Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Unaweza kuchagua kufanya vituo ambavyo umejisajili viwe vya faragha au vionekane kwa umma. Kwa chaguomsingi, mipangilio yote imewekwa kuwa ya faragha.
- Faragha: Usajili wako unapowekwa kuwa wa faragha, hakuna watumiaji wengine wanaoweza kuona vituo ulivyojisajili. Akaunti yako haitaonekana katika Orodha ya Wanaofuatilia kituo, hata ikiwa umejisajili.
Kumbuka: Ikiwa unashiriki kwenye gumzo la moja kwa moja la wanaofuatilia kituo pekee, watazamaji wengine wataona hadharani kuwa unafuatilia kituo husika. - Hadharani: Usajili wako unapowekwa hadharani, watumiaji wengine wanaweza kuona vituo unavyofuatilia. Usajili wako unaorodheshwa kwenye ukurasa wako wa kwanza wa kituo. Akaunti yako inaorodheshwa katika Orodha ya Wanaofuatilia kwa kituo chochote unachofuatilia.
Kufanya usajili wa kituo chako uonekane kwa umma au uwe wa faragha
- Ingia katika akaunti ya YouTube kwenye kompyuta.
- Kwenye upande wa juu kulia, bofya picha yako ya wasifu .
- Bofya Mipangilio .
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Faragha.
- Washa au zima Weka usajili wangu wote uwe wa faragha.