Video yenye ubora wa chini baada ya kupakia

Unapopakia video, kwanza itachakatwa katika ubora wa chini. Hatua hii inakusaidia kukamilisha mchakato wa kupakia video kwa haraka zaidi. Utaratibu wa kupakia ukikamilika, video yako itaweza kutiririshwa kwenye ubora wa chini, katika vifaa mbalimbali.

Ubora wa juu, kama vile 4K au 1080p, unaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuchakatwa. Wakati uchakataji huu unaendelea, huenda video yako ikaonekana kuwa haina chaguo za ubora wa juu kwa saa kadhaa. Baada ya uchakataji wa ubora wa juu kukamilika, chaguo za ubora wa juu zitapatikana kwenye video yako.

Desturi bora za video zenye ubora wa juu

Unaweza kwanza kupakia video yako ikiwa haijaorodheshwa wakati wowote kisha uifanye ipatikane kwa umma baada ya uchakataji wa ubora wa juu kukamilika. Kwa kupakia video ikiwa haijaorodheshwa kwanza na kisha kuichapisha baadaye, watazamaji wataona tu video yako katika ubora wa juu.

Ikiwa unataka chaguo za ubora wa HD zionekane kwa haraka zaidi baada ya kupakia, jaribu kupakia video yako ukitumia ubora wa chini au kasi ya picha ya chini. Kwa mfano, kubadili kutoka chaguo la ubora wa 4K hadi 1080p, kutapelekea muda mfupi zaidi wa uchakataji kabla chaguo la HD kupatikana kwa watazamaji.

Kuhusu muda wa uchakataji

Muda wa kuchakata video hutegemea vigezo vingi, kama vile:

  • Muundo wa video
  • Urefu wa video
  • Kasi ya picha
  • Ubora

Video zenye ubora wa juu zaidi, kama vile video za 4K au 1080p, huchukua muda mrefu zaidi kupakia na kuchakata. Hii pia ni dhahiri kwa video zenye kasi ya picha ya juu, kama vile 60-fps.

Kwa mfano, video za 4K zina ukubwa mara nne zaidi ya video za 1080p. Inaweza kuchukua mara 4 zaidi ya muda wa kawaida kwa ubora wa 4K kupatikana kama chaguo kwenye video yako baada ya utaratibu wa upakiaji kukamilika. Video ya 4K yenye urefu wa dakika 60 na kasi ya picha 30 kwa sekunde inaweza kuchukua hadi saa nne kukamilisha uchakataji wa ubora wa juu. Video ya 4K yenye kasi ya picha 60fps itachukua muda mrefu zaidi.

Angalia ubora wa video

Ili uone iwapo video yako imemaliza kuchakata katika chaguo za ubora wa juu zaidi, angalia ukurasa wa kutazama wa video yako.

  1. Fungua ukurasa wa kutazama wa video yako.
  2. Kwenye kicheza video, chagua Mipangilio .
  3. Bofya Ubora.

Iwapo chaguo za ubora wa juu zaidi bado hazipo kwenye video yako, inamaanisha kwamba uchakataji unaendelea chinichini. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadili ubora wa video yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7726601101212135533
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false