Hapa YouTube, tunaamini katika kushughulikia matumizi mabaya kwa njia zinazoleta athari halisi na chanya huku pia tukifanya tovuti hii kuwa bora kwa watayarishi na watazamaji kote duniani. Mojawapo ya njia ambazo tunajaribu kufanya hivi ni kuzuia matumizi ya lebo zinazopotosha au ambazo hazina uhusiano na maudhui.
Ikiwa video yako imetambuliwa kuwa inayokiuka sera zetu, inaweza kufungwa kuwa ya faragha. Video ikifungwa kuwa ya faragha, haitaonekana kwa umma. Ikiwa mtazamaji ana kiungo cha video hiyo, itaonekana kama isiyopatikana.
Je, nitaarifiwa vipi kuhusu hatua hii?
Utapokea barua pepe inayoeleza kwamba mojawapo ya video zako imefungwa kuwa ya faragha. Katika baadhi ya kesi, huenda ukaweza kukata rufaa. Ikiwa hivyo, kama sehemu ya mchakato wa kukata rufaa, huenda ukatumiwa ujumbe zaidi unaoeleza jinsi ya kuendelea kupitia barua pepe.Ni nini hufanyika kwa video yangu ikiwa itafungwa kuwa ya faragha?
Video ikifungwa kuwa ya faragha, haitaonekana kwenye chaneli yako au kwenye matokeo ya utafutaji na haitaonekana kwa watumiaji wengine. Hakuna mtu anayekufuata atakayeona video ambayo imefungwa kuwa ya faragha. Tofauti na video za faragha zilizochaguliwa na mtumiaji, hutaweza kubadilisha hali ya video hadi baada ya ombi lako la ukaguzi upya wa video lifanikiwe.
Hii ikifanyika, hakuna onyo linalowekwa kwenye akaunti yako. Unaweza kurekebisha matatizo yoyote na ukate rufaa ili video hiyo ikaguliwe upya moja kwa moja kwenye kidhibiti chako cha video. Angalia hapa chini ili upate hatua za jinsi ya kukata rufaa.
Ninawezaje kutatua hili?
- Kagua Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
- Hakikisha kwamba maudhui yako yanatii mwongozo wetu.
- Kata rufaa kwenye Studio ya YT ikiwa umetatua matatizo yoyote au ikiwa unafikiri kuwa tumekosea.
Kwa video ambazo zimefungwa kuwa za faragha kwa sababu ya kupakiwa kupitia huduma ya API isiyoweza kuthibitishwa, hutaweza kukata rufaa. Utahitaji kupakia video hiyo upya kupitia huduma ya API iliyothibitishwa au kupitia programu/tovuti ya YouTube. Huduma ya API ambayo haijathibitishwa pia inaweza kutuma ombi la ukaguzi wa API.
Ili uhakikishe kwamba video yako haifungwi kuwa ya faragha tena, usichapishe maudhui ambayo:
- Yana lebo zisizohusiana au zinazopotosha kwenye sehemu za “Maelezo” na “Lebo” za video yako. Pata maelezo zaidi kwenye makala yetu kuhusu mbinu bora za metadata.
- Yamepakiwa na huduma ya API ya watu wengine ambayo haijathibitishwa.
Kumbuka kwamba orodha hii si kamili.