Ikiwa unatatizika kupakua video kwenye kivinjari au kifaa chako cha mkononi, fuata hatua za utatuzi zilizo hapa chini.
Iwapo muda wa uanachama wako wa YouTube Premium utaisha, hutaweza tena kufikia video ulizopakua.
Hatua za utatuzi
Jaribu kuingia tena katika YouTube Premium
Tatizo: Hujaingia katika YouTube Premium.
Suluhisho Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti inayohusishwa na uanachama wako wa YouTube Premium.
- Jaribu kuondoka kisha uingie tena katika akaunti inayohusishwa na YouTube Premium.
- Hakikisha kuwa unaona nembo ya YouTube Premium (badala ya nembo ya YouTube) katika YouTube.
Kuangalia hali ya uanachama wako
Tatizo: Huenda muda wa uanachama wako wa YouTube Premium umeisha.
Suluhisho:
Hakikisha kuwa muda wa uanachama wako wa YouTube Premium haujaisha.
Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu Mipangilio
Ununuzi na uanachama.
- Iwapo ulipoteza idhini ya kufikia YouTube Premium hivi majuzi na ukajisajili tena, itachukua saa chache kabla ya video ulizohifadhi kuonekana ukishajisajili tena.
- Iwapo utahitaji kutazama video sasa hivi, gusa Menyu
na uchague Jaribu kupakua tena.
- Iwapo muda wa uanachama wako wa YouTube Premium utaisha, hutaweza tena kufikia video ulizopakua. Ili uweze kufikia vipakuliwa vyako tena, jisajili kwenye Uanachama wa Premium.
Angalia uthabiti wa muunganisho wa intaneti
Tatizo: Muunganisho dhaifu wa intaneti unaweza kuzuia upakuaji.
Suluhisho Unahitaji muunganisho thabiti wa intaneti ili upakue video. Hakikisha kuwa kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi wenye kasi ya mbps 3 au ya kasi zaidi au mtandao wa simu wenye kifurushi cha data kinachoruhusu kasi ya 3G, 4G au LTE. Iwapo huna uhakika kuhusu kasi ya sasa ya intaneti yako, unaweza kufanya jaribio la kasi ya intaneti yako mtandaoni.
Angalia matumizi ya data ya mtandao wa simu
Tatizo: Huenda umefikia kikomo chako cha data ya mtandao wa simu ikiwa unatumia kifaa cha mkononi.
Suluhisho: Ikiwa unatumia data ya mtandao wa simu, angalia matumizi yako ya data. Ikiwa umefikia kikomo chako, utahitaji kuunganisha kwenye Wi-Fi au ununue data zaidi ili upakue video. Angalia mipangilio kwenye kifaa chako cha mkononi ili uhakikishe kuwa umewasha data ya chinichini katika YouTube.
Angalia kikomo cha vifaa vya kupakua
Tatizo: Huenda umefikia idadi ya juu zaidi ya vifaa vinavyoruhusiwa kupakua kwa kutumia YouTube Premium.
Suluhisho: Angalia umetumia vifaa vingapi kupakua. Ikiwa umefikia kikomo, utahitaji kusafisha nafasi kwa kuondoa vipakuliwa vilivyo katika vifaa ambavyo havitumiki. Pata maelezo zaidi kuhusu vikomo vya vifaa kwenye YouTube Premium.