Kuondoa maudhui yanayopendekezwa kwenye Ukurasa wa Kwanza

Unaweza kuondoa maudhui yanayopendekezwa ambayo hayakuvutii kwenye Ukurasa wako wa Kwanza. Kuondoa video hizi kunaweza kuboresha maudhui unayopendekezewa ili uone video zinazokufaa zaidi.

Kidokezo: Kipengele hiki kinapatikana tu ukiwa umeingia katika akaunti yako.
Jisajili kwenye kituo chetu cha Watazamaji cha YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya!

Kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au katika kifaa chako cha michezo ya video

Kuondoa maudhui yanayopendekezwa kwenye ukurasa wa kwanza

Unaweza kuondoa video zinazopendekezwa kwa kuchagua “Hainivutii” kwenye ukurasa wako wa kwanza, au katika Ukurasa wa Kwanza na Ukurasa wa Tazama Video Inayofuata kwenye kifaa cha mkononi:

  1. Bonyeza na ushikilie kitufe cha kuchagua kwenye kidhibiti chako cha mbali.
  2. Chagua Hainivutii.
  3. Chagua 'Sababu ya kuondoa' ili ueleze ni kwa nini ungependa kuondoa video. Unaweza kuchagua Tayari nimetazama video, Sipendi video, au Usipendekeze kituo ili utusaidie kukupendekezea video zinazokufaa zaidi.

Futa maoni yako ya “Hainivutii" na “Usipendekeze kituo”

Maoni yako ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo” yanaweza kutumika kuweka mapendeleo kwenye mapendekezo yako. Ili ufute maoni yote uliyotoa ya “Hainivutii” na “Usipendekeze kituo”, tafadhali fuata maagizo hapa chini ukitumia kompyuta, Android, au iPhone au iPad yako.

Mapendekezo kutokana na Shughuli zako kwenye Google

YouTube hutumia data inayotokana na Shughuli za Akaunti yako ya Google kukupendekezea video.

Unaweza kuangalia na kudhibiti shughuli zako katika myactivity.google.com. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti shughuli za Akaunti yako ya Google.

Maudhui yafuatayo yanayopendekezwa yanaweza kuondolewa kwenye ukurasa wa kwanza kwenye kompyuta yako:

  • Video
  • Vituo
  • Sehemu
  • Orodha za kucheza

Ikiwa umezima historia ya video ulizotazama kwenye YouTube na huna historia ya kutosha ya video ulizotazama awali, vipengele vya YouTube vinavyotegemea historia ya video ulizotazama kukupa mapendekezo ya video, kama vile mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, huondolewa.

Ikiwa umezima historia ya video ulizotazama kwenye YouTube na huna historia ya kutosha ya video ulizotazama awali, vipengele vya YouTube vinavyotegemea historia ya video ulizotazama kukupa mapendekezo ya video, kama vile mapendekezo kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, huondolewa.
 

Unaweza kuondoa video zinazopendekezwa kwenye Ukurasa wako wa Kwanza na kurasa za Tazama Video Inayofuata kwenye kifaa cha mkononi.

Ondoa video zinazopendekezwa

  1. Nenda kwenye video inayopendekezwa ambayo ungependa kuondoa.
  2. Gusa Zaidi karibu na jina la video.
  3. Gusa Hainivutii .
  4. Chagua Tueleze ni kwa nini ili ushiriki ni kwa nini ungependa kuondoa video. Unaweza kuchagua Nimeshatazama video au Sipendi video ili ufanye mapendekezo yako yakufae zaidi.

Ondoa kituo kinachopendekezwa

  1. Bofya Zaidi  karibu na jina.
  2. Chagua Usipendekeze kituo alama ya kutoa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15506039678780276329
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false