Una idhini kamili ya kudhibiti uonyeshaji wa maudhui yako kwenye YouTube na unaweza kutumia idhini hiyo wakati wowote kwa kuondoa maudhui yako. Iwapo una wasiwasi kuhusu upatikanaji wa maudhui yako hasa kwenye YouTube Kids, unaweza kutuma ombi la kuondoa maudhui husika katika kituo chako kwenye YouTube Kids.
Kumbuka kwamba fomu hii inaweza tu kuwasilishwa na aliyepakia maudhui husika. Ili kuthibitisha kwamba wewe ndiwe ulipakia, sharti uingie katika akaunti uliyotumia kupakia video.