Kupata orodha na video ukitumia alama za reli

Alama za reli ni maneno muhimu yanayotanguliwa na alama ya #. Alama za reli hukuruhusu kuunganisha maudhui yako kwa urahisi na video au orodha nyinginezo za kucheza zinazotumia alama sawa ya reli kwenye YouTube na YouTube Music. Pia, alama za reli huruhusu watazamaji na wasikilizaji kutafuta maudhui yanayohusiana kupitia utafutaji.

Weka alama za reli kwenye video zako za YouTube au orodha ya kucheza ya YouTube Music

Unaweza kuweka alama za reli kwenye jina na maelezo unapopakia video au kurekodi Video fupi kwenye YouTube au unapounda orodha ya kucheza kwenye YouTube Music.

Ili uweke alama ya reli kwenye video yako kwenye YouTube:

  1. Weka alama ya # kwenye jina au maelezo kisha anza kuweka mada au neno muhimu unalotaka kuhusisha na video yako. Kisha mfumo wetu utapendekeza alama za reli maarufu kulingana na neno uliloweka.
  2. Chagua alama ya reli iliyopendekezwa ili utangaze video yako kati ya video nyinginezo zinazotumia alama sawa ya reli au unda yako ili upate alama ya reli inayofaa kwa maudhui yako.

Kati ya alama za reli zote unazoweka kwenye maelezo ya video, alama za reli hadi tatu zinazochukuliwa kuwa zinashirikisha zaidi ndizo zitaonekana kwenye jina la video yako. Alama zako za reli bado zitaonekana kwenye maelezo ya video yako na video zako bado zinaweza kuonekana kwenye matokeo ya utafutaji. Alama za reli zilizo kwenye jina na maelezo zitaunganisha kwenye ukurasa wa matokeo unaohusisha video nyingine zinazotumia alama ya reli sawa.

Ili uweke alama ya reli kwenye orodha yako ya kucheza katika YouTube Music:

  1. Chagua Maktaba kisha Orodha za kucheza.
  2. Tafuta orodha ya kucheza uliyounda ambayo ungependa kubadilisha.
  3. Chagua Zaidi ''kisha Badilisha ili ubadilishe jina la orodha yako ya kucheza au kuweka maelezo.
  4. Weka alama ya # kwenye jina au maelezo ya orodha ya kucheza.

Baada ya kuhifadhiwa kwenye jina au maelezo ya orodha ya kucheza, alama za reli hufanya kazi kama viungo vinavyoweza kubofyeka. Alama za reli zilizo kwenye jina na maelezo zitaunganisha kwenye ukurasa wa matokeo unaohusisha video nyingine na orodha za kucheza zinazotumia alama ya reli sawa.

Alama za reli Zinazopendekezwa:

Unapoweka maandishi kwenye Video fupi na kuanza kuongeza alama ya reli, utaona mapendekezo yakukusaidia kutumia alama za reli zinazofaa kwwenye maudhui haya. Alama hizi za reli hupendekezwa kulingana na maandishi yoyote yaliyowekwa pamoja na mapendekezo ya upakuaji wa maudhui uliotangulia.

Mapendekezo ya alama za reli yaliyotumika hapo awali yatakuwa na aikoni ya saa kando yake ili kuonyesha kwamba uliyatumia hapo awali.

Sera ya matumizi ya alama za reli

Kama ilivyo kwa video zinazopakiwa kwenye YouTube, ni lazima alama za reli zitii Mwongozo wa Jumuiya yetu. Alama za reli zinazokiuka sera zetu hazitaonekana chini ya maudhui yako na zinaweza kuondolewa. Hakikisha unafuata sera hizi unapotumia alama hizi za reli:

  • Usiweke nafasi: : Alama za reli hazitakiwi kuwa na nafasi zozote. Ikiwa unataka kuweka maneno mawili kwenye alama ya reli, unaweza kuyaunganisha pamoja (#TwoWords, #twowords).
  • Kuweka lebo nyingi: Usiweke lebo nyingi kwenye video au orodha moja ya kucheza. Jinsi unavyoweka lebo nyingi, ndivyo unavyopunguza uwezekano wa video au orodha ya kucheza kupatikana kwa watazamaji au wasikilizaji wanaotafuta. Iwapo video au orodha ya kucheza ina zaidi ya alama za reli 60, tutapuuza kila alama ya reli kwenye maudhui hayo. Kuweka lebo nyingi kunaweza kusababisha video yako iondolewe kwenye video ulizopakia au utafutaji.
  • Maudhui ya kupotosha: Usiweke alama za reli ambazo hazihusiani moja kwa moja na video au orodha ya kucheza. Alama za reli zinazopotosha au zisizohusiana zinaweza kusababisha video au orodha yako ya kucheza kuondolewa. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera za Metadata ya Kupotosha.
  • Unyanyasaji: Usiweke alama ya reli kwa lengo la kunyanyasa, kudhalilisha, kutishia, kufichua au kuhatarisha maisha ya mtu binafsi au kikundi. Kukiuka sera hii kutasababisha video au orodha yako ya kucheza kuondolewa. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera za Unyanyasaji na Uchokozi wa Mtandaoni.
  • Matamshi ya Chuki: Usiweke alama za reli zozote zinazochochea vurugu au chuki dhidi ya watu binafsi au vikundi. Usiweke alama za reli zilizo na lugha ya ubaguzi wa rangi, kijinsia au unyanyasaji mwingine. Kukiuka sera hii kutasababisha video au orodha yako ya kucheza kuondolewa. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera yetu dhidi ya Matamshi ya Chuki.
  • Maudhui ya ngono: Kuweka alama za reli zilizo na lugha chafu au ya kingono kunaweza kusababisha video au orodha yako ya kucheza kuondolewa. Iwapo video ina maudhui yanayokusudia kuchochea ngono, ina uwezekano mdogo wa kukubaliwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera ya Maudhui ya Ngono.
  • Lugha chafu: Matumizi ya lugha chafu au maneno ya kukera kwenye alama zako za reli yanaweza kusababisha kuwekewa mipaka ya umri au kuondolewa kwa video au orodha ya kucheza.
  • Alama zisizo za reli: Ingawa inaruhusiwa kuweka alama za reli, (bado) hairuhusiwi kuweka lebo za kawaida za maelezo au sentensi zinazojirudia katika maelezo. Ukikiuka sera hii, video au orodha yako ya kucheza inaweza kuondolewa au kuadhibiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera za Metadata ya Kupotosha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9693537928303491273
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false