Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Kuanzisha kampeni

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Katika Kidhibiti Maudhui cha Studio, kampeni hukupa njia ya kutangaza maudhui yako moja kwa moja kwenye video zilizopakiwa na watumiaji zinazolingana na maudhui yako. Hususan, kipengee kikiwa sehemu ya kampeni, kadi ya utangazaji huwekwa kwenye video zilizopakiwa na watumiaji zinazolingana na faili ya marejeleo ya kipengee hicho. Kadi hii huwaunganisha watazamaji moja kwa moja na maudhui yako.

Unaweza kutumia kampeni kutangaza video mahususi ya kikundi cha vipengee, kama vile kuunganisha kwenye ukurasa wa kutazama wa filamu yako, video iliyopakiwa na watumiaji ikiwa na matukio kutoka kwenye filamu yako.

Maudhui yanayolingana yanabainishwa kwa Content ID au mchakato wa kudai mwenyewe. Kwa madai ya Content ID, kadi huonekana sehemu ya maudhui inayolingana inapoanza. Kwa michakato ya kudai mwenyewe, kadi huonekana video inapoisha. Kumbuka kuwa kadi hazionekani ikiwa video inayolinganishwa haiwezi kuchezwa kwenye YouTube. Kadi pia hazionekani ikiwa kipande cha video inalingana kwa muda mfupi.

Kuanzisha kampeni

Ili uanzishe kampeni, kwanza unapaswa kuamua jinsi unavyotaka vipengee vilivyo kwenye kampeni yako vibainishwe, iwe kwa kipengee au kwa lebo ya kipengee:

  • Kampeni zinazotumia kipengee zinategemea vipengee vilivyochaguliwa kibinafsi.
  • Kampeni zinazotumia lebo zinategemea vipengee vilivyowekewa lebo maalum ya vipengee.

Kidokezo: Tunapendekeza uanzishe kampeni zinazotumia lebo inapowezekana kwa sababu ya manufaa haya:

  • Vipengee visivyo na kikomo: Kampeni zinazotumia lebo zinaweza kutumika kwenye idadi ya vipengee isiyo na kikomo, ambapo kampeni zinazotumia vipengee zinaweza kutumia vipengee visivyozidi 25.
  • Vya maalum zaidi: Ukiwa na kampeni zinazotumia lebo, unaweza kuanzisha kampeni kwa urahisi kulingana na mandhari mahususi.
  • Masasisho ya kiotomatiki: Lebo ya vipengee ikiwa sehemu ya kampeni, vipengee vyovyote vipya vilivyo na lebo hiyo vitajumuishwa kiotomatiki kwenye kampeni.

Kuanzisha kampeni kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kampeni .
  3. Bofya KAMPENI MPYA kisha chagua mbinu ya kutambulisha vipengee katika kampeni yako:
    • Kampeni inayotegemea kipengee
    • Kampeni inayotegemea lebo
  4. Kwenye kisanduku cha Jina la kampeni, weka jina la kampeni yako.
  5. Kwenye kisanduku cha Video inayoangaziwa, weka URL kamili ya video unayotaka kutangaza.
  6. Bofya Tarehe ya Kuanza  kisha uchague tarehe ambayo unataka kampeni yako ianze.
  7. Bofya Tarehe ya Kumalizika  kisha uchague tarehe ambayo unataka kampeni yako imalizike.
  8. Chagua vipengee au lebo za vipengee ili uziweke kwenye kampeni yako:
    • Kwenye Kampeni zinazotegemea kipengee:
      • Bofya WEKA VIPENGEE.
      • Bofya kisanduku cha kuteua karibu na vipengee ambavyo ungependa kuweka kwenye kampeni yako (hadi vipengee 25).
      • Bofya CHAGUA VIPENGEE # KATI YA 25. (# inawakilisha idadi ya vipengee ulivyochagua).
    • Kwenye Kampeni zinazotegemea lebo:
      • Bofya kisanduku cha Lebo za vipengee.
      • Weka jina la lebo ya kipengee ili utafute lebo ya kipengee iliyopo au uunde lebo mpya.
      • Bofya jina la lebo ya vipengee ili uiweke kwenye kampeni yako.
  9. Bofya HIFADHI.

Vidokezo:

  • Washirika wa lebo za muziki pekee ndio wanaweza kuanzisha kampeni kulingana na kipengele cha sauti cha marejeleo.
  • Unaweza kuanzisha zaidi ya kampeni moja kwa ajili ya vikundi tofauti vya vipengee.
  • Unaweza kuanzisha hadi kampeni 5000 kwa kila akaunti ya Kidhibiti Maudhui.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5109682529397797880
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false