Sasisha uanachama wako wa Premium

Wanachama wa YouTube Premium au YouTube Music Premium watatozwa kiotomatiki bei ya uanachama mwanzoni mwa kila kipindi cha kutozwa hadi utakapoghairi.

Pata maelezo zaidi kuhusu kusasisha uanachama wako unaolipiwa hapo chini.

YouTube Premium

Kusasisha mapendeleo yako ya malipo na uanachama

Ikiwa umejiunga kupitia programu ya YouTube ya iOS, unaweza kusasisha chaguo zako za malipo na usajili kwenye iTunes.

Gharama zinazojirudia nchini India

Kutokana na masharti ya eMandate ya Benki Kuu ya India, unapaswa kuthibitisha au kuweka upya maelezo yako ya malipo ili kudumisha uwezo wa kufikia uanachama wako unaorudiwa. Ili ufanye hivyo, fuata maagizo kwenye programu ya YouTube au kwenye youtube.com. Kumbuka kuwa huenda benki yako isitumie malipo yanayorudiwa kwa sasa. Angalia orodha ya benki zinazoruhusu mfumo wa malipo yanayorudiwa au upate maelezo zaidi.

Kusasisha ili utumie mpango wa familia wa YouTube

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha uanachama binafsi wa YouTube Premium uwe mpango wa familia wa YouTube.

Kubadilisha kutoka mpango wa familia utumie uanachama wa mtu mmoja

YouTube Music Premium

Kusasisha mapendeleo yako ya malipo na uanachama

Ikiwa umejiunga kupitia programu ya YouTube Music ya iOS, unaweza sasisha chaguo zako za malipo na usajili kwenye iTunes.

Gharama zinazojirudia nchini India

Kutokana na masharti ya eMandate ya Benki Kuu ya India, unapaswa kuthibitisha au kuweka upya maelezo yako ya malipo ili kudumisha uwezo wa kufikia uanachama wako unaorudiwa. Ili ufanye hivyo, fuata maagizo kwenye programu ya YouTube au kwenye youtube.com. Kumbuka kuwa huenda benki yako isitumie malipo yanayorudiwa kwa sasa. Angalia orodha ya benki zinazoruhusu mfumo wa malipo yanayorudiwa au upate maelezo zaidi.

Kusasisha ili upate uanachama wa YouTube Premium

Iwapo una uanachama wa YouTube Music Premium unaotumika, unaweza kusasisha upate uanachama wa YouTube Premium wakati wowote. Ili ujisajili kwenye YouTube Premium:
  1. Ingia katika akaunti yako ya YouTube Music Premium.
  2. Nenda kwenye music.youtube.com/paid_memberships kisha Ofa za YouTube.
  3. Chini ya Premium, bofya Pata maelezo zaidi.
  4. Ili ujiunge na YouTube Premium, fuata hatua hizi.

Kusasisha ili utumie mpango wa familia wa YouTube

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusasisha uanachama binafsi wa YouTube Music Premium uwe mpango wa familia wa YouTube.

Kubadilisha kutoka mpango wa familia utumie uanachama wa mtu mmoja

Ikiwa umejumuishwa kwenye mpango wa familia wa YouTube, pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuondoka katika kikundi cha familia ili upate uanachama binafsi.

Kumbuka: Kuanzia mwaka 2022, wateja wapya wa YouTube Premium na Music Premium waliojisajili kupitia kifaa cha Android watatozwa kupitia Google Play. Mabadiliko haya hayataathiri wateja waliopo. Unaweza kutembelea payments.google.com ili uone utozaji wa hivi majuzi na uangalie jinsi unavyotozwa. Ili uombe urejeshewe pesa kwa ununuzi uliofanya kwenye Google Play, fuata hatua zilizoelezwa hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
361708862849795241
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false