Masharti ya arifa za ukiukaji wa hakimiliki: Video

Kidokezo: Njia rahisi zaidi ya kuomba kuondolewa kwa video unayoamini kuwa inakiuka hakimiliki yako ni kwa kutumia fomu yetu ya wavuti.

Ili kuomba kuondolewa kwa maudhui yasiyo ya video, kama vile picha za bango la chaneli, ombi lako lazima lijumuishe maelezo haya yanayohitajika.

Ili kuomba arifa ya ukiukaji wa hakimiliki kwa video, lazima utoe maelezo yanayohitajika yaliyoorodheshwa hapa chini. Bila maelezo haya, hatuwezi kuendelea kushughulikia ombi lako.

Unaweza kuwasilisha maelezo yaliyo hapa chini kwenye maudhui ya barua pepe (si kwenye kiambatisho) kwa copyright@youtube.com au kupitia faksi au barua.

1. Maelezo yako ya mawasiliano

YouTube na aliyepakia maudhui unayoomba yaondolewe wanaweza kuhitaji kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako. Kwenye ombi lako, jumuisha mojawapo ya mambo yafuatayo:

  • Anwani yako ya barua pepe
  • Anwani yako ya mahali halisi
  • Namba yako ya simu

2. Maelezo ya maudhui yako yaliyo na hakimiliki

Kwenye ombi lako, hakikisha unaeleza kwa uwazi zaidi na kwa ukamilifu maudhui yako yaliyo na hakimiliki unayojaribu kulinda.

Ikiwa unaamini zaidi ya kazi yako moja iliyo na hakimiliki imekiukwa, sheria inaruhusu ujumuishe orodha wakilishi ya kazi hizo kwenye ombi lako.

3. URL maalum za video husika

Ombi lako lazima lijumuishe viungo maalum vya kuelekeza kwenye video unayoamini/unazoamini kuwa zinakiuka haki zako. 

Jumuisha URL ya/za video husika katika muundo ufuatao:
 
www.youtube.com/watch?v=xxxxxxxxxxx

Maelezo ya jumla kama vile jina la chaneli au URL ya chaneli hayatoshi.

4. Kubali na ujumuishe taarifa mbili zifuatazo:

“Ninaamini kwa nia njema kuwa matumizi ya nyenzo kwa namna iliyolalamikiwa hayajaruhusiwa na mwenye hakimiliki, wakala wake au sheria.”

"Maelezo yaliyo kwenye arifa hii ni sahihi, na nitaadhibiwa kwa kusema uwongo, mimi ni mmiliki au mwakilishi rasmi niliyeidhinishwa kutenda kwa niaba ya mmiliki wa haki ya kipekee inayodaiwa kukiukwa.”

5. Sahihi yako

Maombi ya uondoaji yaliyokamilishwa yanahitaji sahihi halisi au ya kielektroniki ya mwenye hakimiliki au mwakilishi rasmi aliyeidhinishwa kutenda kwa niaba yake.

Ili kutimiza masharti haya, mwenye hakimiliki au mwakilishi rasmi aliyeidhinishwa anaweza kuweka jina lake rasmi kamili kama sahihi yake katika sehemu ya chini ya ombi. Jina rasmi kamili linapaswa kuwa jina la kwanza na la mwisho, si jina la kampuni.

Jumuisha maelezo ya hapo juu kwenye maudhui ya barua pepe (si kwenye kiambatisho) kwa copyright@youtube.com. Unaweza pia kuwasilisha ombi lako kupitia faksi au barua.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11704799002311336562
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false