Ufikivu kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya YouTube

Programu ya YouTube ya vifaa vya Android hufanya kazi na vipengele vya ufikivu vya Android. Android hutoa usaidizi wa ufikivu kwa watumiaji vipofu na walio na uwezo mdogo wa kuona kupitia kipengele cha TalkBack na vipengele maalum vya ufikivu. Tembelea Kituo cha Usaidizi cha Ufikivu wa Android ili upate maelezo zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasha mipangilio hii.

 

Kuanza kutumia
Baada ya kuwasha mipangilio yako ya ufikivu ya Android, vipengele vya TalkBack na Chunguza kwa Kugusa vinaweza kukusaidia ugundue maudhui na vipengee katika programu ya YouTube. Angalia maagizo ya kipengele cha Chunguza kwa Kugusa ili upate maelezo zaidi kuhusu vipengele hivi.
Kuvinjari programu

Vichupo vikuu vya programu ni Mwanzo, Chaneli Unazofuatilia na Maktaba. Ingia katika akaunti yako ili uone kichupo cha Chaneli Unazofuatilia.

  • Mwanzo hukuruhusu uvinjari video zinazopendekezwa.
  • Chaneli Unazofuatilia hukuruhusu kupata video kutoka kwenye chaneli unazofuatilia.
  • Maktaba ndiko unakopata historia ya utazamaji, video ulizopakia, ununuzi na orodha zako.

Picha ya wasifu iliyo katika sehemu ya juu ya programu hukuruhusu ufikie mipangilio yako, sera ya faragha ya Google, usaidizi pamoja na kuingia katika akaunti.

Ingia katika akaunti yako kwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Katika sehemu ya juu ya programu, gusa picha yako ya wasifu .
  2. Chagua Ingia katika akaunti.

Ondoka kwenye akaunti yako kwa kufuata hatua hizi:

  1. Katika sehemu ya juu ya programu, gusa picha yako ya wasifu .
  2. Chagua Ondoka kwenye akaunti.
Kuvinjari video na orodha

Tumia kidole kimoja kusogeza kwenye video katika Ukurasa wa Mwanzo , orodha au chaneli. Unaposogeza, utasikia jina la video na metadata inayohusiana nayo.

Chaneli: Kwenye chaneli, tumia vichupo vya Ukurasa wa Mwanzo, Video na Orodha kuvinjari maudhui kwenye chaneli uliyochagua.

Kutafuta video na orodha za video

Ili utafute video ukitumia kipengele cha "Chunguza Kwa Kugusa", gusa sehemu ya juu ya skrini ili upate kitufe cha kutafuta. Kitufe kitakuwa karibu na kipengee cha "Chaguo zaidi".

  1. Gusa mara mbili kitufe cha kutafuta kisha uweke hoja yako ya utafutaji kwenye "kisanduku cha kubadilisha."
  2. Tumia kipengele cha "Chunguza Kwa Kugusa" ili uvinjari matokeo ya utafutaji.
Kucheza na kudhibiti video

Baada ya kupata video ya kucheza, gusa mara mbili ili uanze kuicheza. Ili ufungue vidhibiti vya kichezaji, gusa mara mbili kitufe cha "Kichezaji" kilicho juu ya skrini.

Vidhibiti vya kichezaji na chaguo

Kusitisha: Gusa mara mbili kitufe cha "sitisha video" ili usitishe video.

Kupunguza video: Gusa mara mbili kitufe cha "Punguza" ili upunguze video inapocheza. Ukishapunguza video, unaweza kuvinjari au kutafuta inapoendelea kucheza.

Kuondoa video iliyopunguzwa: Ili uondoe kicheza video kilichopunguzwa, gusa mara mbili kitufe cha "Funga kichezaji kidogo" kilicho upande wa kulia.

Kupanua video iliyopunguzwa: Gusa mara mbili kitufe cha "Kichezaji" kisha utelezeshe juu ukitumia vidole viwili ili upanue kicheza video kilichopunguzwa.

Kuweka kwenye orodha ya video: Gusa mara mbili kitufe cha "Hifadhi video kwenye orodha" ili ufungue arifa ya "Hifadhi video kwenye". Tumia kipengele cha "Chunguza kwa Kugusa" ili uchague orodha ya video. Ili uunde orodha ya video, gusa mara mbili "Orodha mpya ya video."

  • Gusa "Kichwa - Kisanduku cha kubadilisha" ili uipe jina orodha yako ya video.
  • Gusa mara mbili "Orodha kunjuzi - Faragha" ili kufanya orodha yako ya video iwe ya faragha, ya umma, au isiyoorodheshwa.

Chaguo zaidi: Gusa mara mbili kitufe cha “Chaguo zaidi” kilicho katika sehemu ya juu kulia ili upate chaguo hizi.

  • Kubadilisha ubora wa video: Gusa mara mbili kitufe cha "Ubora".
  • Kuripoti video: Gusa mara mbili kitufe cha "Ripoti".
  • Manukuu yenye maelezo: Gusa mara mbili kitufe cha "Manukuu".

Chini ya video, utapata maelezo au vipengele vifuatavyo:

  • Maelezo ya video na metadata.
  • Vitufe vya nimeipenda na sijaipenda.
  • Kitufe cha kufuatilia chaneli.
  • Mapendekezo ya video.
  • Chaguo la kuweka maoni.
  • Maoni kuhusu video.
Video ulizopakia

Ili uende kwenye video ulizopakia katika YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Video zako. Tumia kidole kimoja kusogeza kwenye video ambazo umepakia katika chaneli yako.

Kupakia video

  1. Chini ya skrini, gusa mara mbili kitufe cha "Unda".
  2. Katika upande wa juu wa skrini, gusa mara mbili kitufe cha "Pakia video", kinachopatikana karibu na "Tiririsha mubashara."
  3. Ili upate video ya kupakia, sogeza kwenye matunzio ya picha ya kifaa chako. Gusa mara mbili ili uchague video.
  4. Weka kichwa cha video yako katika kisanduku cha kubadilisha cha "Buni kichwa".
  5. Weka maelezo ya video katika kisanduku cha kubadilisha cha "Weka maelezo".
  6. Chagua kiwango cha faragha (Ya Faragha, Isiyoorodheshwa au Ya Umma) kwenye orodha kunjuzi ya "Faragha".
  7. Katika sehemu ya juu kulia ya kona mwa skrini, gusa mara mbili "Inayofuata."
  8. Teua chaguo sahihi la maudhui "yanayolenga watoto" katikati ya skrini.
  9. Katika kona ya juu kulia mwa skrini, gusa mara mbili "Pakia."

Kuhariri video

Ili uhariri kichwa, maelezo au ubadilishe mipangilio ya faragha ya video:

  1. Tumia vidole viwili kusogeza kwenye video ulizopakia.
  2. Gusa mara mbili kitufe cha "Menyu ya vitendo" kilicho karibu na video ambayo ungependa kuhariri.
  3. Gusa mara mbili kitufe cha "Hariri" kwenye kisanduku cha "Tahadhari" cha video.
  4. Gusa mara mbili visanduku vya kubadilishia kichwa au maelezo au orodha kunjuzi ya "Faragha".
  5. Gusa mara mbili kitufe cha "HIFADHI" kilicho katika kona ya juu kulia ukimaliza kuhariri.

Kufuta video

Ili ufute mojawapo ya video ulizopakia:

  1. Tumia vidole viwili kusogeza kwenye video ulizopakia.
  2. Gusa mara mbili kitufe cha "Menyu ya vitendo" kilicho karibu na video ambayo ungependa kuhariri.
  3. Gusa mara mbili "Futa" kwenye kisanduku cha "Tahadhari" cha video.
  4. Unapoulizwa iwapo ungependa "Kufuta video hii," gusa mara mbili kitufe cha "FUTA" kilicho upande wa kulia.

Kuwasha au kuzima mipangilio ya ufikivu

Ikiwa unaona aikoni ya X kwenye kicheza video, ni kwa sababu umewasha mipangilio ya ufikivu kwenye kifaa chako. Unaweza kuzima mipangilio hii ya ufikivu kwenye kifaa chako cha Android au katika programu ya YouTube.
Kwenye kifaa chako cha Android:
  1. Nenda katika Mipangilio kwenye kifaa chako cha Android .
  2. Gusa Ufikivu.
  3. Teua chaguo husika la ufikivu.
  4. Chagua Zima.

Katika programu yako ya YouTube:

  1. Katika sehemu ya juu ya programu, gusa picha yako ya wasifu .
  2. Chagua Mipangilio .
  3. Chagua Ufikivu.
  4. Ikiwa ungependa kubatilisha mpangilio kwenye kifaa cha Android, zima "Kichezaji cha Ufikivu."
  5. Unaweza pia kuweka kipima muda ili ufiche kiotomatiki vidhibiti vya kicheza video baada ya sekunde X.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
15832876382769433167
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false