Kurekebisha hitilafu ya upakiaji kwenye programu za wahusika wengine

YouTube imepata toleo jipya la huduma ya API ya Data ya YouTube v3 kutoka lile la huduma ya API ya Data ya YouTube v2. Hii API ni teknolojia mpya zaidi ya kusaidia kuwasha programu za wengine na kuzijumuisha na YouTube. Wasanidi wa programu za wengine walifahamishwa kuhusu mabadiliko haya mwaka wa 2014 ili kuwapa muda wa kutosha wa kutwaa na kutumia teknolojia yetu mpya. Tumewasaidia kuhamia kwenye teknolojia yetu mpya zaidi tangu wakati huo.

Programu nyingi za wengine tayari zinatumia huduma ya API ya Data ya YouTube toleo la 3, kwa hivyo hakuna kitakachobadilika kuhusu jinsi unavyotumia programu hizi za wengine zilizosasishwa, wakati wa kupakia video kwenye YouTube.

Programu za wengine ambazo hazitumii huduma mpya zaidi ya API ya Data ya YouTube v3, zinaweza kusababisha matatizo unapopakia video kwenye YouTube. Huwezi kupakia video kwenye YouTube ukitumia programu hizi. 

Kidokezo: Unaweza kuombwa uthibitishe upya unapozipa ruhusa programu za wengine.

Kutatua hitilafu kupakia

Ukipata ujumbe unaosema “mchanganyiko wa jina la mtumiaji au nenosiri si sahihi" unapojaribu kuingia katika akaunti ya programu ya wengine, tumia hatua hizi ili kupakia video yako:

  1. Hamisha video kutoka kwenye programu ya wengine.
  2. Pakia video ukitumia tovuti ya YouTube au programu ya YouTube ya kifaa cha mkononi. 
Unaweza pia kujaribu kusasisha programu ya wengine. Hatua ya kusasisha inaweza kusaidia ikiwa msanidi programu anatoa toleo jipya la programu ambalo linatumia huduma ya API ya Data ya YouTube v3. Ikiwa hatua ya kusasisha programu haisaidii, unaweza kuwasiliana na msanidi wako wa programu wa shirika lingine.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10123390138536997275
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false