Kubadilisha orodha za kucheza

Unaweza kuongeza au kubadilisha majina na maelezo, kupanga upya video au kuondoa video kwenye orodha ya kucheza.

Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.

Kuweka maelezo ya orodha ya video

  1. Kwenye kompyuta yako, chagua orodha ya video kwenye Mwongozo wako .
  2. Bofya Badilisha kisha Weka maelezo na uweke maelezo kuhusu orodha yako ya video.
  3. Ili uhifadhi, bofya kisanduku cha kubadilishia.

Kubadilisha jina au maelezo ya orodha ya video

  1. Kwenye kompyuta yako, chagua orodha ya video kwenye Mwongozo wako .
  2. Bofya Badilisha , kisha ubofye jina au maelezo ya orodha yako ya video na ubadilishe inavyohitajika.
  3. Bofya Nimemaliza.

Kupanga upya maudhui kwenye orodha ya video

  1. Chagua mojawapo ya orodha zako za video.
  2. Bofya na ushikilie  karibu na kijipicha cha Video fupi au video.
  3. Buruta video au Video fupi juu au chini ili upange upya orodha ya video.

Kuchuja orodha yako ya video kulingana na aina ya video

  1. Chagua orodha ya video ambayo ungependa kubadilisha kwenye Mwongozo.
  2. Chagua chipu iliyo na aina ya maudhui ambayo ungependa kutazama katika orodha yako ya video:
    1. Yote: Huonyesha maudhui yote yaliyohifadhiwa kwenye orodha ya video.
    2. Video Fupi: Huonyesha Video Fupi zilizohifadhiwa kwenye orodha ya video.
    3. Video: Huonyesha video ndefu zilizohifadhiwa kwenye orodha ya video.

Kuondoa maudhui kwenye orodha ya video

  1. Fungua orodha ya video.
  2. Bofya Zaidi '' karibu na video au Video fupi ambayo ungependa kuondoa.
  3. Bofya Ondoa kwenye [PLAYLIST NAME].
Iwapo huwezi kufuata maagizo haya, huenda unatumia toleo la zamani la YouTube. Iwapo unatumia kivinjari kipya zaidi, sasisha utumie toleo jipya la YouTube.
Unaweza pia kubadilisha orodha zako za video ukitumia programu ya Studio ya YouTube kwenye kifaa chako cha mkononi. Anza kutumia kwenye Kituo cha Usaidizi cha programu ya Studio ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8818487993206953012
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false