Faharasa ya tafsiri na unukuzi

  • ASR: Utambuzi wa Matamshi Kiotomatiki. YouTube hutumia kipengele cha utambuzi wa matamshi kiotomatiki ili kuweka manukuu ya kiotomatiki kwenye video. Kipengele hiki kinapatikana kwa Kiingereza, Kiholanzi, Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kijapani, Kikorea, Kireno, Kirusi na Kihipasnia. ASR haipatikani katika video zote.
  • Manukuu ya kiotomatiki: Wimbo wenye manukuu yanayowekwa na kipengele cha Utambuzi wa Matamshi Kiotomatiki.
  • Manukuu: Inatumika kurejelea unukuzi wa lugha ile ile pamoja na manukuu yaliyotafsiriwa yanayoonekana kama maandishi kwenye video. Kwa chaguomsingi, "manukuu" hurejelea unukuzi katika lugha ile ile. 
  • Manukuu yenye maelezo: Manukuu yenye maelezo huonyesha sauti iliyo kwenye video katika maandishi. Maudhui haya kimsingi ni ya kuwasaidia watazamaji walio na matatizo ya kusikia au viziwi. Maudhui haya hujumuisha manukuu ya maneno yanayosemwa na vipengee vya sauti, kama vile "[muziki unacheza]" au "[kicheko]." Manukuu yenye maelezo pia yanaweza kumtambulisha mzungumzaji, kama vile "Mike: Hujambo!" au kwa kutumia nafasi kwenye skrini.
  • Changia: Ili kubuni au kubadilisha tafsiri za metadata au wimbo mpya wenye manukuu yanayochapishwa kwenye video.
  • Mchango: Tafsiri ya metadata, manukuu, manukuu mapya yenye maelezo au yaliyobadilishwa ambayo huhakikiwa na kuchapishwa kwenye video.
  • Mchangiaji: Mtu aliyejitolea kutuma maudhui mapya ya manukuu, manukuu yenye maelezo, au tafsiri ya metadata; au ambaye amebadilisha au kuhakiki maudhui ya wachangiaji wengine.
  • Mtayarishi: Mmiliki au aliyepekia video.
  • Tuma: Kutuma wimbo ulioandikwa kikamilifu au ambao haujakamilika uhakikiwe ili uchapishwe kwenye video.
  • Wasilisho: Tafsiri au manukuu yaliyoandikwa kikamilifu au ambayo hayajakamilika yanayotumwa yahakikiwe ili yachapishwe kwenye video.
  • Manukuu: Nyimbo za maandishi zinazoambatana na video katika lugha tofauti na inayozungumzwa kwenye video hiyo. Kimsingi maudhui haya huwalenga watazamaji wanaozungumza lugha ya kigeni. Maudhui ni tafsiri ya maneno yanayozungumzwa na maandishi yanayoonekana sehemu ya chini au chini ya video ("tafsiri za mazungumzo").
  • Kuweka muda: Mtu anapotuma manukuu, huwa tunatumia seva yetu ya usawazishaji kupanga manukuu hayo kiotomatiki na video, hivyo kutayarisha wimbo wa manukuu uliowekewa muda.
  • Unukuzi: Maandishi yasiyo na muda yaliyonukuliwa jinsi yalivyo kwenye video.
  • Tafsiri: Kichwa, maelezo au manukuu yanayowekwa kwa kutafsiri metadata au manukuu yaliyopo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15253437829569642969
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false