Msimbo wa kuponi wa YouTube ni vocha inayoweza kutumiwa kwa ununuzi au ukodishaji wa filamu au kipindi cha televisheni. Misimbo ya kuponi inaweza tu kutumiwa kwa madhumuni yaliyobainishwa. Kwa mfano, iwapo ulipokea msimbo wa kuponi wa kukodisha filamu, huwezi kuutumia kununua kipindi cha televisheni.
Unaweza kutumia msimbo wa kuponi kwenye kompyuta au kwa kutumia vifaa mahususi vya mkononi.