Unaweza kupakia na kucheza video za 3D kama video mstatili za 3D, VR180, au 360 3D (video za VR).
YouTube hutumia muundo wa stereo wa kushoto-kulia (LR) upande kwa upande kwa video za 3D. Video inapaswa kuwa na metadata ya stereo kama:
- Kisanduku cha st3d katika .mov/.mp4,
- Kipengee cha StereoMode kinawekwa kuwa upande kwa upande LR katika .mkv/.webm, au
- Metadata ya FPA katika vijajuu vya H264 SEI
Ikiwa video yako ya 3D haina metadata ya 3D, unaweza kuiongeza kwa kutumia programu unayopendelea ya kuhariri video, kama vile Sony Vegas Pro au GoPro Studio. Unaweza pia kutumia zana ya FFmpeg.
Video ya H.264 iliyosimbwa katika metadata ya .mov au .mp4
ffmpeg -i input_file.mkv -vcodec libx264 -x264opts "frame-packing=3" output_file.mp4
Video ya Matroska na WebM
ffmpeg -i input_file.mkv -c copy -metadata:s:v:0 stereo_mode=1 output_file.mkv
Kumbuka: Baada ya kupakia video iliyo na lebo, itacheza tu kama video ya 3D baada ya kuchakatwa kikamilifu. Kabla ya kuchakatwa, itacheza upande kwa upande (kwa maana nyingine haitacheza katika 3D).