Iwapo unakumbwa na matatizo ya video au sauti kwenye video uliyopakia, jaribu hatua hizi za utatuzi ili upate suluhisho.
Matatizo ya sauti
Sauti na video haviendani
Hakikisha kwamba urefu wa vipande vya video na sauti vinalingana. Ikiwa kipande chako cha sauti ni kifupi au kirefu zaidi ya video yako, huenda sauti na video visiendane kwa usahihi.
Ili uhariri vipande vyako vya sauti na video, tumia programu ya kuhariri video kabla ya kupakia maudhui yako kwenye YouTube.
Sauti inacheza kwenye kompyuta lakini si kwenye kifaa cha mkononi
Hatua ya kubadilisha mipangilio ya video inaweza kutatua matatizo ya kawaida ya video na sauti. Ili ukague na kubadilisha mipangilio ya video yako:
Fungua video hiyo kwenye programu ya kuhariri video
Ili ufungue video ghafi yako, tumia programu ya kuhariri video kwenye kompyuta. Iwapo ulirekodi video yako kwenye kifaa cha mkononi, unaweza kuifungua kupitia programu ya kuhariri ya kifaa cha mkononi.
Thibitisha mipangilio ya video
Katika kihariri chako cha video, hakikisha kwamba mipangilio ya video yako inalingana na mipangilio yetu ya upakiaji inayopendekezwa.
- Aina ya Mbano: H.264
- Kasi ya Picha: kasi ya picha 24, 25, 30, 48, 50, 60 kwa sekunde (FPS) ndivyo viwango vinavyopendelewa. Kasi nyinginezo za picha zisizotumika mara nyingi kama vile 23.98, 29.97 na 59.94 pia zinakubalika.
- Kiwango cha Data: Kiotomatiki
- Fremu Muhimu: Kiotomatiki
- Upangaji Upya wa Fremu: Haijachaguliwa
- Muundo: AAC-LC
- Kasi ya biti: kbps 128 hadi kbps 256
- Kasi cha sampuli: 44100 au 48000
- Ukubwa: Chagua ukubwa halisi wa video.
Kuhifadhi na kuhamisha
Baada ya kuweka mipangilio inayopendekezwa katika video, ipakie tena kwenye YouTube.
Matatizo ya video
Video mpya haziwezi kuchezwa katika ubora wa juu zaidi (4K, 1080p)
Unapopakia video, kwanza itachakatwa kwa ubora wa chini. Hatua hii inakusaidia kukamilisha utaratibu wa kupakia video kwa haraka zaidi. Machaguo ya ubora wa juu zaidi, kama vile 4K au 1080p, yanaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuchakatwa. Wakati uchakataji huu unaendelea, huenda video yako ikaonekana haina machaguo ya ubora wa juu kwa saa kadhaa.
Iwapo ungependa video mpya unazopakia zipatikane na machaguo yote ya ubora wa video, jaribu kwanza kupakia video yako ikiwa haijaorodheshwa. Baada ya machaguo yote ya ubora wa video kupatikana unaweza kuifanya video yako ipatikane kwa umma. Pata maelezo zaidi kuhusu ubora wa video kwa upakiaji mpya wa video.
Kumbuka:Ubora wa juu zaidi kama vile 4K huenda usipatikane kwenye vifaa au vivinjari mahususi kutokana na vizuizi vya mfumo.
Rangi hazionyeshwi kwa usahihi
Ikiwa rangi hazionekani kwa usahihi, hakikisha kwamba sifa za uhamishaji wa rangi za video yako, rangi za msingi na metadata ya solo ya kizidishi cha rangi vinalingana na jinsi video ilivyotayarishwa.
- Video zisizo za HDR: Tumia BT.709
- Video za HDR: Pata maelezo zaidi
Iwapo bado rangi hazionekani kwa usahihi, huenda ikatokana na kivinjari au kifaa chako. Ili ufahamu chanzo cha tatizo, jaribu kucheza video yako halisi na uliyopakia kwenye YouTube katika vivinjari vinginevyo.