URL ya Kituo (kulingana na kitambulisho)
Mfano: youtube.com/channel/UCUZHFZ9jIKrLroW8LcyJEQQ
Mfano huu ni URL ya kawaida ambayo hutumiwa na vituo vya YouTube. Hutumia kitambulisho cha kipekee cha chaneli yako, ambacho ni namba na herufi zilizo mwishoni mwa URL.
Pata URL ya utambulisho wako
Ili upate URL ya utambulisho wa chaneli yako:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha Upendavyo
Maelezo ya msingi.
- Kwenye Utambulisho, unaweza kuangalia URL ya utambulisho wako.
URL ya Utambulisho
Mfano: youtube.com/@youtubecreators
URL ya utambulisho hutengenezwa kiotomatiki wakati wowote unapochagua au kubadilisha utambulisho wako kama mmiliki wa chaneli. Mwisho wa URL huanza na alama ya "@" na hujumuisha utambulisho uliochagua. URL zozote maalum ambazo tayari unazo zitaendelea kufanya kazi. Pata maelezo zaidi kuhusu kuangalia au kubadilisha utambulisho wako.
URL Maalum
Mfano: youtube.com/c/YouTubeCreators
Huwezi kuweka mipangilio au kubadilisha URL maalum ambazo ni mpya. URL zozote maalum ambazo tayari unazo zitaendelea kufanya kazi. URL zote zilizopitwa na wakati sasa zinaelekeza watumiaji kwenye URL mpya ya chaneli yako inayotokana na utambulisho wako.
URL ya jina la mtumiaji lililopitwa na wakati
Mfano: youtube.com/user/YouTube
Kulingana na wakati ambao kituo chako kilifunguliwa, kinaweza kuwa na jina la mtumiaji. Majina ya watumiaji hayahitajiki tena kwenye vituo siku hizi, lakini bado unaweza kutumia URL hii kuwaelekeza watazamaji kwenye kituo chako. Hii pia inategemea kama jina la kituo chako limebadilika tangu ulipochagua jina lako la mtumiaji. Majina yaliyopo ya watumiaji hayawezi kubadilishwa.