Kubadilisha akaunti yako iliyounganishwa ya AdSense katika YouTube

Ikiwa tayari umeidhinishwa kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kubadilisha akaunti ya AdSense katika YouTube inayohusiana na chaneli yako ya YouTube. Endelea kutumia akaunti ya AdSense katika YouTube kisha uiunganishe kwenye chaneli yako ili uendelee kutimiza masharti ya kutumia Mpango wa Washirika wa YouTube.

Kumbuka kwamba unaweza kubadilisha akaunti yako iliyounganishwa ya AdSense katika YouTube mara moja tu kila baada ya siku 32.
  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Chagua sehemu ya Chuma mapato kwenye menyu ya kushoto.
  3. Katika Chaguo za Mpango wa Washirika wa YouTube, utaona maelezo kuhusu akaunti ya AdSense katika YouTube ambayo umeunganisha kwenye chaneli yako ya YouTube kwa sasa. 
  4. Chagua Badilisha ili uelekezwe kwenye AdSense katika YouTube. Utahitaji kuweka nenosiri lako kisha uthibitishe upya ukitumia mbinu utakayochagua. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha upya akaunti yako ya YouTube.
  5. Utaelekezwa kwenye AdSense katika YouTube ili uunganishe akaunti yako iliyopo au ufungue akaunti mpya. 
    • Akaunti iliyopo: Ikiwa tayari una akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube, unahitaji kuingia katika akaunti ukitumia akaunti ya Google unayotumia kufikia akaunti yako iliyopo. Kumbuka kwamba akaunti hii inaweza kuwa tofauti na vitambulisho ambavyo huwa unatumia kuingia katika YouTube. 
    • Akaunti mpya: Ikiwa unafungua akaunti mpya ya AdSense katika YouTube, tafadhali kumbuka kwamba tunaruhusu akaunti moja pekee kwa kila mtumiaji. 
  6. Akaunti ambayo umechagua itakuwa sehemu ya juu ya skrini na URL ya chaneli yako ya YouTube itakuwa katika sehemu ya "Tovuti yako." Ikiwa maelezo haya ni sahihi, chagua Kubali uunganishaji. Utaelekezwa kwenye YouTube (usipoelekezwa, chagua Elekeza kwingine).
  7. Umemaliza kuweka mipangilio ya AdSense katika YouTube! Ili uweke mapendeleo yako ya uchumaji wa mapato, fuata hatua zinazofuata kwenye skrini.

Baada ya kuunganisha akaunti yako ya AdSense katika YouTube na chaneli yako ya YouTube, inaweza kuchukua hadi saa 24 kabla ya mifumo yetu kuonyesha uunganishaji huo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8628032142453682162
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false