Ukiona ujumbe kuhusu hitilafu wakati unatuma mialiko ya chaneli, jaribu hatua za utatuzi zilizo hapa chini.
Chaneli imekabidhiwa kwa mmiliki mwingine wa maudhuiUkiona ujumbe unaosema, “Mtumiaji huyu tayari amekabidhiwa kwa mmiliki wa maudhui OWNER NAME: USERNAME
” inamaanisha kuwa mtumiaji tayari ameunganishwa kwenye Mtandao mwigine wa Chaneli Mbalimbali, kwa mfano.
Mtumiaji anahitaji kutenganisha chaneli kutoka kwa mmiliki huyo wa maudhui kabla ya kualikwa kwenye mtandao wako.
Ukiona ujumbe unaosema, “Mtumiaji huyu tayari amekabidhiwa kwa mmiliki mwingine wa maudhui ambaye hashughuliki: USERNAME
” huenda ikawa ni kwa sababu mmiliki wa maudhui hakumaliza kuhusisha akaunti yake ya AdSense katika YouTube.
Mtumiaji anahitaji kutenganisha chaneli kutoka kwa mmiliki huyo wa maudhui kabla ya kualikwa kwenye mtandao wako.
Wamiliki wa maudhui wasio na shughuli wanaweza kumaliza kuanzisha akaunti ya AdSense katika YouTube kwa kufuata maagizo ya kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube.
Ukiona mojawapo ya ujumbe ufuatao kuhusu hitilafu, jina la mtumiaji lina hitilafu ambayo inahitaji kutatuliwa kabla ualike chaneli kwenye mtandao wako:
- “Jina hili la mtumiaji/kitambulisho cha nje si sahihi:
USERNAME
” - “Mtumiaji huyu hajafungua chaneli ya YouTube na hawezi kuunganishwa:
USERNAME
” - “Mtumiaji huyu hawezi kuunganishwa kwa sababu hahusishwi na Akaunti ya Google:
USERNAME
”
Jina la mtumiaji linachukuliwa kuwa si sahihi ikiwa halilingani na jina halisi la mtumiaji.
Kumbuka kuwa chaneli zilizofunguliwa na Kurasa za Google+ au Wasifu kwenye Google+ huenda zisiwe na majina ya mtumiaji ya asili, lakini hutumia “kitambulisho cha nje,” kinachoweza kupatikana kwa kwenda kwenye chaneli na kunakili herufi 15 baada ya "UC" katika URL.
Ukiona ujumbe unaosema, “Umeshamwalika mtumiaji huyu: USERNAME
,” unaweza kukiomba chaneli iangalie dashibodi na kikubali mwaliko wako.
Ukiona ujumbe unaosema, “Unamsimamia mtumiaji huyu tayari: USERNAME
,” inamaanisha kuwa tayari chaneli imeunganishwa na kidhibiti chako cha maudhui.