YouTube huonyesha video zenye uwiano tofauti kulingana na mfumo na muundo wa video. Kicheza video za YouTube hujirekebisha kiotomatiki kwa ukubwa kwa kila video mahususi.
Jinsi video yako itakavyoonyeshwa
Uwiano wa kawaida wa YouTube kwenye kompyuta ni 16:9. Ikiwa video yako ina uwiano tofauti, kichezaji kitabadilika kiotomatiki kuwa ukubwa unaofaa ili kulingana na video na kifaa cha mtazamaji.
Kwa baadhi ya uwiano wa video na vifaa kama vile video wima za 9:16 kwenye vivinjari vya kompyuta, huenda YouTube ikaweka nafasi zaidi kwa utazamaji bora. Nafasi ni nyeupe kwa chaguomsingi, kijivu kilichokolea wakati Mandhari meusi yamewashwa.
Kwa matokeo bora, usiweke nafasi ya pau nyeusi mjoja kwa moja kwenye video yako. Nafasi huathiri uwezo wa YouTube wa kubadilisha kichezaji ili kifae ukubwa wa video yako na kifaa cha mtazamaji.
Uwiano na ubora unaopendekezwa
Kwa uwiano chaguomsingi wa 16:9, simba katika ubora huu:
- 4320p (8k): 7680x4320
- 2160p (4K): 3840x2160
- 1440p (2k): 2560x1440
- 1080p (HD): 1920x1080
- 720p (HD): 1280x720
- 480p (SD): 854x480
- 360p (SD): 640x360
- 240p (SD): 426x240