Kutuma ombi la kurejeshewa pesa kwa ununuzi kwenye YouTube TV

Ikiwa vipengele vilivyojumuishwa kwenye uanachama wako YouTube Tv vina hitilafu au havifanyi kazi kama ilivyobainishwa, bofya kitufe hapa chini ili uombe kurejeshewa pesa. Ukirejeshewa pesa, utapoteza uwezo wa kufikia YouTube TV papo hapo na utarejeshewa pesa zako.

TUMA OMBI LA KUREJESHEWA PESA

Ukiona tozo ambayo hukufanya, unaweza ukaripoti utozaji ambao haujaidhinishwa badala yake.

Kupata maelezo zaidi kuhusu kurejesha pesa katika YouTube TV

  • Kwa kawaida, maombi ya kurejeshewa pesa kwenye kadi za mikopo huchukua siku 3 hadi 5 za kazi.
    • Muda wa kuchakata unaweza kuathiriwa na kampuni iliyotoa kadi yako. Wakati mwingine, maombi ya kurejesha pesa yanaweza kuchukua hadi siku 10 za kazi ili kuchakatwa.
    • Ikiwa kadi yako ya mikopo haitumiki tena, pesa unazorejeshewa zitatumwa kwa benki iliyotoa kadi yako. Ili urejeshewe pesa, wasiliana na benki.
       
  • Ukijisajili kwenye YouTube TV kupitia mtoa huduma za simu au mtoa huduma za intaneti:
    • YouTube haiwezi kukurejeshea pesa.
    • Sera za kurejesha pesa za mtoa huduma wako zitatumika. Wasiliana nao moja kwa moja ili uombe kurejeshewa pesa au kwa maswali yoyote yanayohusiana na malipo yako.
       
  • Unaweza kukatisha au kusitisha uanachama wako wakati wowote.
    • Haturejeshi pesa au salio kwa vipindi vya bili ambavyo havijakamilika.
    • Ukikatisha uanachama wako, utaendelea kuufikia hadi mwisho wa kipindi chako cha bili. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11786378741856744091
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false