube inahifadhi haki ya kukataza mtu kushiriki kwenye mpango huu, kubadilisha mahitaji ya mpango au kusitisha mpango kwa hiari yetu binafsi.

Mchakato wa kukagua ripoti

Wadhibiti wa maudhui kwenye YouTube hukagua video zilizoripotiwa na Wapigaripoti Wenye Kipaumbele kulingana na Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube. Maudhui yanayoripotiwa na Wapigaripoti Wenye Kipaumbele hayaondolewi kiotomatiki au kushughulikiwa kwa njia tofauti kisera, viwango sawa vinatumika kwa ripoti zinazopokelewa kutoka kwa watumiaji wengine. Lakini, kwa sababu ya kiwango cha juu cha usahihi katika maudhui husika, timu zetu zinazipa kipaumbele ripoti kutoka kwa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele kufanyiwa ukaguzi.

Mpango wa Wapigaripoti Wenye Kipaumbele unapatikana tu kwa ajili ya kuripoti uwezekano wa kuwepo kwa ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya. Si mfumo wa kuripoti maudhui ambayo huenda yanakiuka sheria za nchi. Maombi yanayotokana na sheria za nchi yanaweza kutumwa kwa kufuata maagizo yaliyo hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8194147776571122207
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false