Muda wa kusubiri kutiririsha mubashara

Muda wa kusubiri mtiririko ni muda ulio kati ya kamera yako kurekodi tukio na tukio kuonyeshwa kwa watazamaji. Wakati unaweka mipangilio ya mtiririko wako mubashara, fikiri kuhusu jinsi kiwango cha muda wa kusubiri kinavyoweza kuwaathiri watazamaji wako.

Ukipiga gumzo moja kwa moja na watazamaji, muda wa chini wa kusubiri ni bora zaidi ili kujibu maoni na maswali. Kumbuka kuwa kupitia muda wa chini wa kusubiri, huenda watazamaji wakaona uakibishaji zaidi wa uchezaji.

Iwapo huwasiliani na hadhira yako, muda wa juu zaidi wa kusubiri si tatizo.

Kwa nini kuna uhusiano kati ya muda wa kusubiri na ubora?

Kadri muda wa kusubiri ulivyo mdogo, ndivyo uakibishaji wa chini wa kusoma mapema utakavyokuwa kwenye kicheza video. Kiasi cha uakibishaji wa kusoma mapema ni muhimu kwa sababu ni chanzo kikuu cha muda wa kusubiri mtiririko. Kupitia muda wa chini wa kusubiri, kuna uwezekano mkubwa kwa watazamaji kuathiriwa na matatizo kati ya programu ya kusimba na kichezaji.
Msongamano kwenye mtandao na vigezo vingine vinaweza pia kusababisha matatizo ya kutiririsha mubashara, ambayo yanaweza kuchelewesha mtiririko wako. Ucheleweshaji unaweza kutokea wakati una mtandao mkubwa ambao unaweza kustahimili kasi yako ya wastani ya biti ya utiririshaji.
Kwa jumla, kichezaji cha watazamaji wako kinaweza kushughulikia mabadiliko haya ya kasi ya intaneti kwa kuhifadhi baadhi ya data ya ziada ya mtiririko mubashara. Utendaji huu unafahamika kama Ubora wa Uakibishaji katika Takwimu za Wajuaji.

Jinsi ya kubadilisha muda wa kusubiri mtiririko mubashara

Katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja:

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube. Upande wa juu kulia, bofya Buni kisha Tiririsha Mubashara.
  2. Katika sehemu ya juu, bofya Tiririsha au Dhibiti. Buni mtiririko au ufungue mtiririko ulioratibiwa.
  3. Kwenye dashibodi ya mtiririko, bofya Mtiririko Mipangilio.
  4. Chini ya "Muda wa kusubiri mtiririko," chagua muda unaopenda wa kusubiri.

Kamera ya wavuti na mtiririko kwenye kifaa cha mkononi huwekewa mipangilio ya ushirikishaji. Huwezi kuziwekea muda wa kusubiri mtiririko mubashara.

Kuna chaguo 3 za muda wa kusubiri mtiririko mubashara:

Muda wa kawaida wa kusubiri

Inafaa zaidi kwa: mitiririko mubashara isiyo na hali ya kuwasiliana
Chagua "Muda wa kawaida wa kusubiri" ikiwa hupangi kuwasiliana na hadhira yako kwenye mtiririko mubashara. Chaguo hili ndilo mipangilio ya ubora wa juu zaidi kwa watazamaji kwa kuwa lina idadi ya chini zaidi ya uakibishaji wa watazamaji.
Vipengele vya moja kwa moja na ubora wote unatumika katika muda wa Kawaida wa kusubiri.

Muda mfupi wa kusubiri

Bora zaidi kwa: kiwango cha chini cha mawasiliano na hadhira
Teua chaguo hili ikiwa unapanga kuwa na kiwango cha chini cha mawasiliano na hadhira yako na huhitaji kusubiri majibu, kama vile na kura. Watazamaji wengi wa mtiririko wenye muda mfupi wa kusubiri watapata muda wa kusubiri ulio chini ya sekunde 10. Mipangilio hii ni uwiano bora kati ya chaguo hizo nyingine mbili.
Mipangilio hii hairuhusu ubora wa 4K.

Muda wa chini zaidi wa kusubiri

Bora zaidi kwa: mitiririko mubashara yenye kiwango cha juu cha mawasiliano yenye matukio ya ushirikishaji katika muda halisi
Teua chaguo hili ikiwa ungependa kuwasiliana na hadhira yako. Watazamaji wengi wa mtiririko wenye muda mfupi zaidi wa kusubiri watapata muda wa kusubiri ulio chini ya sekunde 5. Inaweza kuongeza uwezekano kuwa watazamaji wako watapata uakibishaji.
Mipangilio hii hairuhusu ubora wa 4K.
Kumbuka: matatizo ya uingizaji mubashara wa data kwenye mtandao wako yataathiri watazamaji zaidi katika mipangilio hii. Hakikisha kuwa muunganisho wako wa mtandao unaweza kudumisha hali ya kutiririsha katika kasi ya biti utakayochagua. Kwa matokeo bora zaidi, tumia AV1 au HEVC ili upate uthabiti na ubora wa juu zaidi katika kasi yoyote ya biti na ufuate mapendeleo ya programu ya kusimba ya YouTube Moja kwa Moja hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9141873893686293517
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false