Kutumia manufaa yako ya YouTube Premium

YouTube Premium ni uanachama unaolipiwa unaoboresha hali yako ya utumiaji kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya Premium hapa chini au uvinjari ofa kwa wanachama wa Premium.

Kutazama video bila matangazo

Kupitia YouTube Premium, unaweza kutazama mamilioni ya video bila kukatizwa na matangazo kabla na wakati video inacheza, ikiwa ni pamoja na matangazo yanayowekwa juu ya video. Hutaona pia matangazo ya mabango ya wengine na matangazo ya utafutaji.

Huenda bado ukaona chapa au matangazo yaliyopachikwa katika maudhui na mtayarishi na viungo vya matangazo, rafu na vipengele katika na karibu na maudhui ambayo yanawekwa au kuwezeshwa na mtayarishi. Viungo, rafu na vipengele hivi vinaweza kuwa vya tovuti yake, bidhaa, uanachama kwenye kituo chake, tiketi za matukio, au maeneo mengine yanayohusiana ambayo anatangaza.

Video zisizo na matangazo zinaruhusiwa kwenye vifaa na mifumo yote ambako unaweza kuingia katika Akaunti yako ya Google—ikiwa ni pamoja na kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti au vifaa vya michezo ya video vinavyoruhusiwa na programu za vifaa vya mkononi za YouTube, YouTube Music, YouTube Kids, iwapo zinapatikana mahali ulipo.

YouTube Music Premium inatoa hali sawa ya utumiaji inayokuruhusu ufurahie maudhui ya muziki katika programu ya YouTube Music bila matangazo.

Kupakua video utazame nje ya mtandao

Pakua video na orodha za kucheza ili utazame nje ya mtandao wakati hujaunganishwa kwenye intaneti. Unaweza kupakua video ili utazame nje ya mtandao kwa kutumia programu ya YouTube, kupakua nyimbo ili usikilize nje ya mtandao kwa kutumia programu ya YouTube Music na kutazama video zilizopakuliwa kiotomatiki katika programu ya YouTube Kids.

Kupitia kipengele cha Upakuaji wa Kiotomatiki, maudhui yanayopendekezwa huwekwa kiotomatiki kwenye maktaba yako ili utazame au usikilize nje ya mtandao. Furahia video popote ulipo na ugundue maudhui mapya bila ugumu wa kutafuta. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti au kuzima kipengele chako cha Upakuaji wa Kiotomatiki.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium, YouTube Music Premium

Uchezaji wa chinichini

Cheza video kwenye kifaa chako cha mkononi huku ukitumia programu nyingine au wakati skrini yako imezimwa. Kipengele cha uchezaji wa chinichini kinapatikana kwenye programu za vifaa vya mkononi za YouTube, YouTube Music na YouTube Kids (iwapo programu hizi zinapatikana mahali uliko) wakati umeingia kupitia akaunti ya uanachama wako wa YouTube Premium.

Kuweka mapendeleo au kuzima kipengele cha uchezaji wa chinichini

Kipengele cha Uchezaji wa Chinichini kinapatikana kwenye programu za vifaa vya mkononi za YouTube wakati umeingia ukitumia akaunti ya uanachama wako wa YouTube Premium. Kwa chaguomsingi, video zitacheza chinichini.

Ili ubadilishe au uzime kipengele cha uchezaji wa chinichini:

  1. Nenda kwenye Mipangilio .
  2. Chagua Uchezaji wa Chinichini chini ya "Chinichini na Vipakuliwa."
  3. Teua chaguo lako:
    • Usizime kamwe: Video zitacheza chinichini (mipangilio chaguomsingi).
    • Imezimwa: Video hazitawahi kucheza chinichini.
    • Vipokea sauti vya kichwani au spika za nje: Video zitacheza tu chinichini iwapo kifaa chako kimeunganishwa kwenye vipokea sauti vya kichwani, spika au vifaa vya nje vya sauti.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium, YouTube Music Premium

YouTube Music Premium

Unaweza pia kufikia YouTube Music Premium kama sehemu ya manufaa yako. Ukiwa na YouTube Music Premium, unaweza:

  • Kufurahia mamilioni ya muziki na video katika YouTube Music bila matangazo.
  • Kupakua nyimbo na video kwenye kifaa chako cha mkononi ili usikilize nje ya mtandao.
  • Kutumia huduma ya uchezaji wa chinichini ili uendelee kucheza muziki unapotumia programu nyingine.
  • Kuwasha hali ya sauti pekee ili usikilize muziki bila kupakia video.
Endelea kutazama

Kupitia uanachama wako wa Premium, unaweza kuendelea kutazama video ulikoachia ili upate hali ya utazamaji bila kukatizwa.

Ukiacha kutazama video, tutahifadhi sehemu uliyoachia ili uweze kuendelea kutazama video hiyo kwenye vifaa vingi.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium

Badilisha uchezaji kupitia vidhibiti vya Premium

Kupitia uanachama wa Premium, unaweza kufanya shughuli nyingi na kufurahia video kwa kasi yako kupitia vidhibiti vya Premium. Ruka maudhui, badilisha kasi ya uchezaji wako na zaidi.

Ili ufikie vidhibiti vya Premium kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya YouTube:

  1. Fungua video katika akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
  2. Gusa Mipangilio Settings.
  3. Bofya Mipangilio ya ziada
  4. Chagua Vidhibiti vya Premium

Video yako itafungua menyu kubwa ya vidhibiti, ambako unaweza:

  • Kucheza, kusitisha, au kuruka video.
  • Kuruka mbele au nyuma ndani ya video kwa sekunde +/- 10.
  • Kupenda video.
  • Kuhifadhi video ili utazame baadaye.
  • Kubadilisha kasi ya uchezaji wako.
  • Kuwasha au kuzima kipengele cha kiwango thabiti cha sauti

Vidhibiti vya Premium vinapatikana kwenye Android, iPhone na vishikwambi, lakini bado havipatikani kwenye kompyuta za mezani.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium, YouTube Music Premium

Kupachika Picha Ndani ya Picha Nyingine (PiP)

Kipengele cha kupachika picha ndani ya picha nyingine (PiP) kinakuruhusu utazame video huku ukitumia programu nyingine kwenye kifaa chako cha mkononi.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia kipengele cha kupachika picha ndani ya picha nyingine kwenye kifaa chako cha mkononi.

Upatikanaji:

  • Watumiaji wa Premium (Android/iOS): Video za muda mrefu (na Video Fupi kwenye Android).
  • Watumiaji wanaoonyesha matangazo nchini Marekani: Video ndefu (bila kujumuisha maudhui fulani kama vile video za muziki).
  • Watumiaji wanoonyesha matangazo nje ya Marekani: kipengele cha Kupachika Picha Ndani ya Picha Nyingine hakipatikani.

Weka video katika foleni kwenye vifaa vya mkononi na vishikwambi

Weka mipangilio ya video zitakazocheza bila kukatiza video unayotazama. Kipengele cha kuweka video katika foleni kwenye kompyuta kibao na vifaa vya mkononi kinapatikana kwenye YouTube Premium pekee.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium

Kubadilisha ubora wa video yako

Ukiwa na YouTube Premium, unaweza kutazama video katika 1080p Premium.

1080p Premium ni toleo lililoboreshwa la kasi ya biti ya 1080p. Kasi ya biti iliyoboreshwa hutoa maelezo zaidi kwa kila pikseli na kukupatia hali ya utazamaji yenye ubora wa juu zaidi. Video zinaweza tu kutumia kasi ya biti iliyoboreshwa ikiwa zilipakiwa katika ubora wa 1080p. Hutapata chaguo la 1080p Premium kwenye:

  • Mitiririko Mubashara
  • Video Fupi
  • Video zilizopakiwa katika ubora wa juu au wa chini kuliko 1080p

Ili kukupa hali bora ya utazamaji, YouTube hubadilisha ubora wa video unayotiririsha kulingana na hali zako za utazamaji. Ikiwa una uanachama wa Premium, huenda ubora wa video zako ukawekwa kuwa 1080p Premium kiotomatiki. Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya ubora ndani ya Programu ya YouTube.

Hupatikana kwenye: YouTube Premium

Beji za Premium

Beji zinazohusishwa na mwenyeji wa Premium hutuza watumiaji kwa uaminifu wao, huku Beji za manufaa zikiwatuza watumiaji kwa uaminifu wao. Unaweza kupata beji kwa kuwa mwenyeji wa muda mrefu zaidi na kwa kujihusisha ukitumia Manufaa ya Premium (k.m. Hafla ya ziada, YouTube Music, Endelea kutazama). Kwa sasa manufaa haya yanapatikana kwa watumiaji walio na miaka zaidi ya 18.

Unaweza kupata Beji za Premium kwenye ukurasa wako wa Manufaa ya Premium katika akaunti yako ya YouTube.

Ili upate Beji zako za Premium:

  1. Fungua programu ya YouTube
  2. Nenda kwenye ukurasa wako wa kwanza
  3. Gusa aikoni ya picha yako ya wasifu 
  4. Bofya Manufaa Yako ya Premium
  5. Nenda chini ya ukurasa huo ili uangalie Beji zako za Premium

Kwa kubofya beji yoyote iliyofungwa, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata beji hiyo

Kumbuka

  • Kusitisha historia ya video ulizotazama kutazuia watazamaji dhidi ya kupata beji zinazohusiana na Manufaa Yako ya Premium (k.m. Hafla ya ziada, YouTube Music, Endelea kutazama). 
  • Kubadilisha historia ya video ulizotazama kutaondoa beji ulizopata awali zinazohusiana na Manufaa Yako ya Premium. 
  • Kughairi Premium kunamaanisha watumiaji hawataweza kufikia tena ukurasa wa Manufaa Yako ya Premium ambapo beji zinahifadhiwa. 
  • Kukubali kuhifadhi nakala ya Premium, huwezesha watumiaji kuona beji walizopata awali.

Manufaa mengine ya Premium

Kama mwanachama wa YouTube Premium, utakuwa na uwezo wa kufikia vipengele vingine vya wanachama pekee, ikiwa ni pamoja na:

Kumbuka: Baadhi ya vipengele hivi vinatumika tu katika maeneo, vifaa na mipango mahususi. Mara kwa mara tunaongeza vipengele vipya ili kuboresha hali yako ya utumiaji wa YouTube Premium, ambavyo unaweza kupata maelezo kuvihusu kwenye ukurasa wetu wa Masasisho ya Premium.
Vidokezo:

Jisajili ili ufurahie manufaa ya Premium

Ili ufurahie manufaa ya Premium, jisajili katika youtube.com/premium.

Jinsi ya kupata YouTube Premium au YouTube Music Premium

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kumbuka: YouTube TV, vituo vya Primetime, uanachama katika kituo na NFL Sunday Ticket hazijumuishwi kwenye manufaa ya YouTube Premium au Music Premium.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9718983685312991864
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false