Kutumia msimbo au kadi ya zawadi ya YouTube

Tumia msimbo au kadi ya zawadi ya YouTube kufanya ununuzi kwenye YouTube. Ukiitumia, msimbo au kadi yako ya zawadi itaongezaSalio lako la Google Play. Unaweza kisha kutumia salio kulipia:

  • YouTube Premium
  • YouTube Music Premium
  • YouTube TV
  • Filamu na Vipindi vya televisheni kwenye YouTube
  • Maudhui dijitali kwenye Google Play
  • Uanachama katika kituo
  • Super Chats na Super Stickers (kwenye vifaa vya mkononi)

Pata maelezo zaidi kuhusu Salio la Google Play hapa. Kwa hitilafu za Salio lako la Google , wasiliana na usaidizi wa Google Play.

Ili kunua kadi ya zawadi nchini Meksiko

Unaweza kununua kadi za zawadi katika wauzaji wengi nchini Meksiko, ikiwa ni pamoja na maduka ya Oxxo, katika viwango vya MX$100, MX$300, au MX$600.

Tumia msimbo au kadi ya zawadi ya YouTube

  1. Ingia katika Akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kadi yako ya zawadi.
  2. Tembelea URL iliyoorodheshwa kwenye kadi yako ya zawadi au nenda kwenye youtube.com/redeem.
  3. Weka msimbo kwenye kadi yako ya zawadi.
  4. Bofya Inayofuata.
  5. Chagua unachopenda kununua iwapo unataka kutumia salio lako mara moja. Weka Salio la Google Play kama njia yako ya kulipa.
  6. Bofya Nunua ili ukamilishe shughuli ya malipo.

Weka pesa kwenye Salio laki la Google Play ili ulipie uanachama wa sasa unaolipiwa wa YouTube.

  1. Ingia katika Akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kadi yako ya zawadi.
  2. Tembelea URL iliyoorodheshwa kwenye kadi yako ya zawadi au nenda kwenye youtube.com/redeem
  3. Weka msimbo kwenye kadi yako ya zawadi.
  4. Bofya Inayofuata.

Baada ya kutumia kadi yako ya zawadi, hakikisha imechaguliwa kama njia ya kulipa ya uanachama wako wa YouTube Premium, YouTube Music Premium, au YouTube TV:

  1. Ingia katika akaunti ya payments.google.com.
  2. Pata uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube na uchague Dhibiti.
  3. Chini ya "Unavyolipa," bofya Badilisha njia ya kulipa.
  4. Chagua Salio lako la Google Play.
  5. Bofya Hifadhi.

Omba kurejeshewa pesa ya kadi ya zawadi au msimbo

Wasiliana na Amazon au muuzaji ambapo ulinunua kadi ya zawadi ili utume ombi la kurejeshewa pesa.
Kumbuka: Ili utumie kadi ya zawadi, ni sharti nchi/eneo linalohusishwa na Akaunti yako ya Google lilingane na nchi/eneo ambako kadi yako ya zawadi inatolewa. Ukiona ujumbe unaosema kadi za zawadi hazitumiki katika nchi/eneo lako, thibitisha kuwa nchi/eneo lako la kadi ya zawadi linalingana na nchi/eneo unakoishi. Ikiwa unahitaji kurekebisha anwani yako au nchi/eneo unakoishi katika Akaunti yako ya Google, unaweza usiweze kutumia salio lako lililopo la Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5430361724679861554
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false