Jinsi ambayo video zilizotafsiriwa huonyeshwa kwa watazamaji
YouTube hutumia ishara ili kulinganisha kiotomatiki lugha ya video (jina, maelezo na manukuu) na mapendeleo ya watazamaji. Ishara zinaweza kuwa ni pamoja na lugha, mahali na video ambazo mtazamaji amezitazama hivi karibuni. Ishara hizi huonyesha video katika lugha inayomfaa zaidi mtazamaji. Huenda lugha hii ikawa tofauti na mpangilio wa lugha kuu ya mtazamaji.
Ikiwa mtazamaji atabadilisha mipangilio yake ya lugha kwenye YouTube, video zote hazitapatikana papo hapo katika lugha atakayoichagua. Hata ikiwa video zimetafsiriwa kwa lugha husika.
Kwa mfano, ikiwa mtazamaji atabadilisha lugha yake kuwa Kiingereza, lakini ishara zinaonyesha kwamba anaelewa Kifaransa pia, basi anaweza kupata toleo halisi la Kifaransa.
Kutazama video zilizotafsiriwa
Ikiwa ungependa kutazama tafsiri za video, unaweza kuitazama video katika lugha tofauti.
- Fungua dirisha la kivinjari katika hali fiche ukitumia Chrome, Firefox, MS Edge au Opera.
- Nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa video yako kwenye YouTube.
- Bofya picha yako ya wasifu
Lugha
Chagua lugha unayopendelea.
Unaweza pia kutumia manukuu kwenye video yanapopatikana.