Cheza video kiotomatiki

Kipengele cha Kucheza kiotomatiki kwenye YouTube kinarahisisha kufanya uamuzi wa video ya kutazama inayofuata. Kipengele cha Kucheza kiotomatiki kikiwa kimewashwa, video nyingine inayaohusiana itacheza kiotomatiki baada ya video unayocheza kukamilika.

How to Autoplay Videos on YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kumbuka:

  • Kwa watumiaji wa YouTube wenye umri wa miaka 13 hadi 17, kipengele cha Kucheza kiotomatiki kimezimwa kwa chaguomsingi. Ikiwa una umri wa miaka 18 au zaidi, kipengele cha Kucheza kiotomatiki kimewashwa kwa chaguomsingi.
  • Ikiwa unatumia akaunti inayodhibitiwa, unaweza kukosa chaguo la kuwasha/kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki ikiwa mzazi wako amezima kipengele cha Kucheza kiotomatiki kwa ajili yako. Pata maelezo zaidi kuhusu vidhibiti vya wazazi kwenye akaunti zinazodhibitiwa.
  • Unaweza kuweka mipangilio tofauti ya Kucheza kiotomatiki kwenye vifaa tofauti. Kwa mfano, unaweza "Kuwasha" kipengele cha Kucheza kiotomatiki kwenye programu ya YouTube ya kifaa chako cha mkononi na "Kuzima" kipengele hicho unapotazama YouTube kwenye kompyuta yako.
  • Ikiwa unatumia mtandao wa simu, kipengele cha Kucheza kiotomatiki kitazimwa kiotomatiki ikiwa hujatekeleza shughuli yoyote kwa dakika 30. Ikiwa unatumia Wi-Fi, kipengele cha Kucheza kiotomatiki kitazimwa kiotomatiki baada ya saa 4.

Kucheza kiotomatiki kwenye kishikwambi au kifaa chako cha mkononi

Baada ya video inayochezwa kukamilika, kicheza video kitaonyesha video itakayofuata. Ukisogeza kicheza video au kuandika kitu, kama vile maoni au hoja ya utafutaji, video inayofuata haitacheza kiotomatiki.

Washa au uzime kipengele cha Kucheza kiotomatiki kwenye video

  1. Nenda kwenye skrini ya kutazama ya video yoyote.
  2. Katika sehemu ya juu ya kicheza video, Washa au Zima swichi ya Kucheza kiotomatiki kwa kuigusa.

 Washa au uzime kipengele cha Kucheza kiotomatiki katika mipangilio yako

  1. Gusa picha yako ya wasifu.
  2. Gusa mipangilio .
  3. Gusa Kucheza Kiotomatiki.
  4. Washa au uzime kipengele cha Kucheza kiotomatiki.
Kidokezo: Ikiwa kipengele cha Kucheza kiotomatiki kimewashwa lakini hutaki video inayofuata ichezwe, gusa Katisha mwishoni mwa video inayochezwa.

Kucheza kiotomatiki kwenye kompyuta yako

Baada ya video inayochezwa kukamilika, kicheza video kitaonyesha video itakayofuata. Ukisogeza kicheza video au kuandika kitu, kama vile maoni au hoja ya utafutaji, video inayofuata haitacheza kiotomatiki.

Kuwasha au kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki

  1. Nenda kwenye skrini ya kutazama ya video yoyote.
  2. Katika sehemu ya chini ya kicheza video, Washa au Zima swichi ya Kucheza kiotomatiki kwa kuibofya.
Kidokezo: Ikiwa kipengele cha Kucheza kiotomatiki kimewashwa lakini hutaki video inayofuata ichezwe, gusa Katisha mwishoni mwa video inayochezwa.

Kucheza kiotomatiki kwenye kifaa cha michezo ya video au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Kucheza kiotomatiki katika programu ya YouTube kwenye televisheni yako

Ili kubadilisha mipangilio yako ya Kucheza kiotomatiki katika programu ya YouTube kwenye televisheni yako:

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye televisheni yako.
  2. Nenda kwenye Mipangilio .
  3. Nenda kwenye Kucheza kiotomatiki.
  4. Teua chaguo la Kuwasha au Kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki.

Kucheza kiotomatiki unapotuma kwenye televisheni yako

Ikiwa umeunganisha televisheni yako kwenye simu au kompyuta kibao, unaweza kutumia kifaa chako kudhibiti hali ya Kucheza kiotomatiki.

  1. Unganisha kifaa chako cha mkononi kwenye televisheni yako kisha uchague video ya kucheza
  2. Ili kupanua foleni yako na kuangalia mipangilio yako ya Kucheza kiotomatiki, gusa upau wa kudhibiti katika sehemu ya chini ya skrini.
  3. Tumia swichi kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki.

Swichi ya kucheza kiotomatiki itaonekana chini ya video iliyochaguliwa

Kucheza kiotomatiki kwenye Skrini Mahiri zako zilizo na programu ya Mratibu wa Google

Kuwasha au kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki

Ikiwa unatumia YouTube kwenye Skrini yako Mahiri na ungependa kuwasha au kuzima kipengele cha Kucheza kiotomatiki:

  1. Fungua Programu ya Google Home kwenye kifaa chako cha mkononi.
  2. Gusa Skrini Mahiri ambayo ungependa kuibadilisha.
  3. Gusa Mipangilio.
  4. Gusa Arifa na nidhamu dijitali.
  5. Gusa Mipangilio ya YouTube.
  6. Kuna njia mbili za kudhibiti mipangilio ya Kucheza kiotomatiki kwenye Skrini yako Mahiri:
    • Ikiwa unatumia huduma ya Voice Match, kipengele cha Kucheza kiotomatiki kinaweza kuwashwa au kuzimwa kwa ajili yako; na
    • Kipengele cha Kucheza kiotomatiki kinaweza kuwashwa au kuzimwa kwa watumiaji wengine wote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17928348383955588745
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false