Kutatua hitilafu za mialiko ya chaneli

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Ukiona ujumbe kuhusu hitilafu wakati unatuma mialiko ya chaneli, jaribu hatua za utatuzi zilizo hapa chini.

Chaneli imekabidhiwa kwa mmiliki mwingine wa maudhui

Ukiona ujumbe unaosema, “Mtumiaji huyu tayari amekabidhiwa kwa mmiliki wa maudhui OWNER NAME: USERNAME” inamaanisha kuwa mtumiaji tayari ameunganishwa kwenye Mtandao mwigine wa Chaneli Mbalimbali, kwa mfano.

Mtumiaji anahitaji kutenganisha chaneli kutoka kwa mmiliki huyo wa maudhui kabla ya kualikwa kwenye mtandao wako.

Chaneli imekabidhiwa kwa mmiliki wa maudhui ambaye hashughuliki

Ukiona ujumbe unaosema, “Mtumiaji huyu tayari amekabidhiwa kwa mmiliki mwingine wa maudhui ambaye hashughuliki: USERNAME” huenda ikawa ni kwa sababu mmiliki wa maudhui hakumaliza kuhusisha akaunti yake ya AdSense katika YouTube.

Mtumiaji anahitaji kutenganisha chaneli kutoka kwa mmiliki huyo wa maudhui kabla ya kualikwa kwenye mtandao wako.

Wamiliki wa maudhui wasio na shughuli wanaweza kumaliza kuanzisha akaunti ya AdSense katika YouTube kwa kufuata maagizo ya kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube.

Hitilafu za jina la mtumiaji

Ukiona mojawapo ya ujumbe ufuatao kuhusu hitilafu, jina la mtumiaji lina hitilafu ambayo inahitaji kutatuliwa kabla ualike chaneli kwenye mtandao wako:

  • “Jina hili la mtumiaji/kitambulisho cha nje si sahihi: USERNAME
  • “Mtumiaji huyu hajafungua chaneli ya YouTube na hawezi kuunganishwa: USERNAME
  • “Mtumiaji huyu hawezi kuunganishwa kwa sababu hahusishwi na Akaunti ya Google: USERNAME

Jina la mtumiaji linachukuliwa kuwa si sahihi ikiwa halilingani na jina halisi la mtumiaji.

Kumbuka kuwa chaneli zilizofunguliwa na Kurasa za Google+ au Wasifu kwenye Google+ huenda zisiwe na majina ya mtumiaji ya asili, lakini hutumia “kitambulisho cha nje,” kinachoweza kupatikana kwa kwenda kwenye chaneli na kunakili herufi 15 baada ya "UC" katika URL.

Tayari mialiko imetumwa

Ukiona ujumbe unaosema, “Umeshamwalika mtumiaji huyu: USERNAME,” unaweza kukiomba chaneli iangalie dashibodi na kikubali mwaliko wako.

Ukiona ujumbe unaosema, “Unamsimamia mtumiaji huyu tayari: USERNAME,” inamaanisha kuwa tayari chaneli imeunganishwa na kidhibiti chako cha maudhui.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17234749449356117573
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false