Tumia Akaunti yako ya Google kwenye YouTube

Unahitaji Akaunti ya Google ili uingie katika akaunti ya YouTube. Akaunti ya Google hufanya kazi kwenye bidhaa zote za Google (kama vile Gmail, Blogger, Ramani, YouTube na zaidi).

Kuanza | Jinsi na sababu ya kuingia katika akaunti kwenye YouTube na kufungua chaneli ya YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Iwapo umewahi kuingia katika mojawapo ya akaunti ya bidhaa hizi, tayari una Akaunti ya Google. Ili uingie katika akaunti, weka anwani ya barua pepe uliyotumia kwenye bidhaa hizo. Kwa mfano, iwapo unatumia Gmail, ni jina lako la mtumiaji kwenye Gmail. Iwapo huna Akaunti ya Google, unaweza kufungua mpya kwenye YouTube.

Yafuatayo ni maelezo machache muhimu ya kukumbuka kuhusu Akaunti za Google na YouTube:

  • Unaingia katika YouTube ukitumia Akaunti yako ya Google. Ili uingine katika YouTube, weka barua pepe na nenosiri lako la Akaunti ya Google. Baada ya kujisajili kwenye YouTube, kuingia katika akaunti yako ya Google kwenye huduma nyingine ya Google kutakuingiza kiotomatiki kwenye YouTube.
  • Hatua ya kufuta Akaunti yako ya Google itafuta data yako kwenye YouTube, ikiwa ni pamoja na video, maoni na vituo vyote unavyofuatilia. Kabla ya kufuta Akaunti yako ya Google, utahitaji kuthibitisha kwamba unaelewa kuwa utafuta kabisa data yako kwenye huduma za Google, ikiwa ni pamoja na YouTube.
Huenda baadhi ya vituo vya zamani, ambavyo havitumiwi vya YouTube(vilivyofunguliwa kabla ya Mei 2009) visiwe sehemu ya Akaunti ya Google. Huenda vituo hivi vikahitaji kuongezwa kwenye Akaunti ya Google kabla viweze kutumiwa.

Unapoingia kwenye YouTube ukitumia Akaunti yako ya Google, unaweza kutumia vipengele vingi vya YouTube:

  • Kupende video
  • Kuhifadhi Unazopenda
  • Kufuatilia vituo
  • Tazama Baadaye
  • Historia ya Video Ulizotazama
  • Kuripoti video

YouTube inaweza kuweka mapendeleo kwenye mapendekezo ya video kulingana na video ulizotazama na vituo unavyofuatilia.

Ikiwa huna historia ya kutosha ya video ulizotazama hapo awali, vipengele vya YouTube vinavyotegemea historia ya video ulizotazama kukupa mapendekezo ya video, kama vile mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, huondolewa.
 
Isipokuwa ufungue kituo, hutaonekana hadharani kwenye YouTube. Shughuli zako ni za faragha kabisa. Iwapo ungependa kupakia video zako, kutoa maoni kwenye video au kutunga orodha zako za kucheza, unaweza kufungua Kituo cha YouTube wakati wowote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2037364879288816240
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false