Kuongeza au kupunguza kasi ya kucheza video za YouTube

Unaweza kucheza video katika kasi tofauti au kusogeza mbele na kurudisha nyuma kwenye vifaa vingi.

  1. Nenda kwenye video.
  2. Elea juu ya kichezaji kisha ubofye Mipangilio .
  3. Bofya Kasi.
  4. Chagua kasi ambayo ungependa kutumia kucheza video.

Ili usogeze mbele: 

1. Bofya na ushikilie popote kwenye video ili kuicheza kwa kasi ya mara 2. 

2. Achilia mbofyo wako ili uache kusogeza mbele. 

Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vinavyokusaidia kudhibiti hali yako ya utazamaji kwenye YouTube

Televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vya kutiririsha

Kumbuka: Huenda kasi ya kucheza isipatikane kwenye vifaa vya kutiririsha na televisheni zote zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti.
  1. Kwenye ukurasa wa kutazama wa video, chagua Mipangilio .
  2. Chagua Kasi.
  3. Chagua kasi ambayo ungependa kutumia kucheza video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10820883230849758063
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false