Kuzuia upachikaji

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Kwa chaguomsingi, watumiaji wa Kidhibiti Maudhui wanaweza kuongeza video za YouTube kwenye tovuti na programu zao kwa kuzipachika. Unaweza kudhibiti upachikaji wa video zako kwa kuruhusu au kuzuia programu na tovuti utakazobainisha. Vizuizi hivi vinatumika kwa video unazomiliki (Maudhui yenye leseni) na video unazodai (Maudhui yaliyopakiwa na mtumiaji).

Kidokezo: Vizuizi vya upachikaji havitumiki kwa programu za iOS.

Zuia upachikaji kwenye tovuti

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
  3. Katika sehemu ya Muhtasari, nenda kwenye Zuia upachikaji kwenye vikoa.
  4. Bofya Maudhui yaliyopakiwa na mtumiaji kisha uteue vizuizi ambavyo ungependa kutumia kwa tovuti zinazopachika video zilizopakiwa na mtumiaji zinazodaiwa kujumuisha kipengee chako:
    • Ruhusu kwenye vikoa vyote (chaguomsingi): Hakuna vikwazo vya kupachika kwenye tovuti yoyote.
    • Ruhusu kwenye vikoa fulani: Zuia upachikaji kwenye tovuti zote isipokuwa tovuti mahususi ulizoandika kwenye kisanduku cha maandishi cha .
    • Zuia kwenye vikoa fulani: Usiruhusu watumiaji kupachika video kwenye tovuti mahususi ulizoandika kwenye kisanduku cha maandishi cha Vikoa.
    • Zuia kwenye vikoa vyote: Usiruhusu upachikaji wowote wa video kwenye tovuti yoyote.
  5. Weka URL kwenye kisanduku cha maandishi cha Vikoa (URL ya kikoa kimoja kwa kila mstari).
  6. Bofya Maudhui yenye leseni kisha uteue vizuizi ambavyo ungependa kutumia kwa tovuti zinazopachika video kutoka vituo vyako.
  7. Weka URL kwenye kisanduku cha maandishi cha Vikoa (URL ya kikoa kimoja kwa kila mstari).
  8. Bofya HIFADHI.

Zuia upachikaji kwenye programu

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio  .
  3. Katika sehemu ya Muhtasari, nenda kwenye Zuia upachikaji katika programu.
  4. Bofya Maudhui yaliyopakiwa na mtumiaji  kisha uteue vizuizi ambavyo ungependa kutumia kwa programu zinazopachika video zilizopakiwa na mtumiaji zinazodaiwa kujumuisha kipengee chako:
    • Ruhusu katika programu zote (chaguomsingi): Hakuna vikwazo vya kupachika video katika programu yoyote.
    • Ruhusu katika programu kulingana na kitambulisho: Zuia upachikaji katika programu zote isipokuwa programu mahususi unazobainisha kwenye kisanduku cha maandishi cha Vitambulisho vya Programu.
    • Zuia katika programu kulingana na kitambulisho: Usiruhusu watumiaji kupachika video katika programu mahususi unazobainisha kwenye kisanduku cha maandishi cha Vitambulisho vya Programu
    • Zuia katika programu zote: Usiruhusu upachikaji wa video katika programu yoyote.
  5. Weka URL kwenye kisanduku cha maandishi cha Vitambulisho vya Programu (Kitambulisho kimoja cha Programu kwa kila mstari).
  6. Bofya Maudhui yenye leseni  kisha uteue vizuizi ambavyo ungependa kutumia kwa programu zinazopachika video kutoka vituo vyako.
  7. Weka URL kwenye kisanduku cha maandishi cha Vitambulisho vya Programu (URL moja ya Kitambulisho cha Programu moja kwa kila mstari).
  8. Bofya HIFADHI.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
18105686415151790589
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false