Mwongozo wa kuunda lahajedwali

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Unaweza kutayarisha lahajedwali la uwasilishaji kwenye YouTube kwa kutumia programu yoyote ya lahajedwali inayotumia usimbaji wa maandishi wa UTF-8. Ili uhakikishe unawasilisha maudhui kikamilifu, unahitaji kuhifadhi faili kwa kutumia usimbaji wa UTF-8. Si programu zote za lahajedwali huhifadhi katika muundo huu kwa chaguomsingi.

Microsoft Excel katika kompyuta za Macintosh haitumii usimbaji wa UTF-8. Iwapo metadata yako inajumuisha herufi zozote zisizo za Kilatini, tumia programu tofauti ya lahajedwali kama vile Majedwali ya Google.

Safu mlalo ya kwanza kwenye lahajedwali huorodhesha safu wima unazowekea thamani ya data, zikitenganishwa kwa mikato. Majina ya safu wima yanahitaji kulingana na majina yanayoonekana kwenye kiolezo cha lahajedwali. Yanaweza kuonekana katika mpangilio wowote, ilimradi kila safu mlalo inatumia mpangilio mmoja. Unaweza kuondoa safu wima yoyote isiyo ya lazima ambayo huitumii kuweka data.

Kila safu mlalo inayofuata kwenye lahajedwali hutumika kuweka thamani za metadata za kipengee kimoja kinachowasilishwa. Thamani zinazotenganishwa kwa mkato lazima ziwe katika mpangilio mmoja kama orodha ya safu wima kuanzia kwenye safu mlalo ya mwanzo. Kila safu mlalo lazima ionekane katika mstari mpya.

Kanuni za kuunda sehemu za kuweka metadata

  • Thamani ya sehemu ya metadata inaweza kujumuisha herufi zozote za UTF-8. Mabano yenye ncha kali (< au >) hayaruhusiwi kutumika katika majina au maelezo ya video.
  • Iwapo thamani ina koma zilizopachikwa, weka thamani yote ndani ya alama mbili za kunukuu. (Unaweza kuweka thamani zote ndani ya alama mbili za kunukuu iwapo unahitaji.)
  • Iwapo thamani ina herufi zilizopachikwa zenye alama mbili za kunukuu, weka herufi mbili zenye alama mbili za kunukuu ndani ya herufi zenye alama mbili za kunuku.
  • Ili uweke orodha ya thamani, tenganisha thamani binafsi ukitumia alama ya upau wa wima ().
  • Herufi zenye nafasi nyeupe zilizotangulia au kufuata zitaondolewa.
  • Sehemu zote zinahitaji kuwekwa katika muundo wa maandishi dhahiri, ikiwa ni pamoja na sehemu ambazo thamani zake ni tarehe au zenye nambari za kipekee.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8957163688270514459
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false