Kutumia msimbo wa kuponi

Msimbo wa kuponi wa YouTube ni vocha inayoweza kutumiwa kwa ununuzi au ukodishaji wa filamu au kipindi cha televisheni. Misimbo ya kuponi inaweza tu kutumiwa kwa madhumuni yaliyobainishwa. Kwa mfano, iwapo ulipokea msimbo wa kuponi wa kukodisha filamu, huwezi kuutumia kununua kipindi cha televisheni.

Unaweza kutumia msimbo wa kuponi kwenye kompyuta au kwa kutumia vifaa mahususi vya mkononi.

Ili utumie msimbo wa kuponi kwenye kompyuta:

  1. Tembelea ukurasa wa Vipindi na Filamu au utafute kwenye YouTube filamu au kipindi cha televisheni ambacho ungependa kununua au kukodisha.
  2. Bofya kitufe kinachoonyesha bei ya kununua au kukodisha.
  3. Chagua Weka msimbo wa ofa chini ya bango la filamu au kipindi cha televisheni na uandike msimbo ambao ulipokea.
  4. Teua chaguo la kununua au kukodisha unalopenda.
  5. Sehemu ya bei ya kukodisha au kununua filamu itaonyesha bei iliyosasishwa kulingana na kiasi cha punguzo. Lakini, ni lazima uchague njia sahihi ya kulipa ili upate filamu au kipindi chako cha televisheni kinachotolewa bila malipo. Chagua njia ya kulipa unayopendelea kisha uguse Nunua.

Iwapo unatatizika kutumia msimbo wako wa kuponi kwenye YouTube, jaribu vidokezo vifuatavyo au uwasiliane nasi ili upate usaidizi.

Vidokezo vya kawaida vya utatuzi wa misimbo ya kuponi:

  • Thibitisha kuwa uliweka msimbo wa kuponi katika sehemu inayofaa. Misimbo ya kuponi kwenye YouTube haitafanya kazi katika sehemu ya 'Tumia Kuponi ya Ofa au Kadi ya Zawadi ya Google Play'.
  • Hakikisha kuwa uliweka msimbo kwa njia sahihi. Kuwa makini kuhusu herufi kubwa na ndogo katika msimbo.
  • Hakikisha kuwa unatumia msimbo wa kuponi kwa madhumuni yake yaliyokusudiwa. Kwa mfano, iwapo ulipokea msimbo wa kuponi wa kukodisha filamu au kipindi cha televisheni kinachotolewa bila malipo, huwezi kutumia msimbo huo kununua aina nyingine ya maudhui.
  • Thibitisha kuwa bado msimbo wako wa kuponi unatumika:
    • Angalia tarehe ya mwisho wa matumizi: lazima baadhi ya misimbo ya kuponi itumiwe kabla ya tarehe iliyowekwa. Iwapo una msimbo unaosema 'kwa muda mfupi tu', tarehe ya mwisho wa matumizi itaonyeshwa kwenye msimbo wa kuponi au katika barua pepe uliyopokea.
    • Angalia iwapo msimbo wa kuponi tayari umetumiwa. Msimbo ukishatumika mara moja, huwezi kuutumia tena kupata filamu au kipindi cha televisheni kinachotolewa bila malipo.
  • Thibitisha kuwa umechagua njia sahihi ya kulipa kabla ya kubofya Nunua ili kukamilisha ununuzi au ukodishaji wenye punguzo wa filamu au kipindi cha televisheni.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
150945527922804394
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false