Iwapo umejisajili kwenye YouTube Premium au YouTube Music Premium, manufaa ya uanachama wako yanapatikana kwenye vifaa vyote vinavyoweza kufikia YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu uanachama wetu wa YouTube unaolipiwa.
Kumbuka: Watumiaji wa YouTube Music Premium bado wanaweza kuona matangazo kwenye podikasti.
Vifaa vya mkononi
- Manufaa yote ya YouTube Premium na Music Premium—kama vile video za muziki bila matangazo, uchezaji wa chinichini na zaidi—yanapatikana kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya YouTube pamoja na programu ya YouTube Music.
- Sasisha upate toleo jipya kabisa la programu za YouTube au YouTube Music ili uhakikishe kuwa unaweza kupata manufaa yote ya mtumiaji wa YouTube Premium.
Vifaa vilivyounganishwa kwenye televisheni
Ukiwa mtumiaji wa YouTube Premium, unaweza kutazama video za muziki bila matangazo na YouTube Originals kwenye televisheni yako. Manufaa yako ya YouTube Premium yanapatikana kwenye kifaa chochote cha kutiririsha, televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha michezo ya video ambacho umetumia kuingia katika programu ya YouTube.
Vidokezo:
- Programu ya YouTube Music haipatikani kwenye vifaa vya sebuleni.
- Uchezaji wa chinichini na nje ya mtandao unapatikana tu kwenye programu za vifaa vya mkononi za YouTube, YouTube Kids na YouTube Music. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia manufaa ya YouTube Premium.
- Hakikisha kuwa una toleo jipya kabisa la programu ya YouTube na umeingia katika ukitumia akaunti yako ya YouTube Premium.
Vifaa vya kutiririsha muziki
- Chromecast ya sauti kwenye programu ya YouTube Music: Watumiaji wa Premium wanaweza kucheza faili za sauti katika programu ya YouTube Music kwenye vifaa vya Chromecast ya sauti au spika zilizounganishwa na Google Cast.
Vivinjari vinavyotumika
- Ili utazame video bila matangazo kwenye kivinjari cha kompyuta yako, ingia katika youtube.com au music.youtube.com ukitumia akaunti yako ya kulipia. Pata maelezo kuhusu vivinjari vinavyofanya kazi kwenye YouTube.
Chromecast
Miundo ifuatayo ya Chromecast hairuhusu kuingia moja kwa moja katika YouTube kwenye TV:
- Ultra
- Toleo la tatu
- Toleo la pili
- Toleo la kwanza
Ili kutuma video za YouTube kwenye TV yako ukitumia Chromecast:
- Ingia katika akaunti yako ya YouTube Premium ukitumia kifaa cha mkononi.
- Unganisha kifaa chako na TV yako ukitumia aikoni ya
.
- Tumia kifaa chako cha mkononi kuvinjari na kuchagua video nyingine za YouTube.